Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Hawapo serious na kazi yao wanashindwaje kubuni sare ambayo watakuwa wanatumia kwenye filamu zao, kama wana malengo ya kuelimisha jamii kuachana na uhalifu ni bora kupitia kitengo cha Polisi jamii waombe elimu kidogo namna gani ya kufanya kwenye kazi zao haiwezekani afisa wa Rank ya juu amuite afande askari wa cheo cha chini yaani OCD anamuita afande askari wa cheo cha chini afande nani ataangalia move za hivyo labda watoto.
 
Mpaka kuvaa gwanda si mchezo! Haijalishi ziwe za jeshi au polisi

Wanaume tumezisotea na tumezilia kiapo!

Ila yule askari wa Zenji nahisi alikuwa wa mchongo au aliingia kwa connection. Avae gwanda na aliwe ndogo?! [emoji15][emoji848] Haiwezekani

Samahani nimetoka nje ya mada kidogo ila gwanda ni habari ingine!
Hata sisi tunatambua ni namna gani vazi hili la mapigano makamanda wetu wanalipambania kwa thamani kubwa ya jasho,damu na machozi,

Ila kinachozungumziwa hapa si watu kulitumia kwa nia ya kujifurahisha bali kwa ajili ya kazi kama ambavyo wewe kamanda unalitumia.

Dunia ya sasa imebadilika siyo ile ya zamani siku hizi hata majeshi yanajitangaza kwa njia kama hizo kuweza kupata nguvu ya ushawishi duniani unafikiri ukijifungia peke yako huko porini kuna mtu atakujua.
 
Sheria za nchi hazitaki mtu asiye member wa majeshi luvaa sare za jeshi lolote la tanzania au kuvaa sare inayofanana na jeshi. Hizo ni sheria alizotunga mbunge wako
Mm na wewe tuombe mbunge wetu apeleke mswada bungeni sheria hiyo ibadilishwe
Huku wakijua fika madukani tokea miaka ya zamani hata leo hii nguo zinazolandana na za jeshi zimejaa tele si kwenye special wala mtumba na hawajai kuzuia uingizaji wake nchini kwahiyo ni kama mtego kwa consumers au
 
Hawapo serious na kazi yao wanashindwaje kubuni sare ambayo watakuwa wanatumia kwenye filamu zao, kama wana malengo ya kuelimisha jamii kuachana na uhalifu ni bora kupitia kitengo cha Polisi jamii waombe elimu kidogo namna gani ya kufanya kwenye kazi zao haiwezekani afisa wa Rank ya juu amuite afande askari wa cheo cha chini yaani OCD anamuita afande askari wa cheo cha chini afande nani ataangalia move za hivyo labda watoto.
Umesema wabuni sare? Je, hujui kama anayetizama filamu akiwa haijui Tanzania ndivyo atakavyoichukulia thamani hiyo ya sare kui-value Tanzania ya mawazoni kwake?

Tunapoililia serikali na wawekezaji watie mkono wao katika sekta hii tunamaana ya kuondoa dosari kama hizo ulizozitaja hapa za wasanii kutokuwa hata na mwongozo wa shughuli za kijeshi zinavyoenda yet wanakuwa wamevutiwa kuigiza scene za namna hiyo matokeo yake ni kuzalisha content utumbo.
 
Huku wakijua fika madukani tokea miaka ya zamani hata leo hii nguo zinazolandana na za jeshi zimejaa tele si kwenye special wala mtumba na hawajai kuzuia uingizaji wake nchini kwahiyo ni kama mtego kwa consumers au
Mkuu haya mambo ni kujiongeza ushaambiwa usizae nguo inayofanana na jeshi lolote
Sasa we ukivaa ndo unajitafutia tabuuu
 
Watafute magwanda yanayofanana na sare labda za jeshi la Congo!

CHADEMA wanavaa kama polisi wa India na hakuna anaewabughudhi.

Wasamii wao ni nani ?

Kwa nini wawe juu ya sheria ?

Tulipinga na kulaani Rais wa kiraia JPM luvaa kijeshi sembuse wasanii ?
 
ILA WITO WANGU KWA WASANII, HEBU TOA HUDUMA ILIYE BORA, WATANZANIA WENGI, WAKIWA WAMEJIPUNZISHA, HUANGALIA, KAZI ZENU.
KWA MFANO SASA HIVI, TUNACHANGAMOTO YA WIMBI LA USHOGA, ILA JUZI, AZAMU SINEMA ZETU, NIMEONA MUIGIZAJI MWANAMME AMEWEKA NYWELE KAMA ZA KIKE, NA KAJIPIGIRIA HELENI VIZURI TU, DOSARI HIYO WAHARIRI WA AZAMU WALA HAWAJAIONA.

