Ni umri gani ukifika unatakiwa kuanza kuwa makini kuchagua vyakula na vinywaji

Ni umri gani ukifika unatakiwa kuanza kuwa makini kuchagua vyakula na vinywaji

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kuna mzee ni jirani yangu anaishi pamoja na familia yake, na mara nyingi huwa nashinda naye nyakati za jioni pamoja na wikendi tukipiga stori moja mbili tatu pamoja na nasaha enzi akiwa kijana na kipindi hiki cha utawala wa Gen Z

Sasa juzi kama kawaida mida ya jioni nimemkuta kakaa nje kibarazani nikamsalimu vizuri tu, ila ni kama hakuwa sawa. Nikamuuliza akasema anachukia pindi mke wake pamoja na vijana wake wanavyomnyanyasa kwenye issue ya chakula na vinywaji, yaani hawataki anywe soda na hawataki ale vyakula kama KFC anadai muda wote ni mchemsho na mboga mboga.

Mimi nikimwangalia mzee ni kama yuko kwenye umri wa miaka 60, anasema Afya ni muhimu sana ila dunia tunapita kama maradhi yapo ni yapo tu jamani.

Kwa upande wangu nashindwa hata nimwambie nini

1786707450395.png
 
Mm nafukia chochote tuu, maake sioni nikifika huko uzeeni,

Ambavyo silagi na kama hizo KFC, sjui pizza, baga sijawahi kuvielewa hivyo vitu

Kina kimathi wako 80+ na wanagonga kisusio na mbeke sisi tunakimbilia KFC tuonekane vyasaka kwako min -me
Bwashee kula mbege yenye msesewe mwingi sukari na pressure utakua unazisikia tu
 
Me niko early 30s ila mwezi wa 7 joints za miguu zilianza kuniimbia ululuuuuyah wachukuuuucha! Nilikua nakunywa sana soft drinks, junk foods na sweets sasa nabalance zaidi ya mwezi sasa sijanywa chai ya sukari nakunywa maji mengii nilihisi dalili mbaya ila naogopa kupima naji balance kwanza.

Muhimu sana kuangalia unakula nini ukivuka tu 30 mana ushakua anko au aunty.
 
Kuna mzee ni jirani yangu anaishi pamoja na familia yake, na mara nyingi huwa nashinda naye nyakati za jioni pamoja na wikendi tukipiga stori moja mbili tatu pamoja na nasaha enzi akiwa kijana na kipindi hiki cha utawala wa Gen Z

Sasa juzi kama kawaida mida ya jioni nimemkuta kakaa nje kibarazani nikamsalimu vizuri tu, ila ni kama hakuwa sawa. Nikamuuliza akasema anachukia pindi mke wake pamoja na vijana wake wanavyomnyanyasa kwenye issue ya chakula na vinywaji, yaani hawataki anywe soda na hawataki ale vyakula kama KFC anadai muda wote ni mchemsho na mboga mboga.

Mimi nikimwangalia mzee ni kama yuko kwenye umri wa miaka 60, anasema Afya ni muhimu sana ila dunia tunapita kama maradhi yapo ni yapo tu jamani.

Kwa upande wangu nashindwa hata nimwambie nini

Since day one....hapo wazazi tunajukumu la kuelimisha jamii juu ya vyakula bora kuanzia ngazi ya familia.

Mtoto akiendelea kulelewa kwenye mazingira hayo itakuwa rahisi kwake kuepuka vyakula visivyofaa na wala sio kusubiri sijui miaka 30 au 40 ndio mtu aanze kutafuta ushauri juu ya vyakula.
 
Back
Top Bottom