Ni virungu vya Polisi ndio vitampeleka Ikulu, kwa kura haendi ng'o!

Msiopenda Samia kuwa rais wote vavayo!
Sasa kati ya wewe na mlete mada nani ambae hapendi bi mkubwa kuwa rais? Mtoa mada anasema mapungufu ili yarekebishwa maana yake automatically uongozi wa Samia utakubalika na ataendelea kuwa Rais lakini wewe unakuja na vijembe that means unakubaliana na hali jinsi ilivyo bei kubwa za chakula na ugumu wa maisha kwako ni sawa vitu ambavyo automatically vinampunguzia Samia uhalali wa kukubalika kiasi kwamba hata ukifika uchaguzi itabidi atumie nguvu kulazimisha kubaki madarakani. Embu jifikirie vizuri kati ya wewe na mtoa mada nani ambae apendi Samia awe Rais
 
Naheshimu mawazo yako, na mengine uliyoyatamka, nakubaliana nawe. LAKINI kuniambia kuwa labda mimi ni mmoja wa walamba asali, hukunitendea haki. Ni kunitusi.

Sijawahi kulamba asali wala hata sijui inalambwa vipi. Katika maisha yangu yote sijawahi kuwa mwajiriwa wa Serikali wala taasisi yoyote ya Serikali. Hiyo asali nitailamba wapi na kwa namna gani? Kama kuna asali, ambayo ningeweza kuisubiria kwa hamu, ni sera nzuri za uchumi. Nimefanya kazi nje kwa muda mrefu, na sasa naona ni wakati wa kuwekeza, hata kwa kiasi kidogo, nchini mwangu. Tujadiliane kwa hoja bila kutwezana.

Jambo moja ninalokubaliana nawe ni kuwa maisha ya wafanyabiashara wengi wa Tanzania ni ya kuviziana. Hakuna ethics za biashara. Ndiyo maana unaweza kumwona machinga amebeba shati, unamwuliza bei gani, anakutazama kwanza wewe unayemwuliza upoje. Wewe utaambiwa sh 30,000. Utanunua kwa sh 30,000, mwingine shati hilo hilo atanunua kwa shilingi 10,000!

Kauli ya Rais kuwa vitu vimepanda Duniani kote kwa sababu ya vita, na hapa kwetu vimepanda bei, ma vitaendelea kupanda, kwa kuzingatia jamii ya wafanyabiashara wa hapa kwetu, haikuwa kauli nzuri maana ilikuwa ni kama kuwaambia kuwa wapandishe bei.

Nadhani ni wakati sahihi sasa kuweka sheria ya Business ethics. Kwa mfano, sheria itamke kuwa mfanyabiashara yeyote anayetumia mazingira ya uhaba wa bidhaa yoyote kujipatia faida halisi (net profit) zaidi ya 50%, atakuwa amekiuka sheria ya maadili ya biashara. Na anayekiuka sheria ya maadili ya biashara aadhibiwe, na kisha kupewa muda wa matazamio.

Lakini pale ambapo ongezeko la bei ya bidhaa yoyote ile ni halisia, hatuna namna nyingine zaidi ya kukabiliana na hali hiyo, au kama bidhaa hiyo ni kiwezeshi cha uzalishaji au kiwezeshi cha uchumi, Serikali iweke ruzuku. Lakini kama hakuna ruzuku, na gharama za uzalishaji zipo juu, mzalishaji ili kulipia gharama za uzalishaji atalazimika kuuza kwa bei kubwa, hakuna namna.
 
Asante mkuu kumjelimisha huyo kilaza
 
Kwako kuita suala la mfumuko wa bei ni jepesi, uliwakosea watanzania wengi wanaohangaika kuokoteza kidogo wanachopata kwa ajili yao, na familia zao, umekuwa kama mtu aliyeshiba, asiyemjua mwenye njaa.

Nimepata imani na hilo baada ya kuona umezungumzia wafanyakazi kwenye kampuni yako, na namna unavyowapa chakula, automatically nikajua inawezekana wewe na kampuni yako mlipitia kipindi kigumu, hasa awamu iliyopita.

Ndio maana sasa umeamua kumtetea anayechangia kuongeza maumivu kwa watanzania kiuchumi, kwasababu inawezekana kwako amechangia kuifufua kampuni yako kwa namna moja au nyingine, ndio maana nikakuita mlamba asali.

Nikaamini hili ndilo likakufanya uandike mawazo yako yaliyojaa ubinafsi, kujaribu kutetea jambo linalowaumiza wengi, kwa kuliita jepesi, binafsi sijaona wepesi wa hilo jambo, zaidi ya hoja zako ulizotumia, kama mishahara kulipa wafanyakazi wa serikalini, wakati tunajua, sekta binafsi ndio imeajiri wengi zaidi, sasa hao wafanyakazi wa serikalini uliowataja, watasaidia vipi kupunguza tatizo la mfumuko wa bei kwa uchache wao?

Ulichoandika mwanzo ulikosea, hasa matumizi yako ya maneno " .... ni jambo jepesi".
 
Malaika amekuta inabidi mkubali huo ukweli. Hali mbaya ameisababisha yeye malaika muovu maana aliachiwa nchi yenye asali na maziwa, ila yeye akaanzisha crackdowns za kiburundi hadi uchumi ukavurugika. Thanks mama Samia amekuja kurudisha matumaini ya uchumi wa muovu yule. Najua umefura lakini ndo ushasoma hivyo.
 