WATOTO WETU WAO, WANAJUA NDIVYO KIJANA WA KISASA ANAVYOTAKIWA KUWA.
 
Elimu hii wasanii na wanatasnia wengi hawaifahamu na hata kama wanajua uenda haifanyi kazi hivyo iliandikwa kisheria kwenye utekelezaji wake na vyombo vinavyosimamia hiyo haki.
Inafanyakazi vizuri tuu ila nimpaka wadau wa sanaa waamue.
Nishawapa mwangaza.
 
Watafute magwanda yanayofanana na sare labda za jeshi la Congo!

CHADEMA wanavaa kama polisi wa India na hakuna anaewabughudhi.

Wasamii wao ni nani ?

Kwa nini wawe juu ya sheria ?

Tulipinga na kulaani Rais wa kiraia JPM luvaa kijeshi sembuse wasanii ?
Yule ndio mwanajeshi namba moja wewe kwa kipindi cha utawala wake.
 
Hivi badoo uko na mieee tyuuh?? Nkajua ushanisahau eti.

Huko kwenye vitu vya maana nimekuachia wee, uwakilishe genius. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ni ngumu kumsahau aliyesaliti chama
 
Yule ndio mwanajeshi namba moja wewe kwa kipindi cha utawala wakSUDAN, BURKINA FASO, MALI, CHAD zinatawaliwa na jeshi chini ya mwanajeshi.

SUDAN, BURKINA FASO, MALI, CHAD, zinatawalliwa na mwanajeshi. Tanzania tunatawaliwa na raia huria, civilian president.

Jeshi linashika silaha. Linapokea amri ya kunyanyua silaha kutoka kwa raia huria, civilian. anaeitwa Amiri Jeshi. Amiri Jeshi sio mwana jeshi.

Samia Hassan hana mafunzo ya jeshi, hana cheo cha kijeshi, hana silaha ya jeshi ( service weapon), hana namba ya kijeshi, hana alama (insignia) ya kijeshi.

Vyeo vyote vya jeshi vina insignia, vina alama. Samia ana nyota ngapi ? Ana V ngapi begani?

Magufuli aliita fundi cherehani Ikulu akamshonea cadeti za jeshi, Samia nae lady see lady do, kaona haina shida kaiga!

Wanasiasa wanajua Raia hawana uelewa, na viongozi wenyewe hawana uzalendo, ndio maana wanatu take advantage na kuharibu mifumo ya taasisi za utawala bora.
 
SUDAN, BURKINA FASO, MALI, CHAD, zinatawalliwa na mwanajeshi. Tanzania tunatawaliwa na raia huria, civilian rule.

Jeshi linashika silaha. Linapokea amri ya kunyanyua silaha kutoka kwa raia huria, civilian. anaeitwa Amiri Jeshi. Amiri Jeshi sio mwana jeshi.

Rais wa Tanzania sio mwanajeshi. Tanzania tunatawaliwa na civilian, raia huria.

Samia Hassan hana mafunzo ya jeshi, hana cheo cha kijeshi, hana silaha aliyopewa na jeshii, hana namba ya kijeshi

Vyeo vyote vya jeshi vina insignia, vina alama yake. Samia ana nyota ngapi ? Ana V ngapi?

Sena wewe ulivyopata akili ndio Magufuli alikua Rais wako was kwanza kumuona kavaa gwanda.
Pia inachangiwa na media technology ambapo siku hizi ata ukiwa mpitimbi huko kitu kikitokea huku unafahamu...
Miaka ya nyuma mbona Marais walivaa wengine tuliona picha kwenye magazeti tuliokua mjini na access ya kupata gazeti la kila siku.
Kuwa Mwanajeshi au Polisi nambari moja sio lazima kupita jeshini, isipokua inatokana na cheo husika cha Ukuu wa nchi
Ndio nyie msanii akivaa nguo za jeshi mnamvua kwakua ni vilaza hamjui sheria na hamchoshi mafuvu yenu kusoma...siku mjichanganye kwa wanaojua haki zao mtakutana na BWANA PEPSI!!
 
Hili mbona linawezekana na ni rahisi sana. Tatizo vijana wahuni sana hawachelewi kutumia hizo uniform kutapeli watu.
Hii ndiyo ilisababisha serikali, kupiga marufuku mavazi yanayo fanana na yanayovaliwa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Kama mnakumbuka ukisikia tukio la ujambazi, lilikua linahusisha watu waliovalia nguo za polisi, ama JWTZ.

Ila ikitengenezwa utatatibu mzuri, ili vifaa na mavazi yasitumike vibaya, inawezekana ni serikali kuweka kila kitu sawa ikihusisha vyombo vya ulinzi na usalama, na wasanii chini ya Wizara yao.
 
