Ni umri gani ukifika unatakiwa kuanza kuwa makini kuchagua vyakula na vinywaji

Ni umri gani ukifika unatakiwa kuanza kuwa makini kuchagua vyakula na vinywaji

Kuna mzee ni jirani yangu anaishi pamoja na familia yake, na mara nyingi huwa nashinda naye nyakati za jioni pamoja na wikendi tukipiga stori moja mbili tatu pamoja na nasaha enzi akiwa kijana na kipindi hiki cha utawala wa Gen Z

Sasa juzi kama kawaida mida ya jioni nimemkuta kakaa nje kibarazani nikamsalimu vizuri tu, ila ni kama hakuwa sawa. Nikamuuliza akasema anachukia pindi mke wake pamoja na vijana wake wanavyomnyanyasa kwenye issue ya chakula na vinywaji, yaani hawataki anywe soda na hawataki ale vyakula kama KFC anadai muda wote ni mchemsho na mboga mboga.

Mimi nikimwangalia mzee ni kama yuko kwenye umri wa miaka 60, anasema Afya ni muhimu sana ila dunia tunapita kama maradhi yapo ni yapo tu jamani.

Kwa upande wangu nashindwa hata nimwambie nini

Kipindi Cha Kunywa Maziwa Pekee Ya Mama (Exclusive Breastfeeding (Miezi 6) baada ya kuzaliwa

Iyo KFC ni chakula?? 🤔.
 
Nijitese kula kwani mm nimechaguliwa kua mlinzi wa dunia ...kuna kupindi niliumwa wakaniambia na presha wakanipangia misosi mm nikaona nateseka tu nikaachana na ratiba zao nikawa nakula nacho kipenda hata presha sijui
Kiukweli mtu mwenye presha asipozingatia ratiba ya ulaji wa kujinyima, presha huwa haipungui bali huendelea kupanda na kuleta madhara ya ndani ya mwili bila yeye kujua.

Presha ni ugonjwa unaoitwa 'silent killer' kwa sababu hauumi na hauna dalili.

Uelewe madhara yake ni kiharusi na magonjwa ya figo, maini na moyo.
 
Me niko early 30s ila mwezi wa 7 joints za miguu zilianza kuniimbia ululuuuuyah wachukuuuucha! Nilikua nakunywa sana soft drinks, junk foods na sweets sasa nabalance zaidi ya mwezi sasa sijanywa chai ya sukari nakunywa maji mengii nilihisi dalili mbaya ila naogopa kupima naji balance kwanza.

Muhimu sana kuangalia unakula nini ukivuka tu 30 mana ushakua anko au aunty.
usikute unapiga nyeto ee dronedrake Poor Brain Mbaga Jr
 
Hapo upo kwenye stage ya Insulin Resistance/ Prediabetes achana achana navy au punguza kwa kiasi kikubwa ili u reverse hiyo hali kabla hujawa Diabetic.
Nyumbani situmii kabisa vitu vyenye sukari, ila Kuna eneo nikienda unakuta hakuna chakula zaidi ya chai na maandazi, au mihogo ya kukaanga na chai 🤔
Nabutua mara Moja nasubiria mateso ya siku nzima
 
Nyumbani situmii kabisa vitu vyenye sukari, ila Kuna eneo nikienda unakuta hakuna chakula zaidi ya chai na maandazi, au mihogo ya kukaanga na chai 🤔
Nabutua mara Moja nasubiria mateso ya siku nzima
Kwani kubutua kwa dharula siku moja moja unadhani kuna shida?

Shida ni ufakamizi kuufanya ndiyo life stile yako!
 
Nyumbani situmii kabisa vitu vyenye sukari, ila Kuna eneo nikienda unakuta hakuna chakula zaidi ya chai na maandazi, au mihogo ya kukaanga na chai 🤔
Nabutua mara Moja nasubiria mateso ya siku nzima
Una umri gani

Katika mazingira hayo inatakiwa ule hiyo mihogo kama ni vipande vidogo vitano tuu bila chai yenye sukari kula hivyo kunywa na maji usiposhiba utakula tena baade. Au kama ni maandazi madogo matatu bila chai yenye sukari.

Jitahidi ukapime kipimo cha sukari kinaitwa HBA1C uone wastani kwa sukari yako wa miezi 3 ipoje.
 
Ukifika ngazi ya tatu(30's) hapo kama hukula hovyohovyo huko ngazi ya kwanza na ya pili vya kutosha,perhaps umetokea life gumu basi, hapo hakikisha unakula TIZI daily mara moja kwa siku ili uendelee kula majunk foody na mabeer na mabroiler bila tabu.

Na kama upo ngazi ya nne( 40's).
Hapo napo kama hukula maisha ulikuwa bado unajisaka kwa miongo mitatu na bado hukujipata.My friend hapo unatakiwa upige TIZI daily mara mbili(asubuhi na jioni) kama bado unataka uendelee kutafuta mifupa angali meno bado yapo.

Kama upo ngazi ya tano na kuendelea( 50's and above),
na hukula vya kutosha ukiwa kwenye your 20's,30's na 40's.Amua moja tu hapo kufa mapema au kuishi kwa masharti ya Janabi walau uongeze miaka 15 mingine ya kuendelea kuzurura hapa duniani.

📌Hakuna cha bure,ukitaka cha uvunguni sharti uiname!!!
 
Aaaah ila sio mti exactly Kuna namna unakuwa kma maua haya ya kutembea hv wenye rangi ya kijani almost na ni majani ya mbuzi 🤔
Huo huo sisi watu Marangu/Wavunjo tunauita Mkananga.

Mfifina naujua na ni majani ya mbuzi pia na huwa una maji sana usipokauka vizuri kuni zake haziwaki vizuri na zinatoa moshi sana.
 
Back
Top Bottom