Ni vigumu sana Tundu Lissu kufanikiwa kisiasa kwasababu ni mtu wa tuhuma na wala hathamini michango ya wanasiasa wenzake ndani na nje ya Chama
Tundu Lissu ni mtu complicated sana na ni vigumu kufanya nae kazi na hawezi kufanikiwa kisiasa hata umfanyie jema gani hawezi kukuthamini. Pamoja na mapungufu ya kituhuma aliyomrushia Mh Mbowe bado anaonekana hathamini mema yote Mh Mbowe aliyofanyia CHADEMA
Tuhuma za Lissu kwa Mh Mbowe ni kana kwamba Mh Mbowe hakuna hata jema moja alilowahi kufanya
Haiishii hapo tu anaenda mbali hata kuituhumu Serikali na raisi pamoja na jitihada zake inazofanya bado haoni jema hata moja linalofanywa na CCM
Amekuwa mtu wa kutuhumu CCM, CHADEMA na hata Mwenyekiti aliyepita Mh Mbowe kana kwamba hakuna mwema hata mmoja yeye peke yake ndiye mwema inawezekana hata mke wake anapokea tuhuma kila mara
Kwa Mwanasiasa mwenye utu, heshima, adabu hawezi kwenda hewani kutuhumu na kumchafua Mwenyekiti wake na Chama chake hadharani kama alivyofanya bali hayo angeyafanya kwa siri ndani ya mikutano ya Chama chake yaishie humo ndani ya Chama na sio nje
Kurusha tuhuma za Chama chako kwenye hadhira ya Taifa ni sawa na kutangaza madhaifu ya mkeo au mmeo mbele za watu badala ya kuyajadili chumbani
Idadi kubwa ya Watanzania hawatumii Muheshimiwa badala yake wanatumia Tundu Lissu kwasababu ya kukosa heshima kwa watangulizi wake
Huwezi kuheshimiwa na watu kama huheshimu wenzako
Safari ya Lissu kufanikiwa kisiasa haipo, sana sana anapoteza muda na swala la uraisi aachane nalo kwasababu hakuna mtu atakayempa nchi mtu asiye na heshima wala adabu
Nasemaje swala la uraisi aachane nalo kabisa na sahau kabisa hakuna mafanikio yeyote afadhali akalime
Kufanikiwa kwake kuwa Mwenyekiti haina tofauti na dhuluma au kutoa kafara
Kapata uenyekiti kwa kuchafua watu ni sawa na kuwatoa kafara na wala mafanikio hayo hayana baraka yeyote kwake ni sawa na mwizi aliyefanikiwa kwa kuumiza wenzake