Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Ni ukweli usiopingika nderingosha, meningitis kuwa kwa sasa watamzania tunapaswa kuangalia shida kuu zinazotufanya tudorore na kuwa hapa. Nionavyo mimi miongoni mwa matatizo yetu makubwa kwa sasa ni matumizi ya sheria. Katiba tuliyonayo ina mapungufu lakini mapungufu yanazidishwa na utawala wa kutotumia hata hicho kikamilifu kidogo kilichopo. Na tutambue kuwa nchi yeyote duniani ukisikia inaendelea cha mwanzo ni kujenga nidhamu ambayo mwangalizi na msimamizi mkuu ni SHERIA. Hivyo ni muda muafaka wa kuwa na kiongozi anayejua sheria na mkamilifu wa kuisimamia. Hata haya ya UFISADI, MIKATABA, MADAWA YA KULEVYA, UONEVU TOKA VYOMBO VYETU VYA ULINZI NA UALAMA, KUBAMBIKIANA KESI, N.K hata katiba tuliyonayo ingeweza kuyakabili kwa kiasi kikubwa tatizo ni MSIMAMIZI WA SHERIA.
Tatizo la pili ni muelekeo wa uchumi wetu. Baada ya sheria kuleta nidhamu, litaibuka la pili vipato vyetu vitufikishe wapi? Hapa linakuja suala la kuwa na kiongozi wa juu ambaye ni mzalendo na mchumi. Tanzania tuna rasilimali za kutosha, zikisimamiwa na mchumi mzuri zinaweza kutuletea maendeleo ndani ya muda mfupi sana. Chukulia upande wa mapato tunayopoteza kupitia mikataba katika sekta ya madini. Hii pekee ikisimamiwa inaweza kuongeza zaidi ya nusu ya bajeti ya nchi.
Kwa kusema hivyo ni muda muafaka wa UKAWA kujipanga na kutuletea kiongozi wa juu mathalani Rais mzuri ktk sheria (TL) na PM awe kiongozi mwenye msimamo thabiti (SLAA) na waziri atakayehusika na masuala ya uchumi / fedha / viwanda awe ni mchumi (Prof. Lipumba). Ushaur kwa sasa ni huo, kwa hizo nafasi chache za juu.




...wazi kabisa....Labda zaidi angalizo muhimu kwa UKAWA..haswa viongozi wao wa juu ni kutokua wabinafsi....na pia kuwa flexible kwenye kuchagua wagombea wao wa urais bara na visiwani....

...Kwa ushauri tu...ningependa sana kuona wazee makini kama kina Dr.Slaa na Prof.Lipumba wanagombea ubunge katika majimbo hata ya hapa dar ili waingie bungeni(mfano wagombee kupitia K'ndoni ama Ilala/temeke)...na nina hakika wakifanya hivyo watapita...na wakiwa bungeni wataongeza viti upinzani na pia watapata nafasi za juu za uongozi wa taifa hili pale UKAWA watakapopata dola....Tukumbuke pia kuna nafasi nyeti kama ya waziri mkuu..ama waziri wa fedha ambazo zimetumika vibaya na zimechangia sana kuliangamiza taifa hili na hivyo zinahitaji watu makini kama wazee hawa....

...Pia viongozi wa UKAWA watambue kuwa sasa hivi wapiga kura wengi wa taifa hili ni vijana na wataangalia sana ni vijana gani watapitishwa kugombea nafasi hizi za juu...Na kwa maana hiyo uteuzi wa mtu kama Lissu ni muafaka sana kwa wakati huu tete....

....Tunapojadili teuzi hii ya urais tusisahau pia kule Zenj....maana nako ni sehemu ya taifa hili..hivyo suala la mgombea mwenza kwa mtu kama Lissu nalo ni muhimu kulijadili....Na kwa muono wangu mtu makini naeona angegombea kwa mafanikio makubwa na Lissu(kama ikitokea hivyo)ni yule kijana makini Ismail Jussa...vijana hawa walionyesha umahiri mkubwa katika bunge la katiba katika kupigania hoja zao....hawa jamaa ni vichwa na hadhina kubwa ya TZ....

...Kwa urais wa zenj....Mkuu Maalim Seif anawaweza kabisa ccm..maana hata urais wa 2010 alishinda yeye na akapokwa urais na ccm kwa hila.....


