Ni vema Chadema iache kuchukua watu kutoka CCM kwani wanawagharimu

mtimawachi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
2,106
Reaction score
3,158
Kwanza nieleze kiitikadi mimi CCM (mshabiki), ila u-CCM wangu haunizuii kuona mabaya/mazuri au 'mazurimabaya' ya chama changu au chama kingine.

Chadema ni chama cha upinzani tena kikuu lakini mimi naomba nikiite chama mbadala au chama shindani kwani kwa kipindi kifupi Chadema kimeweza kubadili siasa za Tanzania.

Nafikiri hata mzee Kikwete(shikamoo) akiulizwa katika utawala wake chama gani kilimsumbua jibu litakuwa Chadema.

Nina uhakika hata vyama vingine vya upinzani havikupenda mafanikio yake vikaanza kuipiga vita Chadema.

Napenda nimpongeze kamanda wa anga mbowe(kama taasisi) kwa kuhimili mikiki mizito hasa katika awamu ya mwisho ya Kikwete na awamu yote ya komandoo magufuli(RIP).

Mbowe siyo tu anastahili pongezi bali heshima nayo anastahili.

Pamoja na yoote Chadema ina mapungufu makubwa yanayojirudiarudia na ninaitaka iache mara moja.

Iache kuchukua watu kutoka CCM kwani wanawagharimu, mwangalie nyalandu alivyokuwa akijigamba juzi!

Iache kuwaona viongozi(marais) wa CCM kama ni wakombozi au wadumazaji wao.

Iache kushadadia migogoro ya CCM

Mbowe aachie uenyekiti akaungane na Mzee Mtei(shikamoo) kama mshauri.

Mashabiki wa Chadema waache kutoa matusi/dharau/kebehi pindi waambiwapo ukweli au mtu akitoa mtazamo tofauti nao

Iwaache wale wanawake 19 waendelee

Asanteni!
 
Hapo kwa kuwaacha wale covid 19 sikuungi mkono..,maana wale ni wahuni, wameshafukuzwa BUNGE LIHESHIMU KATIBA.
Sikatai mkuu ila hili jambo lilitakiwa limalizwe kabla halijawa na sura hii,kwa sasa kila wanachofanya chadema kwa hawa covid kinadhalilika chama
 
CCM shida enu ni mbowe.mmeshindwa kumuua,mmeshindwa kumteka sasa mmeamua mumuombe atoke.Nyerere ameongoza CCM na TANU kwa kipindi gan?
 
Matamanio ya makada wengi wa chama tawala ni ya kwamba CDM iendeshwe kimfumo kama CCM. Hawatambui ya kwamba hizi ni taasisi mbili za kisiasa zinazotofaitiana kimuundo, kiuendeshaji, kisera, na kiitikadi ijapokuwa zote zina lengo moja kuu la kuishika dola.

Mambo yote yaliyogusiwa hapo juu yameainishwa kupitia katiba za vyama hivi. Kwa hiyo basi kabla ya kuanza kuonyesha mapungufu na kupinga mfumo wa uendeshaji wa CDM itakupasa urudi katika katiba yake ili uweze kuutambua vyema jinsi ulivyowekwa.

Ni vyema mtu anapokuja na "critisms" ni vyema pia akaja na "drawn excerpt" kutoka ktk katiba ya CDM kwa lengo la kuonyesha na kuainisha ya kwamba Mbowe anakiuka matakwa ya katiba ya chama kwa kuzidi kung'ang'ania na kuihodhi nafasi ya uenyekiti taifa wa chama.
 
Unamfungia mtu account zake zote, unaharibu raslimali zake zote zinazomwingizia kipato, unamuweka gelezani kwa makosa ya kubumba kumkomoa, ili akupigie magoti.

Mtu huyo anavumilia yote haya kwa zaidi ya miaka 3 bila kutoa kauli yoyote ile.

Aisee semeni yote ila kwa Mh. Mbowe ameandika historia kwa kizazi hiki na kizazi kijacho watamsoma katika historia kwamba alikuwepo Gwiji wa Siasa, mstahamilivu na mtu asiyekurupuka kwa maamuzi.
 
Ni vyema mtu anapokuja na "critisms" ni vyema pia akaja na "drawn excerpt" kutoka ktk katiba ya CDM kwa lengo la kuonyesha na kuainisha ya kwamba Mbowe anakiuka matakwa ya katiba ya chama kwa kuzidi kung'ang'ania na kuihodhi nafasi ya uenyekiti taifa wa chama.
hako ka jamaa ni ka opportunist, sidhani kama hata kana akili ya kuja na hiyo drawn excerpt - kameona maisha magumu CDM hela zimeisha kamejisalimisha..
 
CCM shida enu ni mbowe.mmeshindwa kumuua,mmeshindwa kumteka sasa mmeamua mumuombe atoke.Nyerere ameongoza CCM na TANU kwa kipindi gan?
Mkuu ccm wananufaika zaidi na uenyekiti wa MBOWE kuliko chadema
 
Unamfungia mtu account zake zote, unaharibu raslimali zake zote zinazomwingizia kipato, unamuweka gelezani kwa makosa ya kijinga miezi 4, Unamtisha tisha, unafanya kila liwezekano akwame kila kitu ili baadaye akubali ku sallender.... akupigie magoti lakini wapi.

