- Thread starter
- #101
duh!umeongea ukweli wenye maumivu ndani yake...majitu yanakimbilia ualimu eti yapate mkopo chuo,sasa sijui watakua wanauza chaki huko mashuleni au vp,mishahara yao yenyewe ni kama posho kwa mtu wa TRA..mamaee,watajibeba huko vijijin waendako.
mmh. maisha hayapo hvyo ndugu yangu, hao unaowataja wamepitia mikononi mwa Walimu. Kama umemuelewa DZUKUDZUKU hili halikupi tabu, ni uchaguzi binafsi na ndo mfumo wa kimaisha ulivyo unaweza kushangaa huyu jamaa alikuwa na uwezo wa kuchukua kozi kubwa lakini amesoma Bsc Education, angekuwa dokta wanao nani atakaowafundisha chem&bios madokta unaowasema watatokea wapi kama si mikononi kwa watu kama DZUKUDZUKU, kama kila aliyesoma sayans awe dokta au famasia baada ya miaka fulani TAIFA litakosa hao maprofessional wakiwemo wa TRA. Hivyo usinidharau kuchagua ualimu, hiyo kazi unayojidai nayo sasa ni uchaguzi wako binafsi lakini ulipitia mikononi mwa mwalimu. Isitoshe mitaani kwetu tunawaona hao engineers na wengine wakichoma mahindi.