...Mwisho....NI vema sana UKAWA wakawa makini na kupokea mafisadi/wagombea urais watakaotoswa huko ccm....Hawa hawafai UKAWA kama kweli wanataka kujenga imani kwa watanzania....Wasiwakubali kabisa kabisa mafisadi watakaotemwa ccm....maana hata sasa UKAWA wamefika hapa bila hao mafisadi...Ila ni vema pia UKAWA wakawa open kuwapokea watu makini watakaotemwa kwa hila huko ccm....maana wapo watu makini(wachache)ccm ambao huko ccm hawapendwi kwa misimamo yao na wanaweza kutemwa kwa hila....mfano kama ilivyokua kwa kina Mansour Himidi...
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi habarini!

Niliweka post hivi majuzi na kuahidi kurudi tena na kuelezea kwa nini nimeamua kushawishi umma wa Tanzania ya kwamba TANZANIA ya leo inamuhitaji Tundu Lissu kama mwajiriwa mkuu wa wananchi.

wakati umefika na wakati ndio huu!

Utangulizi:

Nikijikita katika mada moja kwa moja napenda kusema kuwa Tanzania ya leo sio Tanzania ya Nyerere,hapa namaanisha sio Tanzania yenye maadui watatu yaani Ujinga,Umasikini na Maradhi...maadui hawa walishadhibitiwa usiniulize lini au na nani bali tulie tuelezane.

Watanzania wa leo wana elimu bwana...watu wanatumia simu,TV na teknolojia za kigeni bila shida.elimu ya msingi kwa sasa ni kidato cha nne,maelfu kwa maelfu ya vijana wako vyuo vikuu.hivyo sitarajii kumsikia mtu akilalamika juu ya watanzania kupata elimu iwe bora au hiyo hiyo ya kuungaunga...Adui alikuwa ni upatikanaji wa elimu na sio ubora wake!!!

Swali la kujiuliza jee elimu hii wanayopata vijana wetu hasa ile asilimia 75 ya wakulima na labda kwa kuongezea asilimia 10 ya wafugaji inafanana na ile wanayopata asilimia chini ya kumi ya tabaka la viongozi/masingasinga na washirika wao?

Hivi hii elimu waliyopewa watoto wa mbwa imelenga kuajiriwa au kujiajiri?

Watanzania wa leo sio maskini bwana.mabarabara ya lami kila kona,umeme vijijini wa kuwasha taa tu(wanakijiji wataanza kuchelewa kulala).Watu wanamiliki simu,toyo na mafundi cherehani wa sikuhizi hawajui kuweka viraka.Ukiongelea msosi hii sio issue tena kwani siku hizi hakuna kupanga foleni ya mkate huku kuna skonzi za Azam.

Umasikini hakuna tena...naam

Watanzania wa leo hawaumwi kipindupindu,Ukoma,vikope n.k watanzania wa leo wanaumwa dengue,B.P na rare cases kansa ya Tezi....
Isitoshe kuna zahanati au kituo cha kutoa huduma za afya kila kijiji.Adui alikuwa ni upatikanaji wa huduma za afya sasa zipo.

Jiulize sasa huduma hizi za hospitali hata ile zahanati kuu ya Muhimbili zinakujia kwa hisani ya nani?Jibu lako kaa nalo.

Wakuu msichoke naendelea na utangulizi.

ADUI WA TAIFA HILI NI YUPI HASWA KWA SASA??

Kabla sijamtaja ningependa kusema kuwa inawezekana miaka yote tuliyofanya uchaguzi hatukuwahi kuwa na ajenda kama taifa bali tuliendelea kuimbishwa kama kasuku kuhusu maadui hawa watatu.Sasa
ni wakati muafaka tukaingia kwenye uchaguzi huu tukiwa na ajenda ya pamoja.

Adui pekee aliyebaki Tanzania ni UFISADI...yaani huyu ndiye kubwa la maadui .Hata hayati JKN hakustuka au aliunderestimate uwezo wa Adui hili na ndio maana leo hii limekuwa kubwa la maadui.

Tanzania ya leo inakwamishwa na Ufisadi ama mfumo na mtandao wa kifisadi unaokuwa kwa kasi.....

Vijana wanakosa mikopo ya kusoma vyuo vikuu mpaka wanasingizia wazazi wao ni vilema au wafu ili tu wapate mkopo ilihali kuna mafisadi wamehifadhi vijisenti uswisi.

