Ni virungu vya Polisi ndio vitampeleka Ikulu, kwa kura haendi ng'o!

Msiwe mnapenda kujifungia kimawazo.

Swali dogo, ni nchi gani kwa sasa kuna bei nafuu ya bidhaa zozote zile, pamoja na bidhaa za chakula?

Mimi ningependa CCM wapumzike kwenye uongozi wa nchi, lakini siyo kwa hoja nyepesi kama hii.

Ukweli ni kwamba bei ya chakula itapungua pale ambapo kutakuwa na uzalishaji mkubwa. Kwa upande mwingine kuna faida kubwa sana kama bei ya nafaka itaendelea kuwa juu huko nje ya nchi, kwa sababu hiyo italiongezea Taifa mapato ya fedha za kigeni na kuboresha hali za wakulima. Mauzo ya mazao nje ya nchi yakiwa makubwa sana, pato la Taifa litaongezeka sana, na hiyo itaipa uwezo Serikali kuwapa malipo bora zaidi waajiriwa wake.

Shida kubwa kwa sasa siyo bei ya chakula kuwa juu sana BALI ni uwezo mdogo wa wananchi kuzimudu bei hizo kutokana na vipato duni.

Mimi nina kampuni, natoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi, kwa kweli ninajua pinch ya bei kubwa ya chakula kwa sasa. Hata hivyo, nafahamu kuwa hakuna jibu la mkato. Kama Serikali ya Rais Samia itawekeza sana kwenye kilimo kama walivyoahidi, hiyo ni sahihi sana. Kupanda kwa bei za nafaka tusione kama janga, tutumie hali hii kama fursa kwa nchi yetu yenye ardhi kubwa nzuri ya kilimo, na wananchi wengi wanaolalamikia ukosefu wa ajira. Wengi hawataki kulima kwa sababu kilimo hakina tija. Kupanda kwa bei kutaongeza tija kwenye kilimo.

Hali hii tukiitumia vizuri, tuna nafasi nzuri sana ya kulitambulisha Taifa letu kwenye ngazi ya kimataifa. Tulifanye Taifa letu kuwa mzalushaji mkuu wa nafaka Afrika, kama ilivyo Ukraine kwa Ulaya. Tusijifungie maofisi na kuendelra kulalamikia bei za nafaka, tutoke tukaitumie hii fursa nzuri.

Tukubali kumeza dawa chungu ili tupone maradhi sugu ya umaskini kwa wananchi walio wengi.
 
kama wanaomshauri huwa wanapitapita huku inabidi wachukue hii

 ila huwa sina imani na ccm kabisa,hua ninaona kabisa wanachukua hatua za makusudi kunufaisha wachache (wafanyabiashara) na kuwaacha walio wengi wakitaabika kwa masilahi yao binafsi,,

rejea hata bei ya bando,watu kila siku tunalalamika humu lakini tunajibiwa kwa kashfa tu,ametokea mtu anataka kuleta unafuu (Elon mask) lakini chenga zimekua nyingi,hiyo yote waendelee kunufaika wachache tu wakiwemo hao mafisadi wanaomzunguka,,

Rais inatakiwa awe na maamuzi ya kuwanufaisha wananchi wake tofauti na hapo tunaona hapendi kuona wananchi wakipata nafuu hata kidogo
 
Haleluya
Wala siyo dhambi kabisa kudeclare kuwa utampa kura.

Na mimi hata kama namuombea lakini kwenye sanduku la kura hatopata kura yangu kwa sababu nyingi nilizozitoa kupitia posts zangu mbalimbali.
Tatizo wanaharakati uchwara wengi hawajui wanataka nini akija JPM wanamiss JK akija SSH wanamiss JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wivu wa malalamiko ya mtaani ambayo hayajaanza leo wala jana. Vitu kupanda bei ndio maisha ya ushindani na madhara yake hata angekuwa JPM vitu vingepanda bei tu. Ni masuala ya demand and supply.

Hivyo hizi ni hasira zenye kufanana na maji ya moto daima hayachomi nyumba.
 
Mama hana kisima cha mafuta
Dunia nzima mfumuko wa bei...
Mim nitampa kura asubuhiii sana
 
Huwezi kuita hoja ya kupanda gharama za maisha ni nyepesi, labda uwe mlamba asali tu.

