Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Pia nahis kuna tatizo kwenye sheria zetu,sijawai kuona movie iliyotengenezwa na maproducers wakubwa kutumia mandhari ya kibongo (labda serengeti NP) vinginevyo wanaitumia Kenya zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Wabongo wana umimi, hiki changu tu. Sijawahi kmsikia m'bongo anayekubali nyumba yake nzuri (mansion) itumike kuigizia eti "watanichora" halafu waje kuniibia. Kumbe kwa wenzetu mtu anatoa nyumba yake nzuri au duka au kiwanja vitumike kuigizia lakini kwa malipo.
 
Ndo tunapofeli hapo wenzetu wanapewa vitu vyote Kwa uhalisia wake ndo maana wanatoboa
 
Naamini yote YANAWEZEKANA endapo taratibu zutafuatwa kwa kuomba kibali na mahitaji yako , ikiwemo vifaa na mafunzo , ukiweka wazi hizo lako LITAKUWAJE?

Tunapenda kukurupuka ss wenyewe na kutoa maigizo ya HOVYO kisha tunasema tatizo NCHI INAKATAZA KUTUMIA VIFAA HALISI.

Kumbuka HAYO yote yataambatana na MALIPO ya maana.
 
Sasa utashangaa unaweza kuwa stejini na umevaa nguo za jwtz na eti wakaja kukuvua au ukishuka wanakuwashia moto!!
Kumbe shida ni hao hawasomi.

Kuhusu kupata kibali ni rahisi tuu.
Elimu hii wasanii na wanatasnia wengi hawaifahamu na hata kama wanajua uenda haifanyi kazi hivyo iliandikwa kisheria kwenye utekelezaji wake na vyombo vinavyosimamia hiyo haki.
 
Umefanya jambo zuri na kubwa kuleta somo hili hapa, wengi wetu kipengele hiki cha sheria huwa hatukifahamu zaidi ya kujikuta tukishavunja sheria hizi kwa kuvaa mavazi haya kwa kutokujua tukakutana na majeshi yetu ni kipigo na kurukishwa kichura chura au kudhalilishwa hadharani kwa kuvuliwa nguo kana kwamba ndivyo sheria inavyoagiza.
 
Tatizo wanatumia hizo uniform kuteflect hali halisi ya jeshi letu...i.e waonevu, ubabe kwa wanyonge, respect kwa wenye pesa na Rushwa... hakuna anaetaka kutangazwa negatively. Anyway nakumbuka Penzi la misukosuko yule jamaa aliyeigiza Ins. J Plus angependezea sana na uzi...bahati mbaya ni moja ya movie zangu za mwisho kuangalia Bongo Movie sijapata tena interest na hawa watu especially baada ya soko kuwa flooded na series kali za nje ilihali humu ndani tukaendelea kutoa vitu kwa mazoea.
Ndyooo jimmy angependeza sana na gwanda yaan.
 
Nanukuu: Tanzania ni moja ya nchi yenye vijana wenye vipaji vya mapigano na masumbwi kuliko nchi yeyote inayocheza filamu za namna hiyo Afrika lakini kinachotuangusha ni uwekezaji mdogo katika filamu, hatuna teknolojia, vifaa duni, kukosa mafunzo, mazingira magumu ya kuigizia, bajeti ndogo,n.k Mwisho wa kunukuu.
Hii [emoji115] [emoji115] [emoji115] ndio changamoto kubwa na pia kuwekewa vikwazo visivyo vya lazima e.g. upatikanaji wa Sare (Uniform) stahiki katika maigizo au hata kuazimwa vifaa/vitendea kazi maalum ili kufanikisha scenario fulani katika igizo.
Wawekezaji e.g. wale wenye uwezo kifedha (Matajiri)hawaja wezeshwa kuona kwamba hiyo Tasnia nayo ni mojawapo ya fursa ya Uwekezaji. Naamini wakihamasishwa watathubutu kujipa roho ya Ujasiriamali katika Tasnia hii.
Serikali inao wajibu mkubwa wa kuwalinda na kuzilinda kazi zao kwa kutoa Hati miliki kuliko ilivyo sasa hivi vijana mpaka huku vijijini wananakili nyimbo,video na kufanya biashara katika vibanda kwa kutumuia Laptops na Flash bila hata kuwapa chochote waliohenyeka kutengeneza filamu hizo.
Asante kwa mawazo chanya kama haya we ni asset kwa jamii.
 
