Ni wakati muafaka kwa serikali kuruhusu magari ya abiria kusafiri usiku

Ni wakati muafaka kwa serikali kuruhusu magari ya abiria kusafiri usiku

Hizo sababu ulizosema tiba yake siyo magari kuruhusiwa kusafiri usiku, safari za usiku ndo zitaongeza hatari zaid, malori tu ukikutana nayo usiku mwendo yanayo tembea ni balaa sasa ukiruhusu na bus si ndo unaenda kuchinja watu wengi zaidi, angalau mchana watu wa mabus Kuna maeneo wanaogopa kukimbia kwa kuhofia tochi, usiku tochi hamna kabisa mwendo utakua mkubwa Zaid.
 
Hizo sababu ulizosema tiba yake siyo magari kuruhusiwa kusafiri usiku, safari za usiku ndo zitaongeza hatari zaid, malori tu ukikutana nayo usiku mwendo yanayo tembea ni balaa sasa ukiruhusu na bus si ndo unaenda kuchinja watu wengi zaidi, angalau mchana watu wa mabus Kuna maeneo wanaogopa kukimbia kwa kuhofia tochi, usiku tochi hamna kabisa mwendo utakua mkubwa Zaid.
Una taarifa kuwa nchi jirani wanatembea muda wowote? Una taarifa kuwa kampuni hizi zinatembea Usiku?
1. Superfeo ya Songea to Mwanza.
2. Fikoshi ya Mbeya/Mwanza/Mbeya.
3. Premier ya Mbeya/Mwanza/Mbeya.
4. Majinja ya Bukoba to Dar.
5. Happy Nation ya Bukoba to Dar.
6. JM ya Musoma to Dar.
7. Najimunisa
8. Osaka. Ngara to Dar
9. Sabuni Ya Mbeya/Mwanza/Mbeya.
10. Takbir ya Kasulu to Dar.
11. Adventure ya Kigoma to Dar.
12. Aifola ya Kigoma to Dar
Etc

Hapo Kuna Ajali ngapi??
Why tunapenda kulala? Matokeo yake tunawaachia wadereva na watu binafsi ambao sio taaluma zao kusafirisha Abiria. Nenda Mbezi usiku uone, nenda Mwenge, nenda Segera, Chalinze, Morogoro, Singida, Dodoma (CBE), Tinde (junction ya Kahama), nenda Makambako, Mbeya. Kote huko na kwingine nenda Jioni utaona utitiri wa Abiria wanaovizia MAGARI.
 
kuna mshenzi mmoja wa basi la GreenStar, tulichomoka Moro saa 4 usiku, kainusa Ubungo Terminal saa 6 kasoro, huko njiani roho mkononi
Hahahaaha tulitembea Makambako to Njombe Kwa dakika 25 Kwa Superfeo ilikua inatoka Mwanza kwenda Songea
 
Wakuu, week mbili hizi nimesafiri kwenda Tanga na Sasa Niko safarini kwenda Nyakanazi.

Kwa Safari zote hizi, nimegundua na kuthibitisha yale ambayo nimewahi kuyasema hapa mara kadhaa.

1. Mabasi yanaondoka kwa sasi sana unnecessarily. Safari yangu ya Tanga nilifanikiwa kurekodi speed ambapo kuna muda ilifika 138km/hr.

2. Ni chanzo kikubwa cha ajali hasa bodaboda wanaowahisha abiria wanaokua wameachwa, rejea ajali kadhaa kati ya Mbezi Hadi Kibaha.

3. Ni chanzo kikubwa cha usumbufu barabarani, leo tumefika Mikese mabasi yametanua na hivyo kuleta usumbufu kila mtu anawahi mizani.

4. Ni chanzo na kichocheo cha Rushwa, leo kama ilivyo siku nyingine, tumesimamishwa pale Mikese Polisi, Askari wamepewa pesa na gari ikaruhusiwa.

Haya yanatokea Dar na mahali pengine nchini.

Tukubali kuwa tulikurupuka kusimamisha au kuzuia magari ya abiria kusafiri Usiku.
akili za madereva wa kitanzania bado sana. Utaskia matukio kila kukicha. Kwa sasa bado.
 
