CDM ni chama ambacho bado kinakuwa, kina mambo mengi ya kujifunza kutokana na makosa kinayoyafanya,. Kinazidi kuimarika na kuumgwa mkono na Watanzania makini walokuwa wengi.
Licha ya hujuma zinazofanywa na CCM pamoja na vyombo vya dola dhidi yake, ushahidi uko wazi kuwa ni chama bora cha upinzani na chenye nguvu na ushawishi.
Kina hazina kubwa ya viongozi waliokuwa bora na kupikwa vizuri kiuongozi. Wewe ebu jaribu kuangalia wale makada wachache waliounga juhudi na kuhamia CCM, wengi wameaminika na kuteuliwa kuwa manaibu mawaziri ndani ya chama hiki kikongwe kilichozeeka kisera na kimaono.