Naona kuna mkanganyiko huko CCM. Ni muda sasa nimekuwa nikiwasoma makada kadhaa wakidai kuwa CHADEMA ilishajifia miaka hasa tangu “wamtupe” Dr. Slaa na kumchukua Lowassa. Kwamba hicho chama kilishapoteza ushawishi na Magufuli ndio akakizika rasmi kwa utendaji wake “uliotukuka”!
Sasa yaelekea hata kivuli cha CHADEMA kinaleta kizaazaa. Huko Bungeni unashangaa kusikia spika na waheshimiwa wakitumia muda mwingi kujibu kauli za wana CHADEMA zilizotolewa kwenye mitandao huku miswada rasmi ikipata superficial attention!
Anyway, uko sahihi kabisa kwamba CHADEMA ndicho chama rasmi cha wananchi katika kukabiliana na dola. Na kitaendelea “kutisha” hadi siku nchi itakapokaa sawa. Sina shaka wenye uelewa ndani ya dola/CCM wanajua hakuna namna ya kuiua CHADEMA. Hakika Mbowe amefanikiwa kutengeneza “zimwi” ambalo limeshampita kimo hata yeye. Btw. hakuna kiongozi wa CHADEMA mwenye uwezo wa kuwahalalisha covid-19. Ni wanachama na mashabiki wa chama ndio wataamua. Kwanza hadi sasa hao watu wameshapoteza ile “touch” special ya ki-CHADEMA waliyokuwa nayo kabla. Ndugai keshawapaka nuksi ya CCM.