Ni wakati muafaka sasa Mifugo itozwe kodi. Msukuma au Mmasai anamiliki zaidi ya ng’ombe 1,000 na hachangii chochote! It is not fair

Unafikiri wakitozwa kodi utamudu kununua nyama buchani?. Watu wa mazao ya kilimo na mifugo ni wa kupewa ruzuku si kuwaundia kodi
Mwenye bucha analipa kodi kwanini mfugaji asilipe ?basi kama hawalipi kodi na Bei ya nyama ishushwe
 
Upumba.fu tu umeandika

Maliasili zimejaa mnashindwa kuzi exploit..mnalipana mishahara mikubwa ....unaona kubuni njia za kuendelea mkamua mwananch ndo akili
 
Unataka kutuharibia wafugaji ? Tulikimbia kwenye maduka baada ya kuona kodi zimezidi na kuhamia kwenye kufuga ng'ombe wa kunenepesha kwa ajili ya kuuza! Na huku mnataka kutufuata tena?
Achana na mtoa mada akil ndogo. Hajiuliz y pembejeo za kilimo hazina ushuru.anashindwa jua mifugo ni chakula na ni basic need.ukimkamua mkulima wa mifugo umeua sekta ya kilimo au hajui mazao na mifugo vinategemeana

Anashindwa tumia maliasili kibao zmejaa anataka wabuni kuendelea mkamua mwanach maskin zaid na zaid...kagame anawambia wakimpa bandar tu kama ya dsm anakua tajir...sasa tz kuna madin.bandar.maziwa bahar..ardh ya kutosha..wanyama mbuga.milima..

Unakuja mskia mtu asietumia akil anapendekeza et kod kwa wanyama..kuku ngombe mbuzi..ana akil kwel mtoa mada
 
Unafikiri wakitozwa kodi utamudu kununua nyama buchani?. Watu wa mazao ya kilimo na mifugo ni wa kupewa ruzuku si kuwaundia kodi
Inaonekana wewe unamiliki ng'ombe mkuu. Watozwe kama vipi na wafanyabiashara wapewe ruzuku na wao ama wao sio watoto Wa familia yetu. Mbona Samaki ana bei sana na kuku Wa kienyeji na mvuvi analipa kodi.
Ngoja ipande nyama buchani
 
Ilikuwepo zamani ila akaifuta Mkapa pamoja na zile kodi za vichwa na baiskeli.
 
Unafikiri wakitozwa kodi utamudu kununua nyama buchani?. Watu wa mazao ya kilimo na mifugo ni wa kupewa ruzuku si kuwaundia kodi
Kama tukisema tuzingatia tahadhari uliyoitoa itabidi maeneo mengi tuache kutoza kodi kwa vile hatutamudu gharama za bidhaa husika, hata kwenye kilimo itatakiwa tufute kodi kwani vyakula vinapanda bei...kodi ya sh 2000 kwa kila ng'ombe itafanya kilo ya nyama ifike bei gani? kodi itozwe bila kuangalia hili ndio tutafika
 
Hivi karibuni kumeibuka manung'uniko makubwa ya uonevu kwa wafanyabiashara kuhusu tozo kubwa za kodi.

Mishale na lawama wamekuwa wakitupiwa ndugu zetu wa TRA.

Lakini, ukichunguza kwa umakini utagundua tatizo la msingi haliko kwao.

Tatizo ni ubunifu usiotosheleza wa nchi yetu katika kubainisha vyanzo vya kodi.

Vyanzo vikubwa kama Mifugo, vimeachwa bila sababu.

Kwa hesabu ndogo tuu, mfano Wilaya kama Meatu ina takriban ya ngombe zaidi ya laki nne. Ukitoza kodi angalau 2,000/= kwa kichwa cha ngombe kwa mwaka utapata almost 800 million, bado mbuzi na wanyama wengine.

Hiki chanzo kingeweza kupunguza lengo la makusanyo ya Wilaya yaliyoelekezwa kwa wafanyabiashara tu.

