Ni vipi Mungu anahusika kuwaleta duniani watu wanaozaliwa na ulemavu unaofanya maisha yao kuwa Jehanamu, Ni baraka yake kuwa hivyo ?

Kwani unafikiri alishindwa kutuwekea akili au kutukontrol tukawa ni watakatifu Tu .
Hapana
Mungu ametuacha hivi tulivyo ili Sisi wenyewe Kwa akili zetu timamu tutambue ukuu wake na kumuabudu.
Ukielewa KAZI ya shetani utajua ni kwanini unauliza maswali hayo.
 
Alishindwaje kuumba hizo species zenye kumtii yeye tu na zenye kufanya mema tu,

Badala yake Kaumba species zenye kufanya mema na maovu kwa wakati mmoja na yeye hutaka mema tu?????

Anaweza yote kweli huyo Mungu???
Free will, ukiamua kufanya kizuri unafanya na ukiamua kufanya kibaya huzuiwi.

Ila bado tunarudi pale pale kuhusu suala la walemavu ni mzozo
 
Kuna watu dunia hii wanakuwa kukufuru.
Na hayo yote unayoyadai unajua anaekupa pumzi ya kuendelea kukufuru ni Nani.
Ukilijua Hilo basi mrejee Mungu wako na umtake msamaha maana yeye ni mwingi wa kusamehe.
 
Kila jambo kwa utukufu wa Mungu pamoja na sababu zake husika.Na pia sio ulemavu tu hata kupata au kukosa baadhi ya vitu/ watu tunavyovipenda katika maisha ni kwa sababu ya Mungu alishatangulia mbele na kuona.Kuna kisa kimoja cha Padri aliyekuwa na nguvu ya uponyaji, kuna bubu alimfuata akimuomba amponye ila alimwambia uliumbwa hivyo kwa mapenzi ya Mungu na ungalipewa uwezo wa kuongea ungetumia kuwadhuru wengine hivyo ni vyema kubaki kama ulivyo.Aliponya wengine ila yule bubu hakumponya.
 
Kwamba ilikuwa ni lazima kazi zake zidhihirike kupitia hao walemavu? Yaani walemavu na wale wote wenye madhila kama hayo ndiyo watolewe kafara/wabebe gharama za kudhihirisha hizo kazi kwa watu wengine?
dunia bado haijaeleweka hii,, Anyway bigup kwa akili kubwa🙏🙏🙏
 
Kwamba ilikuwa ni lazima kazi zake zidhihirike kupitia hao walemavu? Yaani walemavu na wale wote wenye madhila kama hayo ndiyo watolewe kafara/wabebe gharama za kudhihirisha hizo kazi kwa watu wengine?
Nani kakwambia wametolewa kafara?
 
Yaani dhambi ya mtu mmoja iwadhuru wasio na hatia?
 
Tuache tabia ya kumpakazia Mungu "eti ni mapenzi yake" tutafute chanzo chake!! Mf. Mtu anakuwa taahira ! Hapo hakuna kamchezo ka binadamu? What is the source of evil in the universe?
 
Wapo lakini ni wachache sanaaaaa!!!

Na bidii waliyotumia laiti wangekuwa ni wazima basi ingekuwa ni mara kumi.

Ni kama vile Mo au Bakhresa wangekuwa na ulemavu wangeweza kufanikiwa ila sio katika level walizofikia wakiwa wazima
Kama ndo hivyo basi wasio kuwa na ulemavu wowote wote wangekuwa matajiri.
 
Kuna watu dunia hii wanakuwa kukufuru.
Na hayo yote unayoyadai unajua anaekupa pumzi ya kuendelea kukufuru ni Nani.
Ukilijua Hilo basi mrejee Mungu wako na umtake msamaha maana yeye ni mwingi wa kusamehe.
Chanzo Cha yote ni mungu shetan majini vimbwenga nk chanzo ni mungu
 
Ahsanteeee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…