NI Ujinga uliopitiliza kuongeza Posho za safari mpaka Tsh 250,000 kwa siku huku mkitujazia matozo kila sehemu sie walalahoi.

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Rejea Gazeti la Mwananchi la May 27, 2022

Serikali imetoa kibali cha kurekebishwa kwa posho ya kujikimu safarini kutosha Sh120,000 hadi Sh250,000 kwa daraja la juu na Sh80,000 hadi Sh100,000 kwa daraja la chini.

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 27, 2022 na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishhi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro.

“Rais Samia amebadilisha pia kiwango cha malipo cha kazi maalumu kwa ngazi ya chini kutoka 15,000 hadi Sh30,000 kwa ngazi ya kazi kutoka Sh20,000 hadi Sh40,000 na ngazi ya juu kutoka Sh30,000 hadi Sh60,000”. amesema.

Dk Ndumbaro asema kuwa mabadiliko hayo yataanza rasmi Julai Mosi, 2021 na kwamba bajeti iliyopangwa ndiyo itakayotumika kutekeleza viwango hivyo.

Pia ametoa wito kwa wafanyakazi wa umma kufanya kazi kwa bidi zaidi bila kusubiri kusimamiwa, kujituma, kuwa wabunifu na wenye nidhamu na maarifa.

wakati wao wakijiwazia kujiongezea posho na malupulupu kwa siku hawakuacha kuangalia wanatoa wapi hizo posho, wakaja na tozo kwenye miamala ya simu, wakaona haitoshi wakaja na tozo kwenye Mabank, na kama haitoshi bado wanakuja kwenye Vingamuzi na tutarajie mwakani watakuja kwa sehemu nyingine.
 
Inauma sana, nadhani kwakuwa sisi ni wanyonge na hatuna ubavu wa kupambana nao,tuelekeze maombi Kwa mola wetu atuondolee hii ghasia kama alivyofanya Kwa Magufuli na Kwa Hawa wahuni wengine awachukue haraka sana kabla hali haijawa mbaya zaidi. Aamiyn
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…