Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Muungano huanzia mioyoni mwa wanaoungana. Huwezi kuunganisha watu bila kuwapa faida zao za kuungana. Unapaswa kuwaambia hao watu watafaidikaje na muungano na uwasikilize wao wakupe aina ya muungano wanaoutaka na sio ule watawala wanaoutaka wao kwa maslahi yao. Muungano wowote ni lazima pande zote mbili zinufaike na kuungana kwao. Huwez sema muungano sio suala la kupata haki sawa sasa huo utakuwa muungano wa viongoz wachache kwa maslahi yao na sio wa watawaliwa yani wana nchi. Unahitaji uelewa kwenye swala la muungano wew. Hoja za kuwa taifa kubwa bila wananchi wake kuridhia ni ulaghai wa watawala. Upo hapo?

Wewe kama Binaadamu hutakiwi kujiconfine kwenye kajigraphia Fulani na kukafanya kama mungu wako, open up your mind. unaweza kuishi sehemu yoyote ile unayotaka wewe, lakini ukumbuke hauwezi kuwa confortable kuishi kwenye ka nchi dhaifu

Swala la Muungano sio swala la haki ya binaadamu,Leo tunaenda kupiga kura juu ya katiba na swala la muungano likiwemo, wale wenye umri chini ya miaka 18 hawapigi kura, una uhakika gani matakwa yao tutayazingatia.

wakikua wakasema tubadilishe tutafanyaje?

Tunataka mtu atakaye tuongoza kwenye hili,Kama alivyofanya Nyerere sio mtu mwenye hoja nyiiiiingi kwenye jambo moja kama Lissu.
 
Kitu kingine Lissu ni Socialist, sasa mtu wa namna hii anaweza kuingiza kila mtu kwenye matatizo ya kiuchumi.
 
100% nampa huyo jamaa, ni kweli mkorofi ana jazba lakini hii nchi ilivyooza kwa sasa atatufaa sana hata 5 yrs tu ndio apewe huyo asiye na jazba
 
Na kingine ni kwamba, kama ulivyosema, Lissu amekulia maisha ya kifukara, hivyo sidhani kama anajua ubora wa maisha tunayoyataka, kwake wote tukiwa mafukara inaweza ikawa ndio uongozi bora.
 
Tundu Lissu anafaa sana kuwa AG au waziri wa sheria, atatufaa sana akiwa chini ya Rais Mhe. Dr. John Magufuli. hapo nchi itakaa sawa, ni mchakamchaka. wezi wote jela na fedha zote kurudishwa. Mhe, Mwigulu Apandishwe kuwa waziri kamili wa fedha, Prof, Lipumba awe Gavana BOT, na Dr. Slaa awe PM,
 
Tundu Lissu ni mropokaji na mpiga makelele anayetumia uwezo wake wa kuropoka na kuongea kwa sauti ya ukali kuweza kuwashawishi na kuwaaminisha watu kuwa anachokisema ni kweli. Hawezi kuwa mwanasheria bora huku hata hajui kama kinga ya Mbunge kwa kile anachokisema bungeni ni kwenye suala la madai tu na si kosa la jinai.

Acha woga...!
 
Inayohitajika ni jazba iliyochanganyika na busara. Jazba ya Tundu Lissu, waulize wananchi wa kijiji cha Mahambe, Wilaya ya Ikungi. Jazba yake inatokana na dozi ya dawa alizopewa pale hospitali moja ya Dodoma. lakini kama hatuamini, agombee urais mwaka huu, tutampigia kura lkn tuwe tayari kwa matokeo ya urais wake.

Ndugu hayo mengine ni SIASA za watu wa CCM kwa kumuogopa...mbona hatujackia kuwa huko IKUNGI km kapigana na Wananchi....umewahi kujiuliza hawa watu wanaotutawala leo mbona ni wapole wamelisaidia nini Taifa hili....!
 
Wanaomkataa Lissu ni wale wanaokumbuka harakati zake ktk masuala ya migodi ya madini.Namkubali sana Dr Slaa ila ukaribu wake na Mbowe mtu ambaye amekuwa akiwatetea mafisadi,Mfano namna alivyomwokoa Pinda kwenye kashfa ya ESCROW imenipunguzia imani kwake.Tunamtaka Lissu kama mgombea wa urais kupitia UKAWA ili awanyoonyeshe mafisadi
 
tundu lisu ana akili lakin ana jazba sana hafai

Hivi kwa ujinga unaoongelewaga na baadhi ya wabunge mle mjengoni unafikiri kuna mtu mwenye akili atakosa kupandwa jazba..? Ukimfuatilia vizuri utajua pamoja na kukerwa huwa anabaki kwenye mstari; kama ni mfuatiliaji wa mambo utagundua,hakuna hata siku moja anaongea statements za kumfunga. Huwa anatumia utaalamu wake wa kubishana na viazi wengine kwenye baadhi ya kesi..

Kuna watu waliwahi kutamani kuvunja TV zao kwa ujinga unaotetewa na baadhi ya wabunge kwa kusimamia itikadi za chama badala ya facts au uzalendo..

Angekuwa hajui kutumia akili but only jazba, sidhani kama bado angekuwa wakili; angeshatupwa nje kwenye soko la sheria siku nyingi as mahakamani kuna kero za mjengoni cha mtoto...

