battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,717
- 2,582
Hii Si kweli, Australia ina majimbo wala hakuna ukabila, South African ina majimbo wala haina ukabila, Canada ina majimbo wala haina ulkabila, namuunga mkono mleta mada (uzi huu). Na nampinga huyu Hamas. Yehodaya.Ulichosahau ni kuwa serikali za majimbo hufanya kazi kwenye nchi ambazo zina ubaguzi wa
1.Kikabila
2.Rangi
Nchi zenye tabia hizo ndizo hutumia utawala wa majimbo.
Mfano ni Marekani ,Afrika ya kusini,Kenya,Nigeria ,INDIA,SUDAN NK.Kumaliza ubaguzi wa rangi na wa kikabila ndio Nchi hugawanywa kwenye majimbo.
Majimbo ni kama nchi kamili kabisa yenye raisi wake ambaye ni GAVANA wa JIMBO.Mtu kutoka jimbo moja kwenda jingine sehem zingine huhitaji kuwa na kitu kama passport na visa ya kuingilia jimbo lingine.
Tanzania haina tatizo la ubaguzi wa rangi wala kabila.
Mfumo wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo kuwa maskini wa kutupwa kama hayana raslimali.Mfano chini ya mfumo wa majimbo mkoa wa Morogoro ungeongoza kwa utajiri sababu umeme wote unatoka kidatu morogoro pesa zote za umeme nchi nzima wangetakiwa wapewe watu wa morogoro.
Bandari ya dar es salaa na uwanja wa ndege wa dar mapato yote yangekuwa ya dar tu hayaendi popote.Mikoa kama singida,dodoma,kigoma nk ingekufa maskini wasingekuwa hata na barabara ya lami.Marekani wanakotumia huo utawala wa majimbo kuna majimbo maskini hadi yanatia huruma.
Utawala wa majimbo ni wa wabaguzi wa kikabila na kirangi.