Pana 60km kama nakumbuka vyema, yet speed ilikua KUBWA sana sana kwakua nilikua narekodi
Pole sana mkuu,ila tatizo sio speed, tatizo ni barabara mbovu, kwa 60km kutumia 25min sio speed kali sana, kutoka Windhoek hadi katima mulilo ni almost 1400km,na bus zinatambaa kwa 10 to 12 hrs, kutoka kapiri mposhi hadi nakonde ni kama 800km ,Power Tools inatambaa kwa 10hrs pamoja na kipande cha mpika hadi chinsali kuwa kibovu, tufanyeni kazi kwa smart ili barabara zetu ziwe na kiwango bora, tuache politics na tukubaliane kuwa barabara zetu bado na tuzijenge upya sio kuzipiga vilaka
 
Mkuu unafikiri wakiruhusiwa kusafiri usiku
1.Hawatakwenda mwendo mkali?
2.Ajali hazitakuwepo?
3.Hawatakuwa wasumbufu barabarani?
.4Rushwa hazitakuwepo

Mimi bianfsi nafikiri haya uliyoorodhesha kama yanatokea mchana kweupe usiku yataongezeka.
4.
Hivi basi likitoka Arusha saa 1 jioni linaenda Dar au Morogoro litakimbilia nini? sana sana likimbia litafika Dar saa tisa usiku ambapo abiria wenyewe wanataka likiwahi sana kufika, lifike saa kumi na moja. Kumbuka wanaotembea usiku 75% ni wafanya Biashara hivyo hata wakifika dar saa tisa usiku hakuna jipya kwani mji unakuwa umelala
Mf#2; Gari likitoka Dar saa nne usiku linaenda Dodoma, Litakimbilia nini? wakati Abiria wanataka likiwahi sana lifike Dodoma saa kumi na moja?

Simple logic, magari yanayotembea usiku yaanze Safari mapema hiyo tu ni speed governor tosha; na sio yaanze safari baada ya usiku wa manane, kwani yakichelewa kuondoka, yatakimbia/yatashindana

ukifikiria kwa makini kuna watu takribani 20,000 kila siku wapo kwenye mabasi mchana kutwa badala ya kuzalisha. Mabasi Yangetembea usiku huenda tungegawa nusu yake.
Wangeanza kidogo kidogo maeneo yaliyo salama
na kama hiyo wanaona inachangamoto, mabasi yaanze safari saa kumi ya Alfajiri (4am) ili wafanya biashara na wanaotaka kuwahi wawe wameshatangulia na hapo tutakuwa tumepunguza msongamamo na mashindano barabarani
BINAFSI NAPENDA KUSAFIRI USIKU!
 
Umbali huu ninaweza tambaa kwa 20mins only, tatizo letu barabara zetu ni mbovu, na siku tutakayokubali hili ndio tutaamka usingizini, tuache longo longo tufanye kazi smart, speed sio tatizo kubwa, barabara mbovu ndio tatizo
 
Namshukuru sana Spika Tulia kwa kuibua tena jambo hili.
1. Nashauri mabasi yaruhusiwe kuondoka wakati wowote ufaao badaa ya kulazimishwa kuondoka Dar alfajiri (saa 12).
Kwa mfano.
Mabasi yanayokwenda mikoani yakiruhusiwa kuondoka saa 6 mchana yatafika Kahama alfajiri ambapo yataendelea na safari yake.
2. Kusafiri usiku kutapunguza gharama za wasafiri.
Hivi sasa ili kuwahi stendi ya Magufuli kupanda mabasi ya alfajiri inabidi ama kulala nyumba ya wageni au kutumia usafiri wa gharama kubwa kwa kuwa ni usiku.
Safari zikianza mchana au jioni zitatuondolea adha hii.
3. Muda mwingi unapotea kwa kusubiri.
Kila ukifika usiku mabasi yanaegeshwa.
Kwa kanda ya ziwa ni Kahama.
Abiria wanatumia gharama kwa kulala safarini.
Baadhi ya abiria ni wagonjwa wanaokwenda kwenye matibabu au misiba
Hawa wanacheleweshwa.
Mabasi yakitoka Singida jioni yatafika Dar alfajiri ambapo abiria mfanya biashara ataingia kwenye manunuzi kisha jioni/usiku atapanda basi kurejea alikotoka.
Hakuna.muda wa kupotea.
4. Muda wa matengenezo utakuwapo wa kutosha.
Baadhi ya mabasi ya mikoani kama yaendayo Mbeya na Kahama yanafika usiku na alfajiri yanarudi Dar.
Matengenezo yanakuwa hafifu kwa kuwa gereji nyingi zinakuwa zimefungwa.

Hata hivyo ni LAZIMA jeshi la polisi lijiandae vema kwa ajili ya kuhakikisha usalama.wa.abiria.

Nadhani ni vema LATRA iondokane na utaratibu wa sasa wa kuondoa mabasi vituoni kwa wakati mmoja kama vile ni mashindano ya mbio kwenye riadha.

Nashauri mabasi yaanze safari kwa muda tofauti.

Asante sana Spika Tulia Ackson kwa kuchagiza hili.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom