Ni wajibu wa msanii kuwasilisha wimbo wake Basata kabla hajautoa au sheria inasemaje?

Ni wajibu wa msanii kuwasilisha wimbo wake Basata kabla hajautoa au sheria inasemaje?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Hili limekuwa linanitatiza sana je utaratibu unasemaje Kuhusu hili? Je msanii anaweza kutunga tu wimbo wake na akaurusha tu bila kuruhusiwa na mamlaka hii? (BASATA) na endapo msanii atafanya hivyo kiholela ni adhabu gani anaweza kukumbana nazo.

IMG_20221105_090422_202.jpg
 
Ukiuacha umbogamboga kidogo utakuwa kijana mzuri sana
Lengo lako ni kuuponda wimbo mpya wa Nay wa mitego ila message sent.
 
Je msanii anaweza kutunga tu wimbo wake na akaurusha tu bila kuruhusiwa na mamlaka hii? (BASATA)

mpaka uwe mwana-chama wa BASATA, na vile Ney alijivua uanachama mwaka jana, nafikiri

so anafanya mziki 'mtaani'
 
BASATA haijawahi kutusaidia Wasanii zaidi kutudidimiza
 
mpaka uwe mwana-chama wa BASATA, na vile Ney alijivua uanachama mwaka jana, nafikiri

so anafaya mziki 'mtaani'
Lakini basata wanapaswa kuwa ndio chujio la nyimbo zote nchini tanzania, kusema mtu ataimbia mitaani kunaondoa umaana wa chombo hicho kuwepo.
 
Lakini basata wanapaswa kuwa ndio chujio la nyimbo zote nchini tanzania, kusema mtu ataimbia mitaani kunaondoa umaana wa chombo hicho kuwepo.
uko sahihi ila , labda ichi ndicho kinachowafunga

"....kufuatia sheria yao mpya ya kuzipitia nyimbo za wasanii kabla ya kuzipeleka kwenye vituo vya REDIO na TV"

Ney anaachia kupitia digital platforms siyo huko redioni na kwenye Tv
 
Hili limekuwa linanitatiza sana je utaratibu unasemaje Kuhusu hili? Je msanii anaweza kutunga tu wimbo wake na akaurusha tu bila kuruhusiwa na mamlaka hii? (BASATA) na endapo msanii atafanya hivyo kiholela ni adhabu gani anaweza kukumbana nazo.
View attachment 2407230
Kama wanachama wa basata na anatambuliwa na basata.

anaweza kulipishwa faini

kuvuliwa uwanachama

au kupewa kifungo cha sanaa kwa mda inategemea na kosa

lakini pia kama sio wanachama wa basata maana yake kwenye shughuli kubwa za kitaifa kama show haruhusiwi kuperfome maana hatambuliki kama msanii
 
Kwani basata nini?.
Tanzania bhana. Basata baada ya kuona muziki unalipa au sanaa kwa ujumla wakaanza kuleta sheria za kipuuzi. Basata wahakik mmh bongo bado tunajitafita
 
Back
Top Bottom