Ni vizuri Rais Samia akafuata ushauri wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuhusu Wapinzani

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kutoa ushauri kwa uongozi wa awamu ya 5 kuhusu namna ya kuendesha siasa na wapinzani. Alisema wapinzani waachwe watoe hoja zao tutawajibu kwa hoja, kama ni kuandama waachwe waandamane mwisho watatulia.

Katika uongozi wa Kikwete demokrasia ilionekana kukomaa sana nchini, palikuwepo na uhuru mkubwa wa habari na kuzungumza na nchi ilisifika duniani kwa demokrasia.

Ni vema rais Samia akafuata mtindo wa Kikwete kukabiliana na wapinzani; kuwaacha wafanye mikutano na maandamano bila hofu yoyote na kujibu hoja zao kwa hoja.
 
View: https://x.com/IAMartin_/status/1837226754001293633?t=AkUMLF4SU9iIN5sX0z-7kg&s=09
 
Huyu mama kanishangaza sana jana katoka katoka kutoa maelekezo kwa IGP jinsi ya kuuwa watu wanaotaka majibu juu utekaji unaoendelea nchin
 
Sitaki kuamini maneno yako mkuu. Sidhani Kama tumefika huko
 
Swala la kuhujum haki ya watu kukosoa na kupaza sauti ni ugonjwa wa kurithi toka kwa mkoloni, Nyerere kafanya hivyo, Kikwete pia kafanya hivyo ila tu Magufuli na Samia wamekuja kuvuka mipaka na Kukosa utu kabisa.

Nadhani imefika hatua "Ubaya Ubwela" itasound better kuliko hii ya "We Huogopi"
 
Auaye kwa upanga naye atakufa kwa upanga. Nimekaa palee👉👉👉
 
Back
Top Bottom