Sio kuwa anawakumbatia, wamemteka. Sio kwamba yeye ni mjinga kuona ila atafanyaje? Hao failures ndio wamemuweka hapo alipo. Ndio wahusika wakuu wa mapinduzi ya kumtoa JPM madarakani. Ila tunawaangalia tu
 
Hamia Burundi,sasa Washauri wa Mama ni akina JK[emoji1787][emoji1787].Yeye mwenyewe nchi ilimshinda kuongoza leo kageuka mshauri.
Mimi nikisikia mtanzania anakimbilia nje ya nchi huwa namuona ana akili sana kwasababu peace of mind ni jambo jema!
 
Kwa kweli TISS na JWTZ wanatuangusha sana kama taifa.Wao ndiyo Walinzi wa Katiba ya nchi,kwani Mkuu wa Majeshi akisoma katiba kwa msaada wa Wanasheria wa jeshi,kuna kifungu kinasema Watanzania waishi maisha magumu ilihali kikundi cha watu wachache kinatafuna nchi!!!
Hii Msoga Kingdom lazima iangushwe vinginevyo hii nchi itakuja kulipuka na kila mtu atabaki mdomo wazi!
 

Umekosema kuja kwenye upande wa siasa ungeenda kwenye upande wa vijimambo na sanaa!
 
Rushwa imetamalaki ofisi za serikali, nenda ofisi ya ardhi uone maajabu, pccb nao sijui sikuizi wanafanya kazi gani naona kama na wao wapo ili wapokee rushwa, mambo si mazuri kusemakweli.
 
Inatisha, miaka mingi tulizoea Petrol ikiuzwa bei juu kuliko Diesel. Wameamua kupindua mambo. Leo nimenunua diesel elfu 20, lit 6.7
Ni mambo ya ajabu sana

Sielewi ni kivipi mtu aliyekulia maisha yasiyo ya shida huwa hajui kabisa maisha ya walala hoi
 
Rushwa imetamalaki ofisi za serikali, nenda ofisi ya ardhi uone maajabu, pccb nao sijui sikuizi wanafanya kazi gani naona kama na wao wapo ili wapokee rushwa, mambo si mazuri kusemakweli.
Hili kwa sasa kama huna noti! Unafiwa na mgonjwa wako mkononi
 
Mkuu kuna bwana mdogo mmoja anaitwa Lucas Mwashambwa, yeye haamini kabisa katika ukweli kama huu, yeye husifia tu pasipo kujiongeza na kutaka kujua uhalisia wa mambo yanayoendelea.
 
Acha uvivu tafta Hera acha kulia Lia andaa mipango upige Hera

Mkulima gani asiye penda mzao yapande unajua kulima wewe?

Kwalipi umchukie Samia?

Cheki Saizi kawapa Uhuru Uhuru huohuo mnautumia kumsimanga,kumdharau,

Ange kuwa munguwenu Saizi unge kuwa wanted huoni UKO huru saizi?

Kuhusu mifumuko.ya Bei sjui uta mdanganya Nani nenda Kenya nenda USA nenda Mexico mpaka Kulee aliko toka risu

dunia mzima imekumbwa na hii Hari
Ya mifumuko ya bei
kwanini hamtaki kuku baliana na ukweli?
Je unanataka kuniambia KIPINDI Cha jpm nasasa

nilini Hali ilikuwa ngumu?
Nilini mkulima Ana nafuu? Nikipindi gani ndoa zilivunjika?
Lini watu walijinyonga?
walijimwagia petrol nakujipiga Moto?
Lini watu wali uwawa zaidi?
lini watu walikimbia inchi? Mnadhani tumesahau?

Niambie pia niutawala gani baada ya kuanguka watu walikunywa bia barabarani kwa furaha,watu walichoma mbuzi na kwanini?

Mnataka afanye Nini mama wa watu?

Hivi kwa mwenendo huu wa kiuongozi Samia atakosaje kura?
Kama leo Ccm na chadema wanakaa mezani kuijenga inchi anakosaje kura?

Samia kafungua fursa nyingi niwewe tu

ukiona ualimu sio fanya biashara,ukiona biashara sio kavue,ukiona kuvua sio kalime,ukiona dar pagumu nenda Moro,Moro pagumu nenda iringa,ilinga pagumu nenda mbeya,mwanza nk

unaweza kaa sehemu kumbe sipo mahali pako kimaisha mwisho ukabaki kuililia serikali

Mkuu KIPINDI hiki mpaka kuli anaingiza laki mbili kwasiku, mkulima anatembelea gari,mpiga debe hakosi 50000/=
Nabado useme Manisha magum kweli?

Nikukumbushe tu kwasasa Ccm na chadema wote ni watanzania na wote niwa samia haujasoma upepo bado?πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu kuna bwana mdogo mmoja anaitwa Lucas Mwashambwa, yeye haamini kabisa katika ukweli kama huu, yeye husifia tu pasipo kujiongeza na kutaka kujua uhalisia wa mambo yanayoendelea.
Huyo si ndo wale vijana chawa waa!

Ole aseme ukweli, hana ajira!
 
Ccm , ki ukweli kabisa tumewachoka mpaka tunaumwa! Si kwa mnavyotufanya tuishi aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…