Elections 2015 Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)

Sasa wewe ndo utanifanya niseme!
CHADEMA HAINA RAIS ZAIDI YA SLAA, MAANA HATA SISI MAGAMBA TUNA IMANI NAE!
WATU KAMA LISSU NI SAWA NA VILE VIASKARI VYA 'UNDER 18'! NI VIZURI MNO VIKIPEWA AK 47 MAANA VINAUA BILA KUULIZA NA KUJUA KWANINI VINAUA, SHIDA INAKUJA VIKIPEWA KUONGOZA MAPAMBANO!
 
Kwa nini mkuu?
Umeorodhesha sifa za Lissu vizuri sana, lakini hiyo namba 7 imechafua. Hiyo ndiyo ilitumiwa kama turufu ya MM na kina Tuntemeke kwenye vikao vya mikakati yao ya mapinduzi ndani ya chama. Sioni kama ujana ni sifa muhimu kwa rais mtarajiwa.
 
Kwa kuwa Slaa alikubali ombi la baba askofu?

Nisome mwanzo kabisa utaelewa msingi wa hoja yangu.Nimependa huo mfano wako kwani kwa mustakabali wa nchi hii kwa sasa tunahitaji hiki kiaskari kidogo kinachoua bila kujiuliza kwa sababu Kamanda aliyetegemewa kutuongoza ameshakufa,kinachotakiwa ni kujinasua na kujipanga upya.

Tunahitaji kurudi kwenye mstari halafu tutarejea kwa hawa watu wa kiprotokali.

Hatutoki hapa salama bila ya mtu kama Lissu.

Dr Slaa yupo vizuri ndio maana tunaelezwa alishinda 2010 lakini akachakachuliwa.Mimi ningependa kumuona akimsimamia Lissu kuingia Magogoni na busara na influance yake itaendelea kutukuka kama alivyokuwa JKN.
 
View attachment 216678
angepewa nafasi ya kuwa mwanasheria mkuu wa serikali hawa wezi wangerudisha pesa zetu za escrow zote.
Akiwa rais anakuwa na uwezo zaidi wa kuzirudisha kama ana utashi kwani hatoingiliwa na mtu yeyote. Mwanasheria mkuu anaweza kuwa na nia rais akasema hapana.
 
Akiwa rais anakuwa na uwezo zaidi wa kuzirudisha kama ana utashi kwani hatoingiliwa na mtu yeyote. Mwanasheria mkuu anaweza kuwa na nia rais akasema hapana.
kwenye uraisi bado ana jazba sana .
 
Umeorodhesha sifa za Lissu vizuri sana, lakini hiyo namba 7 imechafua. Hiyo ndiyo ilitumiwa kama turufu ya MM na kina Tuntemeke kwenye vikao vya mikakati yao ya mapinduzi ndani ya chama. Sioni kama ujana ni sifa muhimu kwa rais mtarajiwa.

Pole kwa kukwazika!
Ni ukweli usiopingika kwamba dunia ya sasa inapita kwenye kipindi cha Umri fulani kuupisha umri mwingine.Ujana unataka kupishwa hivyo ni vyema uzee ukatambua hili....sio Tanzania tu bali duniani kote

Ukiangalia wagombea na wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utaelewa ninachokisema.

Strategically Ujana wa Lissu ni added advantage.

Chukulia hivyo mkuu !!
 
Sema unamuogopa Dr.Slaa kiaina!!
 
Naunga mkono hoja, Tundu lissu ni chaguo sahihi kwa sasa, anakubalik na makundi yote nchini, annakubalika vyama vyote. Ni kijana hivyo ni nguvu ya mabadiliko.

