Ni vema Chadema iache kuchukua watu kutoka CCM kwani wanawagharimu

Mkuu chadema ni chama kizuri na kilipokelewa vizuri na watanzania,isipokuwa haitaki kujibadili ili iandane na wakati
 


Hahaahaaa! Mkuu kwani kuwaacha maana yake nini? Wewe umesikia Chadema imemng'ang'ania mtu?

Kama ni hawa 19 mbona walishafukuzwa zamani? Au kwa maana nyingine, Chadema ilikwisha awaacha!

Au mapendekezo yako wewe ni yapi? Au labda sasa unapendekeza kuwa Chadema isiwaache?

Hebu labda funguka zaidi mkuu.
 
Uko sahihi mkuu,ila chadema inahitaji changamoto mpya,mbowe awe mshauri
CDM ni taasisi huru, ina katiba na kanuni zake za kuendesha chama!! sidhani inahitaji ushauri toka Lumumba!!
 
kuna jambo spika atakuwa anafaidika nalo kuwang'ang'ania hawa covid 19, asije kuwa anakula ten percent ya posho zao...ohooo dunia hii ina mengi wakuu.
 
ULIANZA VIZURI LAKINI HAPO MWISHO UMEANDIKA KITU AMBACHO HAKIWEZEKANI MAKENGEZA AACHIE UENYEKITI? NANI KASEMA WAKATI YEYE ANAJUWA KILE CHAMA CHA KWAKE
 
Sawa na asante kwa point hizi lakini unakosea point mbili: Mbowe kuacha uenyekiti, nakwambia CDM haitaenda vizuri mbowe anaendesha chama kwa stail ambayo itabidi tupate mtu wa kuaminika na mwenye umiliki (sense of ownership) iliyo na nguvu na ya dhati kama Mbowe. Fikiria angepewa enyekiti Nyalandu mwaka jana saa hii CDM ingekuwa wapi?

Pili covid 19 huwezi kuwatetea hata kidogo kama una akili nzuri walishakataliwa ndani ya chama sasa unataka wawe wabunge kwa ticket ya chama gani? Uvunjifu mkubwa wa katiba na Mbowe anasimamia hilo vizuri kabisa. Adumu M/lkiti Mbowe!!!!
 
kuna jambo spika atakuwa anafaidika nalo kuwang'ang'ania hawa covid 19, asije kuwa anakula ten percent ya posho zao...ohooo dunia hii ina mengi wakuu.

Hakuaminika Jiwe ije kuwa huyu? Huko mboga mboga nani msafi?

La maana kuliko yote kwa vile Chadema ilikwisha wafukuza na wabunge mjadala huu sasa kujipanga kivingine.

Chakula huiva tu pale kinapokuwa kimetokota kikamilifu. Si kabla.

Muda wa mipangilio zaidi ya mapambano ni huu.
 
Nilikuwa nataka kama imeshaamua kuwaacha basi isiwazungumzie,watulie tu kwani kama chama kina mengi ya kufanya
 
Hapo ndipo nataka pabadilike,uenyekiti uwe taasisi siyo mtu.Kwa point yako MBOWE akifa leo maana yake chadema inakufa si ndio?
 
Hapo ndipo nataka pabadilike,uenyekiti uwe taasisi siyo mtu.Kwa point yako MBOWE akifa leo maana yake chadema inakufa si ndio?
Hayo ya uenyekiti ni mengi na yanajadilika; hata ccm tutenganishe m/kiti wa chama na rais wa nchi na pia uenyekiti uwe taasisi, inawezekana lakini ngumu. Vyama vya upinzani vinahitaji watu wa kujitoa mhanga kama akina Mbowe.

Imagine Halima Mdee angepewa uenyekiti leo CDM ingekuwa wapi?!!!
 
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu.!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura??
 
Nilikuwa nataka kama imeshaamua kuwaacha basi isiwazungumzie,watulie tu kwani kama chama kina mengi ya kufanya

😂😂😂😂😂😂😂😂 Kazi kweri kweri!

Kwa hiyo Chadema ikiwazungumzia roho zenu zinataka kuwatoka kwa kihoro?!

Basi kama ni hivyo rejea kwenye uzi wako ukafanye marekebisho husika kuyaweka hayo wazi. Labda kwa hivyo utaeleweka. Kwani kama kuachwa hawa ni zamani wala si wa leo.

Hata hivyo nisiache kukumbusha, mambo ya Ngoswe, huachiwa Ngoswe mwenyewe. Chadema ni taasisi kubwa mno kutegemeana mawazo yenye ufanisi kwake, kutokea CCM.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu.!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura??
Mzee Tingatinga aliwagalagaza wagombea wote.... ila mlichomfanyia huyu Mzee hatakaa awasahau milele... hadi wa leo haamini jina lake halikurudi !!

Nyarandu kwa Lissu ni mwepesi saaana - na kama ilikuwa gia yenu kwamba agombee URAIS then ajitoe dakika ya mwisho CCM mlifeli...watu walimshtukia mapemaaa
 
Kwa hiyo kwenye chama chenu mtu wa kujitoa mhanga ni MBOWE peke yake? sasa kuna haja gani kujiita makamanda?
 
ULIANZA VIZURI LAKINI HAPO MWISHO UMEANDIKA KITU AMBACHO HAKIWEZEKANI MAKENGEZA AACHIE UENYEKITI? NANI KASEMA WAKATI YEYE ANAJUWA KILE CHAMA CHA KWAKE
Hahahahaaa! basi kama ni hivyo wawaachie na wale wanawake 19 wale.Na bi Halima nasikia anautaka uenyekiti!
 
kuna jambo spika atakuwa anafaidika nalo kuwang'ang'ania hawa covid 19, asije kuwa anakula ten percent ya posho zao...ohooo dunia hii ina mengi wakuu.
Mkuu acha tu awang'ang'anie,hawa watu wanatumia gharama kubwa kushinda nafasi zao halafu watoke tu kindezindezi! Nilimshuhudia mgombea ubunge kule MBARALI bwana MWANG'OMBE jinsi alivyotumia gharama na bado amefeli.Waacheni wamama hawa
 
Ushauri wangu ni huu

Ya Ngoswe mwachie Ngoswe.

Sikio la kufa halisikii dawa.
 
We ni nani hadi uwashauri chadema?
Huwa wasikii ushauri wale. Cha mno jia fae kwa natusi makali [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo lenu kubwa ndo hili sasa, Mbna katoa ushauri mzuri tu, kawasingizia? wengi tunapenda nchi iende vizuri lakini sasa tunakosa chama mbadala mkipewa ushauri mnakua viburi
Kwanini mnaichagua Chadema tu kuipa ushauri. Mbona kuna TLP, ADA TADEA, N.K? Ushauri wenu Chadema haitaki mbona mnangángánia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…