Ni vigumu sana kuishi na Binti asiye ndugu yako wa damu pamoja. Hivi wake zetu mnalitambua hili?

Ni vigumu sana kuishi na Binti asiye ndugu yako wa damu pamoja. Hivi wake zetu mnalitambua hili?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari wana JF,

Waanaume tumeumbwa na macho ya matamanio na ndio mara nyingi hutupelekea kufanya maamuzi mengi ambayo yanakuwa sio sahihi.

Hivi mwanaume rijali anawezaje kaa na binti wa kazi ambaye amekomaa na kakamilika vizuri? Kihalisia ni ngumu sana na wengi huishia kuwafanya wake wenza, je wake zetu wanalitambua hili na wanatuchukuliaje?

Ingefaa kwa hili wajifunze na waangalie namna nzuri ya kutunza familia maana wengine ni wavivu tu.
 
Kumvua nguo na kuruhusu house maid wako kuiona tupu yako ndani ya nyumba unakoishi na watoto wako na mkeo huo ni ulimbukeni na umaskini wa akili,kwanza itamjengea mkeo kudharaulika mbele yake na sijui mtapishana vipi humo ndani!

Au utajifariji umeowa wake wawili?
 
Mkeo nae huko aliko anasema Ni ngumu Sana kuendelea kuangaliana tu na dereva wa Bwodaboda yake ambae ni rijali halafu wasitiane.
Hahahaha mambo haya magumu sana
 
Acha tamaa.
Mchukulie kama mwanao, mdogo wako ama dada yako wala roho wa matamanio hatakua juu yako.

La sivyo wewe ni mzinzi na mshenzi unataka kuutetea ufuska wako kwa kijisababu cha urijali.
Hahahaha mimi nimeandika ukweli tu
 
Habari wana JF ,

Waanaume tumeumbwa na macho ya matamanio na ndio mara nyingi hutupelekea kufanya maamuzi mengi ambayo yanakuwa sio sahihi.

Hivi mwanaume rijali anawezaje kaa na Binti wa kazi ambae amekomaa na kakamilika vizuri?

Kihalisia ni ngumu sana na wengi huishia kuwafanya wake wenza , je wake zetu wanalitambua hili na wanatuchukuliaje?

Ingefaa kwa hili wajifunze na waangalie namna nzuri ya kutunza familia maana wengine ni wavivu tu.
Wewe ulielewa nini katika amri ileeee isemayo,"WALA USIMTAMANI MJAKAZI WA JIRANI YAKO"?.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mengi yanatamanika mbele za macho, kuchagua umtamani nani, ufanye nini na nani, ufanye naye wapi na utayari wa kupokea matokeo ya matendo yako, ndicho kinachotofautisha matumizi sahihi ya akili.
 
Kumvua nguo na kuruhusu house maid wako kuiona tupu yako ndani ya nyumba unakoishi na watoto wako na mkeo huo ni ulimbukeni na umaskini wa akili,kwanza itamjengea mkeo kudharaulika mbele yake na sijui mtapishana vipi humo ndani!

Au utajifariji umeowa wake wawili?
Mbona Prophet Ibrahim hakudharaulika mbele ya mkewe Hajra?

Kama humli subiri wapangaji wenzio wanyatie usiku.
 
Kuna shida kutoka kwenye huduma unayopatiwa na mke wako ndio maana umewaza hivi la sivyo usingesema hivi kabisa.
 
Mnaweza kuepusha migogoro mingi sana kwakutotembea na watu wa karibu na wenza wenu.

Uwezo wa kucontrol tamaa mmepewa na upo ndani ya uwezo wenu, ama sivyo endeleeni kuuwana tu.
 
Ni rahisi sana kuandika haya ikiwa huna ambao wanasababisha huyo msaidizi awepo laiti kama wapo na unaona vile huwa mnapata shida vile msaidizi asipokuwepo basi hisia zako utapeleka pengine.
 
Back
Top Bottom