Tukatae tukubali, kwa hii nchi kunyooka inataka mtu mwenye mkali sana ambaye diplomasia kaiacha nyumbani kwenda ikulu.. Ukileta wa kupaka paka mafuta watu na kwa hali tuliyofikia ya rushwa nje nje, then tegemea nchi hii kuendelea kudorora...
 
Vyumba vya madarasa sio issue mkuu!Kwa historia baba yake na Lissu aliwahi kuitoa nyimba yake iwe shule ya msingi.

Unachangisha wananchi maskini kujenga maabara wakati kodi yao halali inaliwa na singasinga hui ndio upuuzi asioutaka Lissu.

akichukua nchi hii michango ya kipuuzi ndio mwisho wake.

Mkuu meningitis kushinda sio kazi kwa Lisu kazi ni kutangazwa kashinda ndio haitatokea mbele ya masisi em.na hakuna kitakachotokea tena nasema ukawa hawana haja ya kupiga kampeni za nguvu sana naamini Watanzania watawachagua ila ila kutangazwa washindi ndicho hakitatokea chakufanya mapema mikakati ya kulinda kura iandaliwe na mbinu zingine.
 
Mnyika ni namba nyingine, darasa la Saba aliongoza mkoa na form four akapata point Saba. Ndio maana akili ya Mnyika inachaji Sana...

Angalia watu waliofeli darasa la Saba na kurudia mara tatu kama Sospeter Muhongo, au waliorudia mara moja moja kama HKigwangali aka Saidi Bagaile au Lameki Madelu aka Mwigulu Nchemba walivyo watu wa kukurupuka na kutotumia akili. Sio kwamba hawapendi kutumia akili, ila hawana hiyo akili. Nadhani umeelewa kwa nini nataka kujua matokeo ya awali ya TL sasa.
Makosa.
Uwezo wa darasani siyo ishara ya kiongozi bora.
Mafisadi wengi wana some of the smartest brains in the land.
 
Wanaomkataa Lissu ni wale wanaokumbuka harakati zake ktk masuala ya migodi ya madini.Namkubali sana Dr Slaa ila ukaribu wake na Mbowe mtu ambaye amekuwa akiwatetea mafisadi,Mfano namna alivyomwokoa Pinda kwenye kashfa ya ESCROW imenipunguzia imani kwake.Tunamtaka Lissu kama mgombea wa urais kupitia UKAWA ili awanyoonyeshe mafisadi

Tundu lissu ndiyo pekee wa kututoa hapa, ikishindikana basi Dr. slaa
 
meningitis,

..mgombea wa kwanza ni Slaa.

..ikishindikana huyo tunamtaka Tundu Lissu.

cc Pasco

Mkuu JokaKuu thread hii haimaanishi slaa ni mbaya.Hapa najaribu kuionesha jamii kwamba kuna alternative dhidi ya ccm.
Hata Dr Slaa atakubaliana na mimi katika hili.
Hii ni thread maalum kwa UKAWA kujipanga na kuweza kuchukua dola.
 
Last edited by a moderator:
..mleta uzi umefanya kazi nzuri kumchambua mh.Lissu...ili watanzania wengi wazidi kumjua...maana hakika watu kama hawa wanahitajika kwa ukombozi wa mkwamo unaoikabili TZ ya leo....Taifa hili linahitaji sana rais mithili ya Lissu ili kuwakoma nyani kilagi...maana hakika taifa hili linaangamizwa na mafisi na manyang'au walafi...

...Nitaunga mkono uteuzi wa mtu huyu kugombea urais kwa nguvu zangu zote...na namwombea uzima kwa mola...ili siku moja aliongoze taifa hili...Siwaoni watu/wanasiasa wengi kama Lissu katika taifa hili...

nami nitampigia mpaka kampeni!
 
Umuhimu wa kumchambua TL katika kipindi hiki ni kutokana na wimbi la wasaka tonge waliolipwa kuwapigia debe wagombea wale wale wenye sera zile zile na haiba zile zile za tabaka lile lile lililotufikisha hapa.

Rushwa na ufisadi ndio imekuwa tiketi wya kutuchagulia viongozi.

wananchi,wanachama wa vyama vya kisiasa,waandishi na viongozi wa kidini au jadi wanahongwa kuwapigia debe viongozi wabovu na matokeo yake Taifa linaangamia!

Wazalendo wa kweli wa Taifa hili tusimame na kulitetea kwa kuwa madhara ya viongozi wabovu yatatukumba.

say yes to TL and say ney to mafisadi.

Kwako nderingosha
 
Last edited by a moderator:
meningitis,

..lakini tunatofautiana na pale unaposema Tundu ni arrogant.

..mimi nadhani Tundu anajiamini, he is always well prepared, passionate, and confident in his presentations.

..TUNDU LISSU ANATOSHA.
 
Last edited by a moderator:
Kama President material ndio hao akina Kikwete ni bora tumpe Tundu Lissu. Nina uhakika wanaCCM wengi watampa kura akiwemo Anna Makinda

Ha ha ha ha bila kumsahau kipenzi cha Tundu Lissu, Mhe. Job ndugai (Huwa napenda wanapokuwa DK 45 ITV)
 
Back
Top Bottom