Ndo tunapofeli hapo wenzetu wanapewa vitu vyote Kwa uhalisia wake ndo maana wanatoboa
Ndiyo maana yake, mtu aliyewekeza kikubwa lazima ategemee kikubwa pia lakini yule wa kuunga-unga inawezekana hata asipate hicho anachotarajia ndicho kinachoikumba tasnia yetu.
 
Tafuta movie hizi.. Wenzetu Kenya wametuacha mbali.

1.Mission Rescue..

2.Mpakani
Nakumbuka hawa watu miaka michache iliyopita tulikuwa tumewaacha mbali mno, wakiwa na hakina baraza, mama kayai na yule fupii mwala ndo walikuwa waigizaji wao maarufu lakini leo hii eti nawao tunawaza kufuatilia muvi zao.
 
Mpaka kuvaa gwanda si mchezo! Haijalishi ziwe za jeshi au polisi

Wanaume tumezisotea na tumezilia kiapo!

Ila yule askari wa Zenji nahisi alikuwa wa mchongo au aliingia kwa connection. Avae gwanda na aliwe ndogo?! 😳🤔 Haiwezekani

Samahani nimetoka nje ya mada kidogo ila gwanda ni habari ingine!
 
Wabongo wana umimi, hiki changu tu. Sijawahi kmsikia m'bongo anayekubali nyumba yake nzuri (mansion) itumike kuigizia eti "watanichora" halafu waje kuniibia. Kumbe kwa wenzetu mtu anatoa nyumba yake nzuri au duka au kiwanja vitumike kuigizia lakini kwa malipo.
"..lakini kwa malipo" hiyo ndiyo sababu kuu ndugu, filamu zetu zinaendeshwa chini ya bajeti ndogo mno kiasi kwamba karibia robo tatu ya kile kilichotumika kwenye muvi iwe ni magari,nyumba mpaka maofisi ni ya kuazima na kuombaomba kwingi hivyo siyo rahisi unishawishi niame nyumba yangu kwa muda na familia nikua che uigiziemo wakati unajua fika kuwa mkono mtupu haurambwi.
 
Ni shabiki kindaki ndaki wa Jimmy.

Misuko suko
Double J
Foundation
Afu kuna ile kacheza na baby madaha. Jina nimesahau

Hizi alitisha sanaaaa, sichoki kutazama yaan.
We naonaga Comments zako kwenye mada za hovyohovyo tu na za ushoga. Kwenye vitu serious walaaaaa! Ila siku ukiletwa muswada wa kujadili maslahi yenu watu wa shetani (wa upinde) utachangia 😀

Dunia inaenda kasi sana! 😂🙌🏾
 
Pia nahis kuna tatizo kwenye sheria zetu,sijawai kuona movie iliyotengenezwa na maproducers wakubwa kutumia mandhari ya kibongo (labda serengeti NP) vinginevyo wanaitumia Kenya zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo maana ya mchango wa serikali katika kutoa kipaumbele katika jambo lake, tofauti na hapo tutaendelea kuwatupia lawama wasanii na maproduction managers ambao nao hawana la kufanya.
 
We naonaga Comments zako kwenye mada za hovyohovyo tu na za ushoga. Kwenye vitu serious walaaaaa! Ila siku ukiletwa muswada wa kujadili maslahi yenu watu wa shetani (wa upinde) utachangia [emoji3]

Dunia inaenda kasi sana! [emoji23][emoji1487]
Hivi badoo uko na mieee tyuuh?? Nkajua ushanisahau eti.

Huko kwenye vitu vya maana nimekuachia wee, uwakilishe genius. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jana nilipata wasaha wa kutizama luninga na bahati nzuri nikabahatika kutupia jicho katika muvi zetu almaarufu Bongo movies, kusema ukweli vijana wanajitahidi na kufanya kila wawezalo kuweza kuifikisha sanaa yao mbali licha ya changamoto kibao.

