Ni ujinga uriokithiri kurithi adui wa mtu kwa kusimuliwa habari zake

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Hakuna kitu cha kijinga na cha kishamba kama tabia ya kurithi adui au maadui wa mtu ,,, unakuta mtu anavuta taswira ya ubaya wa mtu au wa watu kwa kusimuliwa tu wakati hajawai hata kuwatia machoni hao watu au huyo mtu

Usiwe mwepesi wa kuamini maneno ya watu , jambo lolote lile lifanyie tafiti mwenyewe ujiridhishe kabla ya kutoa hukumu. Kumbuka wazushi ni wengi wanao chafua majina ya watu kwa chukizao binafsi
 
Halafu hii imeenea sana. Mtu anakuchukia bila sababu hakujui humjui
 
Kweli kabisa. Ila ndio hatuna jinsi.

Umenza kupata magego tu na kuuma uma matiti unachapwa kidizaini halafu unaambiwa una shea na babako. Hilo jicho lako kwanza kwa mama na hasira inayofuata kwa babako asee.
 
Vipi mkuu unavyosikia habari za shetani na mabaya yake kwenye mahubiri na vitabu vya dini ..nao ni ujinga au chuki zao binafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…