SUDAN, BURKINA FASO, MALI, CHAD, zinatawalliwa na mwanajeshi. Tanzania tunatawaliwa na raia huria, civilian rule.

Jeshi linashika silaha. Linapokea amri ya kunyanyua silaha kutoka kwa raia huria, civilian. anaeitwa Amiri Jeshi. Amiri Jeshi sio mwana jeshi.

Rais wa Tanzania sio mwanajeshi. Tanzania tunatawaliwa na civilian, raia huria.

Samia Hassan hana mafunzo ya jeshi, hana cheo cha kijeshi, hana silaha aliyopewa na jeshii, hana namba ya kijeshi

Vyeo vyote vya jeshi vina insignia, vina alama yake. Samia ana nyota ngapi ? Ana V ngapi?

Magufuli aliita fundi cherehani Ikulu akamshonea cadeti za jeshi, Samia nae lady see lady do, kaona haina shida kaiga!

Wanasiasa wanajua Raia hawana uelewa, na viongozi wenyewe hawana uzalendo, ndio maana wanatu take advantage na kuharibu mifumo ya taasisi za utawala bora.
Utawala bora ni nini kwa tafsiri yako?
 
Watafute magwanda yanayofanana na sare labda za jeshi la Congo!

CHADEMA wanavaa kama polisi wa India na hakuna anaewabughudhi.

Wasamii wao ni nani ?

Kwa nini wawe juu ya sheria ?

Tulipinga na kulaani Rais wa kiraia JPM luvaa kijeshi sembuse wasanii ?

Kwani kwako wewe Rais unamtambua kama nani?

Pili JWTZ unatambua kirefu chake ni nini?

Tatu, Mavazi ya Chadema (kama ulivyoyahita) una hakika ni sare za jeshi la polisi la India?

Nne, Wasanii ni umbile la ndani la jamii (ugusa maisha ya jamii, uburudisha, uelimisha na ni sauti ya jamii) na pia ni taswira au kioo cha jamii/taifa kwa nje kwa maana ya kuumba,kutangaza na kuuza image ya taifa lao.
 
Sena wewe ulivyopata akili ndio Magufuli alikua Rais wako was kwanza kumuona kavaa gwanda.
Pia inachangiwa na media technology ambapo siku hizi ata ukiwa mpitimbi huko kitu kikitokea huku
Okay, wewe mwenye umri mkubwa tuonyeshe basi Nyerere na Mwinyi na Mkapa wakiwa na gwanda za kijeshi.
 
Okay, wewe mwenye umri mkubwa tuonyeshe basi Nyerere na Mwinyi na Mkapa wakiwa na gwanda za kijeshi.
So umekiri kwamba wewe ni dogolasi...
Mimi sikwambii ni yupi kati ya hao nilishaona katinga gwanda
Ila kahalisia nilisha muona.
 
Utawala bora ni nini kwa tafsiri yako?

Raia wote kuwa sawa mbele ya sheria, ni mhimili mmoja wa utawala wa sheria.

Wasanii sio watu wenye special class, ni raia huria, civilians, na Rais sio mwanajeshi, ni raia huria, civilian.

Sheria haiwaruhusu civilians kuvaa military fatigue. It is that simple.
 
Utawala bora ni dhana ya ujumuishaji na ushirikishwaji wa wahusika wote ndani ya jamii katika maamuzi na utekelezaji wake kwa maendeleo yao, kwa kuzingatia misingi ya haki, usawa,uwazi na uwajibikaji.

Nchi yetu ni nchi inayofuata misingi ya utawala bora na jeshi letu ni sehemu ya utawala huo likitambuliwa kama jeshi la wananchi wa Tanzania ni zao la wananchi.

Nchi hii haitawaliwi kijeshi bali jeshi ni chombo cha dola (dola=serikali iliyotokana na wananchi) ambacho uundwa kwa lengo la kusimamia sheria na kutoa ulinzi kwa taifa dhidi ya maadui na raia na mali zao.

Hivyo chombo chenye mamlaka ya mwisho ya kuamua mustakabali wa taifa kupitia dhana ya utawala bora ni RAIA

Na Kiongozi mkuu anayekuwa amechaguliwa na raia kusimamia dhana nzima ya utawala bora ni Rais (naye utokana na Raia) naye uunda Dola (serikali) sasa ndani ya dola ndipo ilipo mihimili mitatu ya serikali kuu, bunge na mahakama kisha ndipo jeshi linakuja kujumuishwa kama chombo cha ulinzi na usalama kwa ajili ya Raia na taifa lao.

Hivyo basi jeshi ni chombo kinachotokana na Raia kinachowajibika chini ya Rais ambaye ni kiongozi wa Raia wote na jeshi likiwemo na Rais huyu ni zao lililotokana na Raia pia.
 
Back
Top Bottom