Haya mambo hayaji ghafla kama mvua isiyo na mawingu, ni matokeo ya kauli na matendo ya kiongozi husika wa nchi, asiyejua kupima madhara ya kauli zake.

Gharama zinapanda kwasababu Rais alishawaruhusu wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa zao, kwa kuwapa kisingizio cha vita ya Urusi vs Ukraine, hivi huyu ni Rais wa watanzania au wafanyabiashara? na unaachaje kumlaumu?

Umezungumzia mipango ya muda mrefu, tuuze nje ili tupate fedha za kulipa wafanyakazi mishahara, kama vile nchi hii, kila raia ni mfanyakazi wa serikali! mbona husemi wakati huu wanafanya nini ili kupunguza gharama ya ukali wa maisha?

Hizo nchi unazotaja za nje tunaona serikali zao zikijiongeza kukabiliana na hali hiyo, wengine wanatoa ruzuku, hebu tuambie, hapa kwetu wana mpango gani zaidi ya kusema watatoa chakula toka kwenye maghala ili kushushe bei ya nafaka, ambapo mpaka leo bado kimya?

Mleta mada amekuja na mfano halisi, wa jinsi bei ya bidhaa kupanda inavyoathiri mtu mmoja mmoja, na familia kwa ujumla, mpaka wengine wanachanganyikiwa tena wale tegemeo, ajabu wewe unaita hili suala jepesi?!

Come on..!!
 
KAKA CCM NI MBELE KWA MBELE WAMEVIMBIWA
 
Tatizo ni mradi wa gesi..mafisadi yana mgao wao ndiyo maana hata bwawa la umeme lilipigwa vita sana....hivyo wata jitahidi kukwamisha bei ya umeme isishuke ibaki juu daima ..rostam azizi ni mtu hatari sana hapa tz
 
Asante kuwakumbusha mkuu
 
Asipoenda ikulu 2025 nani mwingine atakwenda? Mwigulu? Lissu? Heche? Zitto?

Wapinzani tulionao muda walionao hautoshi labda mpaka 2030 maana kwa sasa hata ajenda ya maana hawana wanaruka ruka tu. Nilifikiri mikutano ya siasa ikiruhusiwa watawasha moto kweli kweli kwa hoja kali kuuamsha umma. Ajabu nao wamegeuka waimba mapambio...na kupigwa marisasi....

Kwa katiba hii iliyopo na tume hii ya uchaguzi mama wala asiwe na wasiwasi. Ushindi 2025 ni 100% guaranteed; na pengine ndo maana hana wasiwasi....
 
Alokwambia kwamba angekuwepo JPM halafu mambo yakaenda hovyo kama sasa wananchi wangemuelewa ni nani?

Ugumu wa maisha na uhovyo wa viongozi kwa kushindwa kutatua kero zao haitegemei nani yuko madarakani wananchi kumkataa!

Mkuu, fikiri kwa kina!

Ugumu na ukali wa maisha, ni rafiki kwa mtu nani?
 
Kwanini asiende ikulu kwa kura za kishindo, tuwachague hao wametufanyia nn ss wananchi, hata ofs hawana wataweza kujenga madarasa nchi nzima hawa, ss tunaangalia background yamaendeleo ambayo chama au mgombea ametuletea mpaka Sasa Dr SSH Ndye mgombea sahihi
 
HAPA TU PANAKUFANYA UONEKANE WEWE NI MZUSHI USIYE NA AKILI
Ungelionyesha sasa uzushi wangu na ukoswaji wa akili,

Kwa ulivyoandika bila kuja na hoja ya kunionyesha ukosaji akili yangu, bado nakuita mpumbavu
 
samia hadi achoke yeye kuongoza
 
Labda wewe ndio umekua na kuelewa kinachoendelea duniani.

Miaka ya Nyerere kinamama walivaa vitenge vya kupika, tulikula ugali wa yanga.

Maisha huwa na matumaini kwamba kesho itakuwa nzuri kuliko leo, hata wanasiasa wanachoongea kwenye kampeni ni sehemu ya hayo matumaini.

Tunapolia muda huu kuna watanzania wenzetu wanaotajirika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…