Madawa yanakosekana katika zile zahanati za kila kijiji ikiwemo ile zahanati kuu kisa ni madeni au labda watu wanataka kujipigia 10%

Kwa ufupi ufisadi ni janga janga janga la kitaifa kwani hata umeanza kujidhihirisha makanisani.

Tunahitaji kuwawajibisha,kuwachukia na ikiwezekana kuwapoteza.

Kazi hii hahitaji mtu legelege bali mwenye dhamira na tabia isiyokoma ya kuwa na misimamo isiyoyumba....Hii ndio SABABU MOJA YA KUMPA LISSU KIJITI KWA TIKETI YA UKAWA.

Tunapomkabidhi Mama Tanzania tumwambie kazi yako ni moja tu ya kutuondolea ufisadi na mafisadi.

Kama ni viongozi tunao tunachohitaji ni kuwaondoa viongozi wenye nasaba za kifisadi.

Kama ni madaktari au waalimu au majaji wapo na tutaendelea kuwapata lakini tunahitaji kusafisha watumishi wote wenye genes za kifisadi.

Hatuna uhaba wa maafisa ugavi au wahasibu wanaoshiriki ufisadi tunahitaji kuzalisha wagavi au wahasibu waadilifu n.k n.k

SIFA KUMI ZA TUNDU LISSU KWA MUKTADHA WA HOJA HII

1-Tundu Lissu ni mkweli kwa kimombo yuko Honest.mara nyingi hujiweka wazi katika misimamo yake na hivyo kuwafanya wake kumuelewa na wao kuamua au kuchukua upande.Kijiko hukiita kijiko na sio beleshi dogo!

2-Maono/Malengo yaliyonyooka ama kwa kimombo niseme anaweza kufocus.
Kama uliwahi kumsikiliza bungeni basi utajua hajaikosa hii tabia kwani hata panapotokea distractions kama vile kutukanwa basi yeye hubaki katika mstari na kuendelea kukifafanua au kukifikia kile anachotaka.

3-Heshima kwa utu.Toka mwanzo wa siasa/harakati Tundu lissu amejikuta akipambania utu wa mwanadamu,rejea harakati za migodini.

4-Uwezo wa kujenga hoja na kushawishi.
Hili ni jambo muhimu kwani ukienda Zanzibar Tundu Lissu ameweza kuwavutia wazanzibar mpaka kupachikwa jina la Messi wa Ukawa.Naweza kusema hakuna kiongozi kutoka bara tena mkiristo anayeweza kuwa na ushawishi kwa upande wa zanzibar isipokuwa TL.iwe ndani au nje ya UKAWA.

Na hii ndio turufu muhimu kwa UKAWA kwa wakati huu.

5-Ujasiri
Tundu lissu hajawahi kuogopa especially kuwaogopa mafisadi.

6-Ujuvi au labda kwa lugha ya malkia niite Arrogance.Arrogance ni tabia isiyopendwa na wengi lakini Tabia hii ndio inayohitajika pindi unapopewa kazi ya kipambana na mafisadi papa na watumishi wajuaji.

pia ni sifa hii inayohitajika pale utakapokutana na mataifa makubwa yanayotaka kunyakua rasilimali za nchi hii.

7-Ni kijana na bado ni mkakamavu.

8-Ni mwanasheria nguli anayejua kucheza na sheria na hiki ndio kiama cha mafisadi kwani watafilisika kwa kukodi mawakili wa kupambana na Rais mwenye dhamira ya kuwanyoosha.

9-Ameishi na kukulia katika umasikini.Amekumbana na kuchukia dhahma za kuchangishwa michango ya kipuuzi huku kodi zikiliwa na mafisadi.

10-Anajifunza na kucope na mazingira kwa haraka.Uwepo wake ndani ya bunge baada ya Dr Slaa kuondoka umekuwa ni chachu ya mabadiliko nchini.


Nimalize kwa kusema kuwa Tundu Antiphas Mughwai Lissu ni aina ya kiongozi anayehitajika kwa sasa.