Baadhi ya changamoto kuu za kiwanda hiki ni;

1. Elimu - Taaluma nchini haijatambua bado sanaa na mwamko wa vyuo na michepuo yake haitoi nafasi katika sanaa.

2. Wasanii wachache mno wenye elimu ya sanaa na wengi huigiza au kuongoza filamu kwa uzoefu na hamasa tu.

3. Exposure - Kutokana na ukata uliopo wasanii wetu hawawezi kujifunza kwa njia ya tembea uone mengi.

Uwekezaji duni, kukosa haki na fursa sawa kama nchi zingine katika mauzo, udhibiti, usambazaji na matangazo, Kukosa kupewa kipaumbele, mazingira duni ya kuigizia,n.k.

Pamoja na yote haya watu hawa wanaendelea kila siku kuandika hadithi, kubuni na kuwekeza kidogo walichonacho kuhakikisha sisi na familia zetu tunaburudika na kuelimika.

Ila kilichonishangaza zaidi ni pale nilipobaini kuwa kuna kukwama kwingine kwa sanaa kunakochagizwa na kile ninachoweza kukiita ulimbukeni wa serikali katika kuielewa sanaa.

Hivi ni kipi kilipelekea maamuzi ya kusitisha/marufuku kwa wasanii wanapoigiza uhusika wa kipolisi au kijeshi wasivae sare za jeshi letu?

Ikumbukwe India na Korea ambao ni mifano ya mataifa machache yaliyopiga hatua katika soko la filamu na tunaongoza kutizama na kuzisifia muvi zao za kiintelijensia almaarufu detective, wanajitangaza kupitia filamu hizo duniani kote.

Nchi za wenzetu hawaoni taabu kuwaunga mkono wasanii wao linapokuja suala la kuitangaza nchi, msanii atapewa ushirikiano wa mafunzo, difenda, ambulance, zimamoto, kituo cha polisi, polisi halisi wachache akihitaji wakuigizia, sare mpaka na silaha zikihitajika katika sanaa yake ili mradi anachofanya ni kuigiza na pia kwa maslahi mapana ya kuelimisha jamii na uchumi wa taifa lake.

Sasa leo hii bongo muvi ukiitizama unabaki kushangaa tu, mtu anayeitwa polisi na vile alivyo-appear katika uhusika ni vituko.

Tukihitaji sanaa yetu ikue basi tuwaache wasanii wawe na fikra huru na mipaka ya shughuli zao isiingiliwe na hisia binafsi au mihemko ya kundi fulani katika jamii kuguswa na kazi ya fasihi.

Kama ilivyoshuhudiwa juzi kati wauguzi wa afya wakidai wasiigizwe, hii haina utofauti na polisi ambao nao baada ya kutizama igizo la filamu iliyochezwa na waigizaji wakongwe almaarufu J Plus na Seba walikataa sare zao zisitumike tena kisa kwa hisia zao binafsi walijihisi kudhalilishwa.

Badala yake tuipe sanaa nguvu yake ili iweze kui-shape jamii katika mwelekeo chanya pasipo na vizuizi mwisho wa siku sanaa kama kazi nyingine rasmi inahitajika kumnufaisha msanii na taifa pia.

Kwani kwa kutokufanya hivyo na tukiendelea na hiki kinachofanya sanaa yetu iendelee kukosa uhai na uhalisia wake tunakuwa tumezalisha yafuatayo;

Sanaa inakosa uthubutu, ubunifu, uhalisia na uhuru wa mitizamo tofauti.

Nchi inakosa fursa ya kujitangaza vyema kupitia sanaa na inazidi kuua vipaji na kupunguza ajira kwa vijana wake.
Sheria za nchi hazitaki mtu asiye member wa majeshi kuvaa sare za jeshi lolote la tanzania au kuvaa sare inayofanana na jeshi. Hizo ni sheria alizotunga mbunge wako
Mm na wewe tuombe mbunge wetu apeleke mswada bungeni sheria hiyo ibadilishwe
 
Back
Top Bottom