Ni vigumu sana Tundu Lissu kufanikiwa kisiasa kwasababu ni mtu wa tuhuma na wala hathamini michango ya wanasiasa wenzake ndani na nje ya Chama

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Ni vigumu sana Tundu Lissu kufanikiwa kisiasa kwasababu ni mtu wa tuhuma na wala hathamini michango ya wanasiasa wenzake ndani na nje ya Chama

Tundu Lissu ni mtu complicated sana na ni vigumu kufanya nae kazi na hawezi kufanikiwa kisiasa hata umfanyie jema gani hawezi kukuthamini. Pamoja na mapungufu ya kituhuma aliyomrushia Mh Mbowe bado anaonekana hathamini mema yote Mh Mbowe aliyofanyia CHADEMA

Tuhuma za Lissu kwa Mh Mbowe ni kana kwamba Mh Mbowe hakuna hata jema moja alilowahi kufanya

Haiishii hapo tu anaenda mbali hata kuituhumu Serikali na raisi pamoja na jitihada zake inazofanya bado haoni jema hata moja linalofanywa na CCM

Amekuwa mtu wa kutuhumu CCM, CHADEMA na hata Mwenyekiti aliyepita Mh Mbowe kana kwamba hakuna mwema hata mmoja yeye peke yake ndiye mwema inawezekana hata mke wake anapokea tuhuma kila mara

Kwa Mwanasiasa mwenye utu, heshima, adabu hawezi kwenda hewani kutuhumu na kumchafua Mwenyekiti wake na Chama chake hadharani kama alivyofanya bali hayo angeyafanya kwa siri ndani ya mikutano ya Chama chake yaishie humo ndani ya Chama na sio nje

Kurusha tuhuma za Chama chako kwenye hadhira ya Taifa ni sawa na kutangaza madhaifu ya mkeo au mmeo mbele za watu badala ya kuyajadili chumbani

Idadi kubwa ya Watanzania hawatumii Muheshimiwa badala yake wanatumia Tundu Lissu kwasababu ya kukosa heshima kwa watangulizi wake

Huwezi kuheshimiwa na watu kama huheshimu wenzako

Safari ya Lissu kufanikiwa kisiasa haipo, sana sana anapoteza muda na swala la uraisi aachane nalo kwasababu hakuna mtu atakayempa nchi mtu asiye na heshima wala adabu
Nasemaje swala la uraisi aachane nalo kabisa na sahau kabisa hakuna mafanikio yeyote afadhali akalime

Kufanikiwa kwake kuwa Mwenyekiti haina tofauti na dhuluma au kutoa kafara
Kapata uenyekiti kwa kuchafua watu ni sawa na kuwatoa kafara na wala mafanikio hayo hayana baraka yeyote kwake ni sawa na mwizi aliyefanikiwa kwa kuumiza wenzake
 
Unadhani angepata hata huo uenyekiti....watanzania si vipofu
 
Afanikiwe mara ngapi, kaisha kuwa mbuge miaka kibao, ameisha kuwa makam mwenyekiti Chadema na sasa mwenyekiti wa chadema.. unataka apate mafanikio gani tena..
 
Uenyekiti wake wa kukukashifu na kurusha tuhuma kwa watangulizi wake hauna baraka yeyote
 
Afanikiwe mara ngapi, kaisha kuwa mbuge miaka kibao, ameisha kuwa makam mwenyekiti Chadema na sasa mwenyekiti wa chadema.. unataka apate mafanikio gani tena..
Anataka uraisi
 
Mbona tayari amefanikiwa kisiasa? Nyie team mbowe and alike mnawewesuka sana na mheshimiwa Lissu. Kwa sasa mheshimiwa Lissu ndio super brand ya siasa nchini.
 
Mpaka alipofika amefanikiwa, huo uenyekiti hapo CHADEMA waliutaka wengi walipoukosa wakahama chama yeye amekomaa mpaka akaupata bado unamuona hajafanikiwa?
 