Halikadhalika, Serikali hutumia gharama kubwa kutengeneza miundombinu ya mifugo. Ni kwa nini gharama hizo zisitokane na kodi ya mifugo,badala ya kutumia kodi za wafanyakazi na wafanyabiashara.

Ni maoni yangu kuwa sekta zote za kipato rasmi,zichangie kwa usawa maendeleo ya nchi yetu badala ya kuelekeza nguvu zote kwa kundi dogo.
Nyie jamaa wajinga sana.....
hicho ndio chakula chetu....
hao jamaa ukiwadisturb waache kufuga nyama utakuwa unaisikia kwenye redio
 
Hivi karibuni kumeibuka manung'uniko makubwa ya uonevu kwa wafanyabiashara kuhusu tozo kubwa za kodi.

Mishale na lawama wamekuwa wakitupiwa ndugu zetu wa TRA.

Lakini, ukichunguza kwa umakini utagundua tatizo la msingi haliko kwao.

Tatizo ni ubunifu usiotosheleza wa nchi yetu katika kubainisha vyanzo vya kodi.

Vyanzo vikubwa kama Mifugo, vimeachwa bila sababu.

Kwa hesabu ndogo tuu, mfano Wilaya kama Meatu ina takriban ya ngombe zaidi ya laki nne. Ukitoza kodi angalau 2,000/= kwa kichwa cha ngombe kwa mwaka utapata almost 800 million, bado mbuzi na wanyama wengine.

Hiki chanzo kingeweza kupunguza lengo la makusanyo ya Wilaya yaliyoelekezwa kwa wafanyabiashara tu.

Halikadhalika, Serikali hutumia gharama kubwa kutengeneza miundombinu ya mifugo. Ni kwa nini gharama hizo zisitokane na kodi ya mifugo,badala ya kutumia kodi za wafanyakazi na wafanyabiashara.

Ni maoni yangu kuwa sekta zote za kipato rasmi,zichangie kwa usawa maendeleo ya nchi yetu badala ya kuelekeza nguvu zote kwa kundi dogo.
Mkuu,

Nakuunga mkono kwa asilimia zote hasa mwenye idadi zaidi ya ishirini ni sharti alipe kodi na wawepo wakaguzi wenye mafunzo yanayoheshimu haki za binadamu ili kuzuia uonevu na wachache kujinufaisha binafsi. Sheria itungwe haraka na ianze kufanya kazi mapema mwakani 2022.

Mwenye kondoo na mbuzi zaidi ya 50 nao pia walipe kodi.

Lengo kuu

1. Mapato ya taifa
2. Kutunza na kulinda mazingira yaliyokavu na oevu
3. Kuchochea ufugaji wenye tija kupitia mazao ya maziwa, samli, ngozi na kinyesi chake
4. Kuchochea hamasa kwa wafugaji holela kujali afya na maisha bora ya familia na taifa
 
Watanzania tuanze kufikiria ni jinsi gani kodi zipunguzwe siyo ziongezwe au walipa kodi waongezeke. Serikali ndiyo ijifunge mkanda na ipunguze matumizi na ufujaji ili kodi zinazolipwa tayari zitoshe.
 
Hivi karibuni kumeibuka manung'uniko makubwa ya uonevu kwa wafanyabiashara kuhusu tozo kubwa za kodi.

Mishale na lawama wamekuwa wakitupiwa ndugu zetu wa TRA.

Lakini, ukichunguza kwa umakini utagundua tatizo la msingi haliko kwao.

Tatizo ni ubunifu usiotosheleza wa nchi yetu katika kubainisha vyanzo vya kodi.

Vyanzo vikubwa kama Mifugo, vimeachwa bila sababu.

Kwa hesabu ndogo tuu, mfano Wilaya kama Meatu ina takriban ya ngombe zaidi ya laki nne. Ukitoza kodi angalau 2,000/= kwa kichwa cha ngombe kwa mwaka utapata almost 800 million, bado mbuzi na wanyama wengine.