Mtu huyo anavumilia yote haya kwa miaka 3.

Aisee semeni yote ila kwa Mh. Mbowe ameandika historia kwa kizazi hiki na kizazi kijacho watamsoma katika historia kwamba alikuwepo Gwiji wa Siasa, mstahamilivu na mtu asiyekurupuka kwa maamuzi.
Uko sahihi mkuu,ila chadema inahitaji changamoto mpya,mbowe awe mshauri
 
Matamanio ya makada wengi wa chama tawala ni ya kwamba CDM iendeshwe kimfumo kama CCM. Hawatambui ya kwamba hizi ni taasisi mbili za kisiasa zinazotofaitiana kimuundo, kiuendeshaji, kisera, na kiitikadi ijapokuwa zote zina lengo moja kuu la kuishika dola.

Mambo yote yaliyogusiwa hapo juu yameainishwa kupitia katiba za vyama hivi. Kwa hiyo basi kabla ya kuanza kuonyesha mapungufu na kupinga mfumo wa uendeshaji wa CDM itakupasa urudi katika katiba yake ili uweze kuutambua vyema jinsi ulivyowekwa.

Ni vyema mtu anapokuja na "critisms" ni vyema pia akaja na "drawn excerpt" kutoka ktk katiba ya CDM kwa lengo la kuonyesha na kuainisha ya kwamba Mbowe anakiuka matakwa ya katiba ya chama kwa kuzidi kung'ang'ania na kuihodhi nafasi ya uenyekiti taifa wa chama.
Mkuu haina haja ya hiyo drawn nini sijui,mapungufu ya chadema yapo wazi.
Kumbuka ujio wa Mzee LOWASA(shikamoo),tuliwaonya,hata hiyo katiba yenu unadai mnafuata mliikana mkamfanya awe mgombea,makosa yaleyale mkayarudia kwa akina Nyalandu halafu mkiambiwa mnajitia ujuaji
 
Kwanza nieleze kiitikadi mimi CCM (mshabiki), ila u-CCM wangu haunizuii kuona mabaya/mazuri au 'mazurimabaya' ya chama changu au chama kingine.

Chadema ni chama cha upinzani tena kikuu lakini mimi naomba nikiite chama mbadala au chama shindani kwani kwa kipindi kifupi Chadema kimeweza kubadili siasa za Tanzania.

Nafikiri hata mzee Kikwete(shikamoo) akiulizwa katika utawala wake chama gani kilimsumbua jibu litakuwa Chadema.

Nina uhakika hata vyama vingine vya upinzani havikupenda mafanikio yake vikaanza kuipiga vita Chadema.

Napenda nimpongeze kamanda wa anga mbowe(kama taasisi) kwa kuhimili mikiki mizito hasa katika awamu ya mwisho ya Kikwete na awamu yote ya komandoo magufuli(RIP).

Mbowe siyo tu anastahili pongezi bali heshima nayo anastahili.

Pamoja na yoote Chadema ina mapungufu makubwa yanayojirudiarudia na ninaitaka iache mara moja.

Iache kuchukua watu kutoka CCM kwani wanawagharimu, mwangalie nyalandu alivyokuwa akijigamba juzi!

Iache kuwaona viongozi(marais) wa CCM kama ni wakombozi au wadumazaji wao.

Iache kushadadia migogoro ya CCM

Mbowe aachie uenyekiti akaungane na Mzee Mtei(shikamoo) kama mshauri.

Mashabiki wa Chadema waache kutoa matusi/dharau/kebehi pindi waambiwapo ukweli au mtu akitoa mtazamo tofauti nao

Iwaache wale wanawake 19 waendelee

Asanteni!
Sisi CHADEMA Covid-19 tushawaacha, ila tutaisema serikali kwa upuuzi huo
 
Hapo kwa kuwaacha wale covid 19 sikuungi mkono..,maana wale ni wahuni, wameshafukuzwa BUNGE LIHESHIMU KATIBA.

tatizo ni kwamba mnatumia mda mwingi sana kuwapa headlines wale wanawake, kwa mda huu mnabidi muweke kila kitu open hatuwatambui then baada ya hapo rudini kutengeneza chama sasa, wekeni uongozi ukae vizuri mbowe astaafu watu wenye mawazo mapya watake over then sehem ya intelijensia ikkuzwe, then anzeni upya yaliopita yasahaulike, ccm ikianza tena yale mambo yake ya zamani ya rushwa hatutasita kuipiga chini lakini wakati tunaipiga chini kue na mbadala mzuri sasa! mkifanya ivo tu hata uchaguzi ujao tukiona ccm haieleweki tunawasupport sio shida mradi nchi isogee mbele sasa kwa kwel
 
hako ka jamaa ni ka opportunist, sidhani kama hata kana akili ya kuja na hiyo drawn excerpt - kameona maisha magumu CDM hela zimeisha kamejisalimisha..
Mh! umesoma uzi vizuri lakini au ndiyo kama kawada yenu ya ujuaji
 
Kwanza nieleze kiitikadi mimi CCM (mshabiki), ila u-CCM wangu haunizuii kuona mabaya/mazuri au 'mazurimabaya' ya chama changu au chama kingine.

