Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Mleta mada umenifikirisha

Lissu ni kiongozii mzuri ndio maana hata katika serikali za mitaa ameshinda kwa asilimia 99.9% kutoka kwenye viti alivyokuwa navyo mwanzoni.

Kuna wale wenye siasa nyepesi eti kuwa Lissu ni kichaaa...my foot...wananchi wasingempa kura zote hizo kwenye serikali za mitaa.

Napafahamu singida.Wakazi wake bado wana elimu duni...hivyo ni vigumu kwa wao kukubali mabadiliko...kwa lissu kupata mafanikio hayo ni dhahiri wananchi wamemuelewa.

Kama taifa tusifanye kosa.

Lissu amekuwa kiongozi Bungeni...akisema kitu ndicho hicho

Lissu amekuwa nguzo muhimu kulielekeza taifa katika katiba inayofaa

Lissu hana hata chembe ya Ufisadi

Lissu hafichi kitu...he is honest and transparent
 
Naunga mkono lisu agombee urais kwa tkt ya ukawa kwanza mdahalo utakuwa poa nchi itatakasika .mbivu na mbichi zitatoka jana. Naamini hakuna mgombea fisadi atakayepanda jukwaani. Rushwa .kofia .t shirt. Zikiwepo ni kwa nidhamu. Kama ni muungano lisu anashaurika kwa lenye mashiko.
 
CHADEMA msije mkafanya kosa la kumsimamisha mgombea mwingine zaidi ya Lissu kwasababu,Kwa mfano Dr Slaa anaweza kiongozi mzuri sana wa nchi hii lakini tatizo linakuja je anachagulika?Tayari inajulikana kabisa Dr Slaa anaweza kuzikosa kura za Watanzania wa imani nyingine.Ni dhahiri hakuna atakaueweza kushinda urais kwa kutegemea kura za watu wa imani moja tu.Hapo ndipo Tundu Lissu anapotokea kuwa mgombea salama kidogo kwani misimamo yake ya kisiasa imetokea kuwakuna Watanzania wa imani nyingine pia hivyo ana uhakika wa kupata kura kutoka upande huo pia.Lissu ni kijana na ni msomi anaweza kuwavutia vijana wengi kwenda kupiga kura kwa wingi.Lissu ana mwonekano hii inaweza kumsaidia kupata kura za wanawake pia.Fikiria CCM wakimsimamisha Pinda kama mgombea wao wa urais na UKAWA wakamsimamisha Lissu nini kitatokea.
...you got it bra....pamoja na quality zote za Lissu..haya uliyoweka hapa ni nyongeza pia....thanks..
 
Nimeufuatilia uzi huu kwa makini sana na nimeona yafuatayo: Wengi wanaomuunga mkono Tundu Lissu wamejenga hoja za kueleweka, Wale waliompinga hawajatoa hoja yoyote nyingine zaidi ya kusema ana jazba lakini pia wameshindwa kueleza kuwa hata kama ana jazba lakini kama ni mzalendo tatizo liko wapi! Kwa maana nyingine jazba za TL zinaweza kuwa na msaada maana watakao kabiliana nazo ni wale mafisadi.
Sasa naanza kuona idadi ya watz waliochoka ubabaishaji imeongezeka sana na ni wakati sasa wa kumsimamisha Tundu Lissu ktk nafasi ya Urais. najua kuna risk ya kumkosa bungeni lakini "high risk high life" tuchukue hiyo risk maana nchi imefikia mahali pabaya.
 
mm ni CUF ukweli nilitamani sana mtu kama Lissu angekuwa upande wetu ata ivyo naunga mkono sana juhudi zake kwakweli namkubali sana anajuwa siasa na kupambana kiume, ukweli kabisa ni kwamba nimeanza kuijuwa Chadema na kuipenda kwa kumfuatilia huyu Tundu Lissu tu sana sana anapokuwa bungeni na kwenye mjadala hivi kwenye TV
 
Tundu lissu uyuu jamaa anajua siasa na pia anamsimamo sana. Tundu lisu ni sawa na wabunge 20 wa CCM. Ukawa tuendelee kutafuta majembe zaidi kama LISU.
 
..

....3-Heshima kwa utu.Toka mwanzo wa siasa/harakati Tundu lissu amejikuta akipambania utu wa mwanadamu,rejea harakati za migodini.


...Salute !!!
 
lisu ni kiongozi mzuri sana but anafaa awe MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI uraisi hatouweza yupo strict sana na raisi anatakiwa awe flexible sometime.

katika maamuzi namfananisha na magufuli kabisa but even magufuli awezi kuwa raisi kutokana na kuwa na kaliba zinazofanana.

doctor slaaa
lipumba.
mbowe.
lowasa
kidogo wanaweza kuvaa hivyo viatu ya uraisi wa TZ

Nakuunga mkono kabisa mkuu, TL anatufaa sana pale bungeni kama AG, hata mikataba ya kifisadi itaisha.
 
Mleta mada nakubaliana na wewe kuwa kwa sasa adui mkubwa ni Ufisadi.
 
Tundu Lissu ana advantage nyingi sana,ni handsome pia,akina mama wanapenda ma_handsome boy.Hicho ndicho kilichomsaidia JK,Ila Lissu ana akili

Mkuu nimeipenda hii, Juzi wakati tunaangalia bunge alikua anaongea waziri mkuu Pinda, mwanamke mmoja akasema kama ccm inataka ipotee kwenye uchaguzi ujao basi wamweke Pinda, akaendelea kusema hata JK alipata kura nyingi kutoka kwa wanawake sababu ni handsome.
Wanajamvi hii habari ya kuangalia sura bado inaitafuna nchi yetu.
 
Back
Top Bottom