Ni vitu Gani huvipendi katika Movie zilizotafsiriwa kwa Kiswahili?

Ni vitu Gani huvipendi katika Movie zilizotafsiriwa kwa Kiswahili?

Kinachonikera hasa ni:
1. Tafsiri za Uongo
2. Picha hupungua ubora (Quality)

Kama itatokea nimelazimika kutazama filamu hizo zilizotafsiriwa basi nitatazama aliyotafsiri Dj Mack. Ana makosa yake ila ana afadhali kulinganisha na Ma-Dj wengine.
Hapo no 2 tutatafuta suluhisho, si unajua tena issue za kiufundi
 
Mimi namkubali Dj mjukuu mwana mbambadu japo anauongo mwingi lakini ananogesha muvi kea stori na maneno yako na amefanya niacha hata kuangalia za Subtitle coz hakuna madoido.
Oya mjukuu MTU hatari wewe,hasa movie zile za Korea za porini

Sisi tuliokulia uswahilini bila movie iliyotafsiriwa na DJ aisee hujaniweka kuangalia movie,ni mazoea tuliokuwa nayo

Watoto wa kishua hawawezi kuelewa utamu wake
 
Jamaa kwenye Korea pori hakuna anayemuweza ana kipaji cha kunogesha na kutunga maneno na misemo kuntu wakati mwingine hata mafunzo ya kimaisha.

Mimi kuna muvi nimeziona YouTube kwa subtitle lakini nikiona katafsiri Mjukuu narudia kupata ladha ,mastori na vibweka .Sasa naangalia King Gwangaeto aliyotafsiri humo kuna amsha amsha kibao
 
msichoelewa ni kwamba anayetafsiri,anakusimulia kinachoendelea sio kutafsiri kinachoandikwa hapo chini.

akifatsiri kila neno linalopita hapo chini tutasikia mlio kama wa google translater.
 
Kuangalia movie usioelewa lugha yake ni Upunguani, Utatoka na nini sasa kama lugha husika huielewi na unakaza fuvu hutaki zilizotafsiliewa si bora ukacheze game tu.
Kana vichwa vina funza kabisa unaanzaje kuangalia movie ya kifaransa,kikorea nk na hizo lugha huzijui tena zinatittle za kigiriki kabisa si kwamba utasoma.
Ni ulimbukeni na kuforce Ughaibu, Vuta chuma iliyotafsiliwa uangalie movie kwa raha sio kwa imagination kama unafunua albam ya Picha mnato(Photo)
kwani kuna mtihani baada ya kuangalia movie??

kikubwa burudani,kama tunhezitizama kwa kuzielewa anorld angekuwa anafahamika na watu wachache sana.
 
Zilinifurahisha utotoni ila kwa sasa No thank you!

Nilikuja kugundua kuna tofauti kati ya tafsri na simulizi, wanaotafsiri kibongo bongo wengi huwa hawatafsiri bali wanasimulia kutokana na wao walivyoielewa movie baada ya kuiangalia 'several times'. Japo kuna baadhi ya channels wamejiongeza saa hivi.

Kwa sasa napenda movies zenye 'subtitles' hapo ntaangalia iwe ya kihindi, kichina, kikorea, kirussia, ......you name it!

Ila za kusimuliwa sizipingi huku uswahilini kwetu zinabamba sio kipolepole na watu wana''enjoy life and that's all we need''.
 
Umemaliza vizuri sana
 
Nakuunga mkono mia mia huyu mr amejitahidi sana kwenye kutafsiri na kunogesha movies, kama mada inavyo sema kitu kinacho ni kera ni ile movie inaendelea mtafsiri anapigiwa simu na kupokea na kuonge kama dakika nzima, bora hata ange pause kidogo.
Watoto wa juzi nyie hsmkuepo enzi za mkandara
 
Back
Top Bottom