Tuungane kutokomeza ufisadi!!!

japo sina mahaba sana na hicho chama ila huyu mjamaa tundu lissu hakika namkubali mno na ni mwanasiasa wa kizazi hiki ambaye yupo very competent na kubwa zaidi ana kitu cha ziada cha kuwa na akili sana ambazo pia anajua kuzitumia ipasavyo ila ktk suala la yeye kuwa rais hapa nadhani ndiyo nitapishana na wewe. kwa features zake za kibinadamu na kihaiba hawezi na hafai kuwa rais ila nikisikia tundu lissu ni waziri mkuu au waziri wa sheria na katiba au mshauri mkuu wa rais kwa masuala ya sheria nitamuunga mkono kwa asilimia zote 100%. hongereni chadema kwa kuwa na mtu kama tundu lissu na ninamkubali kwa kiasi kikubwa tu na namwomba asichoke kusema ukweli kwa watawala.
 
CHADEMA inahitaji mtu nje ya wabunge waliopo ndio agombee urais. Ushindi wa kiti cha Urais ni probability bila kujali uwezo au uzalendo wa mtu. Kumpoteza Lissu kwenye panel ya wabunge ni pengo kubwa kwa chama. Tumeona hilo Kwa kumpoteza Dr Slaa. Tusirudie makosa yale tena. Uhakika wa ushindi kwa Upinzani kwenye kiti cha urais ni 2020 na hii itategemea sana ongezeko la idadi ya wabunge 2015. Nafasi kubwa kwa sasa kwa upinzani ni kuongeza idadi ya wabunge. Maoni yangu Lissu akatetee jimbo lake. Ikitokea upinzani ukashinda kiti cha urais basi atakuwa na nafasi kubwa kuhudumia watanzania kwa nafasi ya uwaziri au AG
 
Dr.Slaa alisema Tundu Lissu ndani yake kuna Dr.Slaa kumi (10).
Maneno hayo aliyatamka Dr. Slaa mwenyewe wakati anaikosa nafasi ya kuwa mbunge mwaka 2010 .
 
namkubali sana tundu lisu .Anaweza tupeleka tunapotaka. yupo serious kweli na watanzania. Naomba ukawa wamupe nafas jamaa .
 
Kweli mkuu, anafaa sana kua AG

Kwenye nafasi ya AG Lissu anafit ila kwa mawazo yangu angefaa sana kwenye ile wizara ya nishati na migodi, kwani kwa umahili wake wa sheria na nasaba za kizalendo alizonazo angetusaidia sana kwenye mikataba mibovu.
 
japo sina mahaba sana na hicho chama ila huyu mjamaa tundu lissu hakika namkubali mno na ni mwanasiasa wa kizazi hiki ambaye yupo very competent na kubwa zaidi ana kitu cha ziada cha kuwa na akili sana ambazo pia anajua kuzitumia ipasavyo ila ktk suala la yeye kuwa rais hapa nadhani ndiyo nitapishana na wewe. kwa features zake za kibinadamu na kihaiba hawezi na hafai kuwa rais ila nikisikia tundu lissu ni waziri mkuu au waziri wa sheria na katiba au mshauri mkuu wa rais kwa masuala ya sheria nitamuunga mkono kwa asilimia zote 100%. hongereni chadema kwa kuwa na mtu kama tundu lissu na ninamkubali kwa kiasi kikubwa tu na namwomba asichoke kusema ukweli kwa watawala.
...huna mahaba na chama anachotoka Lissu...na kwa maana hiyo huwezi kupenda yeye awe rais...maana akigombea urais TZ lazima atashinda..na hili ndilo linaloogopwa sana na watu wa ccm....maana Lissu anakubalika na kila mtu kwenye taifa hili.....Wengi wanatamani Lissu awe kiongozi wao...maana amedhihirisha hili si kwa maneno bali kwa vitendo...Woga wako kwa Lissu kugombea urais TZ hauna tofauti na uoga wa rais JK pale aliposema bora Slaa awe rais kuliko Lissu awe mbunge....
 
tundu ni zaid ya mwanasiasa ni zaid ya mwanaharakat kwa tanzania yetu ya leo,ambayo imejaa vioja na hata jk analitambua hilo, ni afadhar wana ccm {wabunge}30 wapotee ktk raman ya siasa kulko TUNDU maana anahtajka kwa nyakat za sasa.
 