Wala sio team Mbowe kufanikiwa kwake kuwa Mwenyekiti haina tofauti na dhuluma au kutoa kafara
Kapata uenyekiti kwa kuchafua watu ni sawa na kuwatoa kafara na wala mafanikio hayo hayana baraka yeyote kwake ni sawa na mwizi aliyefanikiwa kwa kuumiza wenzake
 
Mpaka alipofika amefanikiwa, huo uenyekiti hapo CHADEMA waliutaka wengi walipoukosa wakahama chama yeye amekomaa mpaka akaupata bado unamuona hajafanikiwa?
Mafanikio ya kuchafua wengine yana baraka zipi sawa na mwizi tu
 
Hilo la kuchafua dogo kabisa, wanaouwa wenzao ili wafanikiwe mbona haujalizungumza
Hata yeye alichofanya ni kumuua Mh Mbowe ili apate uenyekiti, hana tofauti na mwizi au muuaji
 
Ni vigumu sana Tundu Lissu kufanikiwa kisiasa kwasababu ni mtu wa tuhuma na wala hathamini michango ya wanasiasa wenzake ndani na nje ya Chama

Tundu Lissu ni mtu complicated sana na ni vigumu kufanya nae kazi na hawezi kufanikiwa kisiasa hata umfanyie jema gani hawezi kukuthamini. Pamoja na mapungufu ya kituhuma aliyomrushia Mh Mbowe bado anaonekana hathamini mema yote Mh Mbowe aliyofanyia CHADEMA

Tuhuma za Lissu kwa Mh Mbowe ni kana kwamba Mh Mbowe hakuna hata jema moja alilowahi kufanya

Haiishii hapo tu anaenda mbali hata kuituhumu Serikali na raisi pamoja na jitihada zake inazofanya bado haoni jema hata moja linalofanywa na CCM

Amekuwa mtu wa kutuhumu CCM, CHADEMA na hata Mwenyekiti aliyepita Mh Mbowe kana kwamba hakuna mwema hata mmoja yeye peke yake ndiye mwema inawezekana hata mke wake anapokea tuhuma kila mara

Kwa Mwanasiasa mwenye utu, heshima, adabu hawezi kwenda hewani kutuhumu na kumchafua Mwenyekiti wake na Chama chake hadharani kama alivyofanya bali hayo angeyafanya kwa siri ndani ya mikutano ya Chama chake yaishie humo ndani ya Chama na sio nje

Kurusha tuhuma za Chama chako kwenye hadhira ya Taifa ni sawa na kutangaza madhaifu ya mkeo au mmeo mbele za watu badala ya kuyajadili chumbani

Idadi kubwa ya Watanzania hawatumii Muheshimiwa badala yake wanatumia Tundu Lissu kwasababu ya kukosa heshima kwa watangulizi wake

Huwezi kuheshimiwa na watu kama huheshimu wenzako

Safari ya Lissu kufanikiwa kisiasa haipo, sana sana anapoteza muda na swala la uraisi aachane nalo kwasababu hakuna mtu atakayempa nchi mtu asiye na heshima wala adabu
Nasemaje swala la uraisi aachane nalo kabisa na sahau kabisa hakuna mafanikio yeyote afadhali akalime

Kufanikiwa kwake kuwa Mwenyekiti haina tofauti na dhuluma au kutoa kafara
Kapata uenyekiti kwa kuchafua watu ni sawa na kuwatoa kafara na wala mafanikio hayo hayana baraka yeyote kwake ni sawa na mwizi aliyefanikiwa kwa kuumiza wenzake
Hata mwehu hawezi kukuelewa kusema Lissu atakuja kuwa Rais. Ni binadamu mlalamishi kila jambo wakati mpk umri huo hakuna lolote alilolifanyia nchi. Mtu wa kutukana, kuzusha, kutuhumu, kulalamika, kusema uwongo kwake jambo la kawaida, ni kwasababu Chadema ni nyumbu hastahili kuwa m/kiti asilani. Ana tabia za kitoto
 
Back
Top Bottom