Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
- Ambao wana nafasi ya kukusaidia ndiyo watakuangusha na kukurudisha nyuma kwenye mapambano yako.
- Wanasiasa wetu (hasa wale wenye tabia ambazo baba wa taifa aliziita za kimalaya malaya) ni adui zetu namba moja.
- Tutachelewa kupata mabadikiko kwa sababu ya ujuaji mwingi na kukosa utayari wa kujifunza na kujipanga kimkakati.
Vipi wewe umekubali jambo au mambo gani?
Maalum kwa Gen Z,
Usiache kujielimisha, taarifa ni moja ya silaha, jua haki yako, wajibu na mambo ya msingi unayotaka yabadilike.
Isome katiba (IPAKUE HAPA) kama hujui pa kuanzia nakuwekea vipengele vichache:
- Ukurasa wa 16 - 23: Fahamu zaidi kuhusu haki yako ya kuishi, haki ya usawa, haki ya uhuru wa mawazo n.k
- Ukurasa wa 27 -39: Kuhusu raisi (serikali na mamlaka zake)
- Ukurasa 57 - 62: Kuhusu tume ya uchaguzi
- Ukurasa wa 32 - 37: Fahamu kuhusu uhaini, unahusisha nini na makosa mengine dhidi ya serikali
- Ukurasa wa 40 - 43: Kuhusu mikusanyiko na ghasia
- Ukurasa wa 44 - 45: Kuhusu kutumia madaraka vibaya