Wanabodi,
Kwanza sio kila kitu ni siasa, vitu vingine ni hoja za kikatiba, Sheria, taratibu na kanuni.
Ukileta hoja specific, hakuna ubaya kujifagilia ubobezi wako katika eneo husika.
Mimi Paskali Mayalla ni Mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea, ila pia nilisomea sheria, LL.B, UDSM, ile kutua tuu UDSM, siku ya kwanza kipindi cha Kwanza ni LW 101, unajua mwalimu wangu wa kwanza kabisa UDSM ni nani?... ni Dr. Tulia Akson!.
Prof. Issa Gulamhussein Shivji na Palamagamba Kabudi, walitufundisha LW. 200 ndio yenye Katiba, nilifumua A, utadhani mtihani nilikuwa natunga mimi!. Hivyo kwenye hoja hii ya Katiba ya Chadema, mimi naizungumza as an authority.
Katiba ni kakitabu kadogo tuu, ila kukaelewa ni shughuli. Kabla ya chama chochote cha siasa kusajiliwa ni lazima kiwasilishe katiba yake kwa Msajili wa vyama, ipitiwe na wataalamu wa katiba, wajiridhishe kuwa iko sawa na inaendana na katiba ya nchi.
Hivyo hata Chadema, iliposajiliwa kwa mara ya kwanza ile 1992, iliwasilisha katiba fulani amaizing iliyokuwa nzuri kabisa, yenye kipengele cha ukomo wa uongozi mwisho ni vipindi viwili vya miaka 5 na mwanachama wa Chadema alikuwa huru kuitafuta haki yake mahakamani.
Mwaka 2006, Chadema wakafanya marekebisho ya Katiba na kuyasilisha ofisi ya msajili wa vyama, na ikakubaliwa.
Nilipoipitia katiba hiyo ya Chadema ya 2006, nikakuta kile kipengele cha ukomo wa uongozi, hakipo!, kimenyofolewa kinyemela!. Nilipokiulizia kipengele hicho humu jf, Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Slaa alinishukikia vilivyo na kukanusha kuwa Chadema halikuwahi kuwa na kipengele hicho!.
Hii maana yake ni hata Katibu Mkuu Chadema, alikuwa haijui Katiba ya chama chake!. Kama Katibu Mkuu ambaye ndie custodian wa katiba ya Chadema, haijui katiba hiyo, what do expect kwa the rest of the people?.
Baada ya Dr. Slaa kunishukia, aliyeninusuru ni JJ. Mnyika kukiri kifungu hicho kilikuwepo na sasa hakipo sio kuwa kimenyofolewa!, no!, bali ni hakikujadiliwa kabisa hivyo kikayeyuka tuu into thin air!
Katiba hiyo ya 2006 pia ikapenyeza kifungu ambacho kinakwenda kinyume cha katiba ya JMT kumzuia mwanachama wa Chadema kwenda mahakamani, akienda tuu ndio amejifukuzisha Chadema!.
Tukija kwenye hoja za bandiko hili ambazo mimi nimeziita Chadema ni ubatili, ubatili ubatili mtupu mpaka basi!. CC ya CDM haina mamlaka kumjadili Mwenyekiti wa Bawacha, kwasababu sio mamlaka yake ya nidhamu, CC hiyo ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumjadili na kumfuta uanachama Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee?!.
Mamlaka sahihi ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha ni Baraza Kuu, na mamlaka yake yenye uwezo wa kumfuta uanachama Halima Mdee, ni Mkutano Mkuu pekee!. Sasa kwenye kikao cha juzi cha Baraza Kuu la Chadema, kuna mtu yoyote alisikia likijadil mashitaka yoyote ya Halima Mdee?. Ilichofanya Baraza Kuu ni kubariki maamuzi yale batili ya CC ya Chadema. Kitendo cha Baraza Kuu, kurudhia kuvuliwa uanachama wa Halima Mdee, Baraza Kuu lilipata wapi mamlaka hiyo?!.
Katiba ya Chadema ipo na imeweka taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu, kwanini hazifuatwi?. Sasa vitu vidogo tuu na straight kama hivi vinawashinda hawa jamaa, jee ingetokea watu kama hawa ndio wameshinda uchaguzi na kuikalia Ikulu yetu si ni ingekuwa ni majanga?. Kwa lugha nyingine, inawezekana Chadema ni Chama Majanga ila tuu watu walikuwa hawajui, hivyo mitikisiko kama hii ndio itawaonyesha wengine maeneo yenye matundu na jinsi nyumba yao inavyovuja.
Kama Chadema ndio chama kikuu cha upinzani kwa huku bara, jee tunaupinzani wowote wa kweli ambao ni serious, capable, credible, na reliable, wenye the ability and the capabilities wa kuiondoa CCM madarakani?!.
Paskali
Nimeisoma hukumu, 1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CC ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!.
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?.
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!.
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team!.
A Way Forward
1. Kwa vile Mahakama imekubali kuwa Chadema imewatimua hao 19 kihalali, japo uamuzi wa Baraza Kuu umepinduliwa, sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu, ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.
2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue rasmi Halima Mdee, kwasababu ndio mamlaka yake ya nidhamu, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, na zile fedha bado zipo, Chadema wakifanya kama walivyofanya, fedha za kugharimia kitagharimia vikao vyote viwili, zitatoka, na tena Chadema inaweza ku take advantage ya kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.
Paskali.