Chadema ni chama cha upinzani tena kikuu lakini mimi naomba nikiite chama mbadala au chama shindani kwani kwa kipindi kifupi Chadema kimeweza kubadili siasa za Tanzania.

Nafikiri hata mzee Kikwete(shikamoo) akiulizwa katika utawala wake chama gani kilimsumbua jibu litakuwa Chadema.

Nina uhakika hata vyama vingine vya upinzani havikupenda mafanikio yake vikaanza kuipiga vita Chadema.

Napenda nimpongeze kamanda wa anga mbowe(kama taasisi) kwa kuhimili mikiki mizito hasa katika awamu ya mwisho ya Kikwete na awamu yote ya komandoo magufuli(RIP).

Mbowe siyo tu anastahili pongezi bali heshima nayo anastahili.

Pamoja na yoote Chadema ina mapungufu makubwa yanayojirudiarudia na ninaitaka iache mara moja.

Iache kuchukua watu kutoka CCM kwani wanawagharimu, mwangalie nyalandu alivyokuwa akijigamba juzi!

Iache kuwaona viongozi(marais) wa CCM kama ni wakombozi au wadumazaji wao.

Iache kushadadia migogoro ya CCM

Mbowe aachie uenyekiti akaungane na Mzee Mtei(shikamoo) kama mshauri.

Mashabiki wa Chadema waache kutoa matusi/dharau/kebehi pindi waambiwapo ukweli au mtu akitoa mtazamo tofauti nao

Iwaache wale wanawake 19 waendelee

Asanteni!
Hivi ukiulizwa maswali yafuatayo utajibuje?
1. Lengo la hopja yako ni nini?
2. Kwanini unapenda sana Mbowe aondoke kwenye uongozi ndani ya Chadema wakati wewe mwenyewe umesema siyo mwanachama wa Chadema bali CCM?
3. Kwanini mnalazimisha Covid-19 waendelee kuwa wanachama wa Chadema?
4. Nini kiliwashinda hadi aliyejiita Jiwe akaondoka? Hicho kilichowashinda ndicho kitaendelea kuwaadhibu kwa kujiona ninyi ni wa milele na mnaweza kufanya lolote, bila kujua kuwa huo ni ubatili tu. Kama Chadema ni dhaifu chini ya Mbowe si ndio furaha yenu? Sasa kelele za nini?
5. Tangu lini mwanaCCM au CCM ikawa na nia njema na Chadema?
6. Kwanini msiendelee na mambo yenu?
 
Tatizo lenu kubwa ndo hili sasa, Mbna katoa ushauri mzuri tu, kawasingizia? wengi tunapenda nchi iende vizuri lakini sasa tunakosa chama mbadala mkipewa ushauri mnakua viburi
 
Mkuu haina haja ya hiyo drawn nini sijui,mapungufu ya chadema yapo wazi.
Kumbuka ujio wa Mzee LOWASA(shikamoo),tuliwaonya,hata hiyo katiba yenu unadai mnafuata mliikana mkamfanya awe mgombea,makosa yaleyale mkayarudia kwa akina Nyalandu halafu mkiambiwa mnajitia ujuaji
CDM ni chama ambacho bado kinakuwa, kina mambo mengi ya kujifunza kutokana na makosa kinayoyafanya,. Kinazidi kuimarika na kuumgwa mkono na Watanzania makini walokuwa wengi.

Licha ya hujuma zinazofanywa na CCM pamoja na vyombo vya dola dhidi yake, ushahidi uko wazi kuwa ni chama bora cha upinzani na chenye nguvu na ushawishi.

Kina hazina kubwa ya viongozi waliokuwa bora na kupikwa vizuri kiuongozi. Wewe ebu jaribu kuangalia wale makada wachache waliounga juhudi na kuhamia CCM, wengi wameaminika na kuteuliwa kuwa manaibu mawaziri ndani ya chama hiki kikongwe kilichozeeka kisera na kimaono.
 
tatizo ni kwamba mnatumia mda mwingi sana kuwapa headlines wale wanawake, kwa mda huu mnabidi muweke kila kitu open hatuwatambui then baada ya hapo rudini kutengeneza chama sasa, wekeni uongozi ukae vizuri mbowe astaafu watu wenye mawazo mapya watake over then sehem ya intelijensia ikkuzwe, then anzeni upya yaliopita yasahaulike, ccm ikianza tena yale mambo yake ya zamani ya rushwa hatutasita kuipiga chini lakini wakati tunaipiga chini kue na mbadala mzuri sasa! mkifanya ivo tu hata uchaguzi ujao tukiona ccm haieleweki tunawasupport sio shida mradi nchi isogee mbele sasa kwa kwel
Asante mkuu,ila hawa jamaa hawaambiliki
 
Back
Top Bottom