MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Katika pita pita zangu huku JF nimeshtushwa na kiasi kikubwa cha ukosefu au upungufu wa akili wa kundi kubwa la watu wanaoshabikia vita ya mashariki ya kati na kwingineko
Kwangu mimi, vita na matokeo yake au madhila yoyote yatokanayo na ukandamizaji wa aina yoyote siyo jambo la kushangilia au kufurahia.
Kwasababu yoyote ile, siyo jambo sahihi kushika silaha na kumuua mtu mwingine au kumsababishia maumivu na uharibifu au upotevu wa mali zake
Haijalishi nani yuko sahihi au la, wahanga wa vita na ukandamizaji siyo wale wanaokosa au kuanzisha hizo vita, ni watu wasio na hatia, akina mama na watoto
Risasi inapopigwa aimtafuti mbaya peke yake, hali kadhalika bomu linaporushwa halimtafuti mtu mbaya peke yake, risasi inapiga mwema na mbaya na bomu linaleta madhara kwa mwema na muovu
Kwanini tunachukua upande, tunasimama na huyu au yule, washirika wa vita hii ya mashariki ya kati, wote ni watu wasiowaza vizuri, pengine wako kimaslahi zaidi
Wewe ndugu yangu hapa JF, nini kimekusibu mpaka unashangilia madhila ya watu wengine?> JITAFAKARI NA JIRATIBU