Uchaguzi 2020 Ni wakati gani JWTZ inapaswa kuingia mtaani kushiriki shughuli za kisiasa na kutuliza ghasia?

Uchaguzi 2020 Ni wakati gani JWTZ inapaswa kuingia mtaani kushiriki shughuli za kisiasa na kutuliza ghasia?

Natamani wanajeshi wetu wawe kama wa Malawi. Kazi yao ni kulinda wananchi dhidi uonevu wowote.

Kuna siku itafika. Iwe kesho au ............

Mtu muonevu atapigwa ngeu ya Gafafi
Wameapa kuilinda nchi na sio kumlinda mtawala, uoga wetu ndio unawaangusha
 
Ni suala la upeo tuu kuelewa maana ya ulinzi wa nchi; upeo ukiwa chini utakosa clear dichotomy kati ya nchi, mtawala, mtawala na dola.
Ni kwa tawala za kidikteta na kijamaa tu ambapo kazi ya vyombo vya ulinzi ni kulinda maslai ya mtawala na sio nchi.
Mbona Malawi tu vyombo ulinda nchi na sio chama
 
Jeshi halipangiwi na raia nini cha kufanya, liko kwa kazi moja tu kuhakikisha nchi unakuwa salama muda usiku na mchana 24/7

Wewe endelea na maisha yako kama Jana juzi na Leo na wao waache waendelee na majukumu yao Aisha mipakani makambini au mitaani wewe yahakuhusu
yahakuhusu ndio nini??
 
Zamani tulikua tunafundishwa majukumu ya ulinzi yalivyogawanyika. Kwa kumbukumbu zangu mgawanyo ulikuwa hivi:
1. Usalama walikua na jukumu la kukusanya kuchakata na kushare taarifa kwa jamii na vyombo vingine kuhusu viashiria mbalimbali vya uvunjifu wa amani au fursa ambazo Kama nchi tunapaswa kuziona na kuzipigania. Walihusika kukusanya taarifa kuhusu diplomasia ya kimataifa , uchumi nk na kusambaza taarifa kwenye mamlaka husiku kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Hawa kwa Ulimwengu wa Sasa tunaweza sema ni search engine au Google ya nchi, kila taarifa unaweza ipata.

2. Polisi walikabidhiwa ulinzi wa raia na Mali zao

3. JWTZ walikabidhiwa ulinzi wa mipaka dhidi ya maadui wa nje wanaotaka kulivamia taifa letu.

4. Uhamiaji walipewa udhibiti mipakani kuchuja wa kuingia na kutoka.

5. Magereza ilikua sehemu yakuhifadhi watuhumiwa na wahalifu pamoja na kuwafunza namna yakuachana na uhalifu, kurekebisha tabia.

Lakini baadaye kikaongezeka chombo kingine kinaitwa TAKUKURU kinachofuatilia usalama wa rasilimali Mali zetu,maadili na utoaji huduma pamoja na kudhibiti rushwa na viashiria vyake.

Aidha, vyombo vyote hivi vina uniform ambazo nikisoma kwenye websites na machapisho mbalimbali online zimeainishwa vyema kabisa kwa ajili ya mwananchi kujua na kumtambua vyombo vyetu japo katika mazingira flani ndani ya vyombo wapo Askari kanzu.

Lengo langu kuu ni kuhusiana clip inayosambaa ikielezwa ni ya Zanzibar na hata hapa janvini ipo. Clip ile inaonyesha askari mwenye nguo za JWTZ, Polisi na uniform nyeusi ambazo hazijasajiliwa kwenye chombo chochote kwa mujibu wa uniform za taasisi zetu. Lakini pia uniform uvaliwa na watu nadhifu na kwa unadhifu. Ukiangalia hii clip unabaini hawa wenye uniform nyeusi wamenyoa mnyoo usioendana na vyombo vyetu lakini pia mitutu ya slaha walizoshika imeelekezwa kwa raia kinyume kabisa na ukubwa na nguvu ya raia waliolengwa. Sasa basi, naomba tuelimishane kwa lengo lakujifunza

1. Ni wakati gani JWTZ anaingia mtaani kukabiliana na raia?
2. Hizi uniform nyeusi ni za Jeshi gani?
3. Vyombo vyetu vipo tayari kukubaliana na taarifa chafu kwamba hizi ni uniform za Butundi? Kwanini tusilitolee majibu kuvisafisha vyombo vyetu kutoka kwenye maneno ya watu wasiovitakia mema vyombo hivi?
4. Zanzibar ipo vitani?
You have been told several times that your president is a dictator.
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Kwa awamu ii.ni wakati wa kuiba kura JW wakimbizane na vibox vya kupigia kura .hadi FFU walalamike kuingiliwa kazi yao teh teh teh
 
Mtii sheria bila shurti. Linda tunu amani, otherwise utakuwa in trouble.
 
Back
Top Bottom