Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Msiwe mnapenda kujifungia kimawazo.
Swali dogo, ni nchi gani kwa sasa kuna bei nafuu ya bidhaa zozote zile, pamoja na bidhaa za chakula?
Mimi ningependa CCM wapumzike kwenye uongozi wa nchi, lakini siyo kwa hoja nyepesi kama hii.
Ukweli ni kwamba bei ya chakula itapungua pale ambapo kutakuwa na uzalishaji mkubwa. Kwa upande mwingine kuna faida kubwa sana kama bei ya nafaka itaendelea kuwa juu huko nje ya nchi, kwa sababu hiyo italiongezea Taifa mapato ya fedha za kigeni na kuboresha hali za wakulima. Mauzo ya mazao nje ya nchi yakiwa makubwa sana, pato la Taifa litaongezeka sana, na hiyo itaipa uwezo Serikali kuwapa malipo bora zaidi waajiriwa wake.
Shida kubwa kwa sasa siyo bei ya chakula kuwa juu sana BALI ni uwezo mdogo wa wananchi kuzimudu bei hizo kutokana na vipato duni.
Mimi nina kampuni, natoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi, kwa kweli ninajua pinch ya bei kubwa ya chakula kwa sasa. Hata hivyo, nafahamu kuwa hakuna jibu la mkato. Kama Serikali ya Rais Samia itawekeza sana kwenye kilimo kama walivyoahidi, hiyo ni sahihi sana. Kupanda kwa bei za nafaka tusione kama janga, tutumie hali hii kama fursa kwa nchi yetu yenye ardhi kubwa nzuri ya kilimo, na wananchi wengi wanaolalamikia ukosefu wa ajira. Wengi hawataki kulima kwa sababu kilimo hakina tija. Kupanda kwa bei kutaongeza tija kwenye kilimo.
Hali hii tukiitumia vizuri, tuna nafasi nzuri sana ya kulitambulisha Taifa letu kwenye ngazi ya kimataifa. Tulifanye Taifa letu kuwa mzalushaji mkuu wa nafaka Afrika, kama ilivyo Ukraine kwa Ulaya. Tusijifungie maofisi na kuendelra kulalamikia bei za nafaka, tutoke tukaitumie hii fursa nzuri.
Tukubali kumeza dawa chungu ili tupone maradhi sugu ya umaskini kwa wananchi walio wengi.