Hiki chanzo kingeweza kupunguza lengo la makusanyo ya Wilaya yaliyoelekezwa kwa wafanyabiashara tu.

Halikadhalika, Serikali hutumia gharama kubwa kutengeneza miundombinu ya mifugo. Ni kwa nini gharama hizo zisitokane na kodi ya mifugo,badala ya kutumia kodi za wafanyakazi na wafanyabiashara.

Ni maoni yangu kuwa sekta zote za kipato rasmi,zichangie kwa usawa maendeleo ya nchi yetu badala ya kuelekeza nguvu zote kwa kundi dogo.
NI WIVU TUUUUU!!
 
Kodi ya mifugo isiyojuliana inapatikanaje?

Mifugo haina vaccines wala matibabu yoyote.

Serikali ingepata chanzo maridhawa cha kodi kama hawa wanyama kungekuwa na subsides kwenye pembejeo na chanjo za uhakiki. Pia wawe na bima ndio kingekuwa chanzo maridhawa cha ilivyo kwenye kodi na bima za magari.

Usione vyaelea mkuu wamaasai mpaka wanaywesha gongo wanyama wao wanapougua, maana hata dawa ya magonjwa mengine wao hawazijui.

Lazima serikali ikitaka hiki kuwa chanzo cha mapato iwekeze. Imagine katika mipango miji (master plan) huwezi kuona mahali pametengwa kama mahali pa kufuga au malisho ya wanyama.

Sasa hawa wanyama wanakuwa attached na makazi ya binadamu ila serikali haiwatambui hata kwa makazi tu halafu ukiite chanzo cha mapato. Magonjwa, ukame na udhoofu unapowakumba wanaokufa mpaka unaogopa.
JF jamani kwa ubunifu wa kodi tu😀!

Umesema kweli kuwe na uwekezaji, miundo mbinu itakayoleta udhibiti.

Wanyama wanaozurula pori kwa pori!
Mfugaji ni mchungaji na mzurulaji tu na ng'ombe wake.
Hawana makazi, Maswa, leo Rufiji, kesho Kilombero, mtondogoo blonde la Usangu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mkuu hata wamachinga wanaozurura na bidhaa zao huko na kule wanachangia kupitia kipande cha 20,000/=. Nafikiri wanaozurura na mifugo ndo walipe kodi kubwa. Wanaharibu mazingira ambapo gharama za kuyarekebisha ni kodi ya mfanyakazi na mfanyabiashara.
 
NI WIVU TUUUUU!!
Mkuu, mimi ni mfugaji, napenda hii kodi ije,nichangie pato la Taifa nchi iwe na uwezo wa kujenga majosho na malambo kwa kila kitongoji. Ikifanya hivyo, nitapunguza hasara za vifo vya mifugo vinavyosababisha nirudi nyuma kimaendeleo!
 
Inabidi wahaya na wachaga walipie kodi migomba kila mgomba mmoja utozwe dola 50$ .

Najua wachaga na wahaya ni matajiri Sana wakikasirika watalipia mgomba mmoja dola 100$.
 
Kama tukisema tuzingatia tahadhari uliyoitoa itabidi maeneo mengi tuache kutoza kodi kwa vile hatutamudu gharama za bidhaa husika, hata kwenye kilimo itatakiwa tufute kodi kwani vyakula vinapanda bei...kodi ya sh 2000 kwa kila ng'ombe itafanya kilo ya nyama ifike bei gani? kodi itozwe bila kuangalia hili ndio tutafika
Mkuu cement imefikla 25,000/= . Ukipembua vyema, utakuta kodi na tozo zingine inachangia hadi 10,000/=. Ukija kwa ngombe, bei ya dume la ngombe wa kisukuma linauzwa hadi milioni moja.
Wapi kodi ni kubwa kwa uwiano wa bei ya bidhaa?
 
Back
Top Bottom