Tundu lissu huyu jamaa namkubali sana tena sana. Hana mpinzani
 
Tundu lisu hana masters ana degree tu, pia hawezi wala hana sifa ya kuongoza nchi, amejaa matusi tu kichwani hafai kwa matumizi ya umma

We una matumizi yoyote ya umma? Au ni sehemu ya majizi yanayokwapua kutoka kwa umma? Lissu ni rais wa 5 wa Tz, jiandae kisaikolojia
 
Tundu Lissu ni mropokaji na mpiga makelele anayetumia uwezo wake wa kuropoka na kuongea kwa sauti ya ukali kuweza kuwashawishi na kuwaaminisha watu kuwa anachokisema ni kweli. Hawezi kuwa mwanasheria bora huku hata hajui kama kinga ya Mbunge kwa kile anachokisema bungeni ni kwenye suala la madai tu na si kosa la jinai.

We una uwezo upi? mropokaji ukimlinganisha na na nani? au hafai kuwa badala ya nani? mi naona anafaa ndani ya ukawa na ccm
 
Well said, tundu lisu ni mtendaji, hupaswi kugombea uraisi. Uraisi bado slaa anafaa kwasasa

Tundu lissu akitumika kama mtendaji katika serikali kutakuwa na ufanisi

Km una nia nzuri na mabadiliko ni hv: wote wanafaa lakini wote hawauziki sawa, so achana na huu wimbo
 
...huna mahaba na chama anachotoka Lissu...na kwa maana hiyo huwezi kupenda yeye awe rais...maana akigombea urais TZ lazima atashinda..na hili ndilo linaloogopwa sana na watu wa ccm....maana Lissu anakubalika na kila mtu kwenye taifa hili.....Wengi wanatamani Lissu awe kiongozi wao...maana amedhihirisha hili si kwa maneno bali kwa vitendo...Woga wako kwa Lissu kugombea urais TZ hauna tofauti na uoga wa rais JK pale aliposema bora Slaa awe rais kuliko Lissu awe mbunge....

no comment.
 
Nafikiri Tundu Lissu angeendelea kuwa mbunge, uwezekano wa UKAWA kushinda sio mkubwa kiasi hicho, tuwe wakweli ila idadi ya wabunge lazima wataongeza, tena kubwa tu. Wajikite kwenye kuongeza idadi ya wabunge, upande wa urais asimamishwe yeyote ila si Tundu Lissu. Lissu inapendeza asimamishwe kama mgombea urais wakati uwezekano wa kuwa rais toka upinzani ni mkubwa. Endapo Lissu atagombea urais mwaka huu, na wakashindwa, ambayo nafikiri ndivyo itakavyokuwa, tutamkosa mtu kama huyu katika bunge ambalo nina uhakika litawaka moto zaidi. Tundu Lizzu agombee 2020 au 2025, atakuwa ameiva kabisaaa!! Kama ukawa watashinda mwaka huu, basi Tundu Lissu ateuliwe kama mwanasheria mkuu au waziri mkuu.
Tundu Lissu, tafadhari usigombee urais mwaka huu. Tunakuhitaji bungeni bado.
 
Nafikiri Tundu Lissu angeendelea kuwa mbunge, uwezekano wa UKAWA kushinda sio mkubwa kiasi hicho, tuwe wakweli ila idadi ya wabunge lazima wataongeza, tena kubwa tu. Wajikite kwenye kuongeza idadi ya wabunge, upande wa urais asimamishwe yeyote ila si Tundu Lissu. Lissu inapendeza asimamishwe kama mgombea urais wakati uwezekano wa kuwa rais toka upinzani ni mkubwa. Endapo Lissu atagombea urais mwaka huu, na wakashindwa, ambayo nafikiri ndivyo itakavyokuwa, tutamkosa mtu kama huyu katika bunge ambalo nina uhakika litawaka moto zaidi. Tundu Lizzu agombee 2020 au 2025, atakuwa ameiva kabisaaa!! Kama ukawa watashinda mwaka huu, basi Tundu Lissu ateuliwe kama mwanasheria mkuu au waziri mkuu.
Tundu Lissu, tafadhari usigombee urais mwaka huu. Tunakuhitaji bungeni bado.

Dead wrong!hatuna muda mwingine wa kupoteza.acha woga
 
CHADEMA chukua tahadhari kwa mambo yanayoweza kuwagawa kwa kipindi hiki muhimu.
 
Ni heshima ya pekee ambayo anaendelea kujijengea mtumishi huyu wa wana singida
 
Back
Top Bottom