NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Nimechoka na majibu ya mkato kwamba mambo ya Mungu tumwachie Mungu mwenyewe, hili jibu haliwezi kamwe kutosha kwa maisha magumu wanayopitia walemavu, Ufafanuzi unahitajika !!
Wanasema kila kitu ni utukufu wa Mungu, watu wote wanaozaliwa wameumbwa kwa baraka yake, Kwa walemavu je ni baraka kwa magumu wanayoyapitia kiasi cha kuifanya dunia kuwa jehanamu kwao?
Nayaongea haya kwa uhalisia na wala si kiburi cha uzima, watu hawa wanateseka sana hapa duniani, Wenye hali hizi waliofanikiwa kiuchumi wapo ila ni wa kuhesabika na jihudi walizotumia laiti wangekuwa wazima basi wangefanikiwa mara 10 zaidi.
Mtu anazaliwa haoni, yani hata kusoma Biblia / Koran hawezi
Mtu anazaliwa hasikii, hata kwenda kanisani / Msikitini haambulii kitu
Mtua nazaliwa na ulemavu wa akili, ni changamoto
Mtu anazaliwa haoni wala hasikii, hapa hawezi kujifunza chochote maana njia zote za kupokea ujumbe zimezibwa
Mtu kazaliwa na magonjwa yenye maumivu makali / maisha yake ni maumivu tu