#GOODMORNING
 
Tundu Lissu ana advantage nyingi sana,ni handsome pia,akina mama wanapenda ma_handsome boy.Hicho ndicho kilichomsaidia JK,Ila Lissu ana akili
 
Kimsingi Tundu Lisu niMZALENDO ambaye ningependa awe moja ya viongozi wakuu wan chi hii. Hata hivyo,yafaa awe WAZIRI MKUU. Na Baraza kuwa hivi:
Rais, Dr SlaaWaziri Mkuu: Tundu Lisu,Mwanasheria Mkuu: Mnyika Waziri wa Mambo yaNdani: LemaWaziri wa Fedha na Uchumi:Prof. LipumbaJaji Mkuu: ……Waziri wa Katiba naSheria………….Nishati na Madini……………………Waziri wa Afya………………………….Waziri wa Ulinzi………………………….Waziri wa mambo ya njena Ushirikiano wa Kimataifa………………….Waziri wa TAMISEMI…………………………………………………….
 
Hamna mtu mwenye sifa nzuri kama Rais mteule Dr. Slaa. Mugabe ana miaka 90s na Dr ana nusu yake.
 
Pengine si wakati muafaka kumtaja raisi kupitia UKAWA, lakini nashindwa kupambana na na hoja yako kuhusu LISSU, Anaweza na huonekana ana dhamira ya dhati, na kwa kuwa taifa hili lina tatizo la makusudi la kisheria kama mikataba ya hovyo, kwa kiongozi kama Lissu amabaye ni mjuzi wa sheria itakuwa poa sana, umejitahidi kutuaminisha na ukweli ni kwamba kila kitu kipo ila vinaatumiwaje kumalizia tatizo la ujinga, maradhi na umaskini? jibu ni ufisadi ndio kikwazoo kikubwa.
Ukimpima Lissu na Jk, Lissu anaonekana ana dhamira na malengo, jazba huja mara tu anapotukanwa hasahasa anapoguswa binafsi na si hoja zake, pamoja na hilo hujichukulia mtu wa kawaida sana, tofauti na vingozi wanaopenda kujikwaza (wale wanaopenda kuitwa waheshimiwa), anajua wajibu wake na kufuata maelezo kwa kadri taaluma aliyonayo inavyomtaka awe, naamini akiwa raisi wa taifa hili atatimiza wajibu na yote ambayo watz tunategemea kutoka kwa kiongozi huyo mkubwa. Anafaa na anastahili.
 
Atawafunga ccm wote,ila ndo kwa sasa mtu anyefaa airudishe nchi katika mstari yupo opposite ya mzee wa msoga kabisa katika maamuzi.
 
Pengine si wakati muafaka kumtaja raisi kupitia UKAWA, lakini nashindwa kupambana na na hoja yako kuhusu LISSU, Anaweza na huonekana ana dhamira ya dhati, na kwa kuwa taifa hili lina tatizo la makusudi la kisheria kama mikataba ya hovyo, kwa kiongozi kama Lissu amabaye ni mjuzi wa sheria itakuwa poa sana, umejitahidi kutuaminisha na ukweli ni kwamba kila kitu kipo ila vinaatumiwaje kumalizia tatizo la ujinga, maradhi na umaskini? jibu ni ufisadi ndio kikwazoo kikubwa.
Ukimpima Lissu na Jk, Lissu anaonekana ana dhamira na malengo, jazba huja mara tu anapotukanwa hasahasa anapoguswa binafsi na si hoja zake, pamoja na hilo hujichukulia mtu wa kawaida sana, tofauti na vingozi wanaopenda kujikwaza (wale wanaopenda kuitwa waheshimiwa), anajua wajibu wake na kufuata maelezo kwa kadri taaluma aliyonayo inavyomtaka awe, naamini akiwa raisi wa taifa hili atatimiza wajibu na yote ambayo watz tunategemea kutoka kwa kiongozi huyo mkubwa. Anafaa na anastahili.
 
Tatizo lingine la lissu ni kwamba, anaweza kuharibu kabisa confidence ya mahakama kutimiza wajibu wake bila kuingiliwa. Lissu ni mtu ambaye haziamini kabisa mahakama zetu.

Akiwa rais anaweza kulazimisha Mahakama ziwe chini ya ofisi ya Rais, kitu kitakachotuingiza matatani na nchi wahisani.
 
Acha mambo ya ajabu mbona hao wanaotaka kugombea urais hujaitaji matokeo yao ya shule hizi ni chuki binafs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…