Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Majimbo Yote ni shida tu.Nenda india angalia jimbo la Kashmir linavyosumbua india.Jimbo lina utajiri mkubwa kutwa linaota kujitenga.Ni headache kwa india.Afrika kusini ni balaa tupu wanafukuzana na kukimbizana kwenye majimbo kama kuku.Huwezi KUISHI KWA RAHA au kugombea jimbo lisilo lako kama wewe si mzawa!!!
Perhaps....lakini ukweli ni kuwa decentralisation inachochea maendeleo. Unaweza ukanitajia ni nchi ngapi zilizo kwenye G8 ambazo hazina mfumo wa majimbo? Au hata hapa Afrika tu. Ukiangalia the top economies zote ziko hivyo!
 
Ni bahati mbaya wanasiasa na vyama hawataki kuelezea sera zao.Wanachokalia ni kulipua mabomu tu ya nani kala nini au kaiba.Sawa yule kala au kaiba lakini wewe sera zako ni zipi zifafanue hawataki.Yaani inauma sana.Hawawatendei haki wananchi kwamba je wachague mtu kwa kuwa kalipua bomu au wamchague kwa sera zake.Wanaweka wapiga kura njia panda kwenye mikanganyiko.Mtu ansema tu sera ya majimbo halafu anatokomea bungeni au mitini bila kufafanua wala nini.

* Nakuunga mkono sana mkuu wanasiasa wetu ni pasua kichwa huwezi kumkuta akielezea sera za chama chake ili wananchi waelewe na kuchambua sera zao, ila wao ukalia kuikosoa CCM kana kwamba bila CCM kufanya makosa hawezi kuwa na maneno. Shida wanasiasa wa nchi hii ni kubwa sana hata viongozi wa vyama hivyo si ajabu akakuta na wao hajui sera za vyama vyao, nawashangaa sera zao uelezea wakati wa uchaguzi tu pengine ni kufutilana Nicolas kafanya nini nimlipue tunaka sera madhubuti ili kusonga mbele.
 
* Nakuunga mkono sana mkuu wanasiasa wetu ni pasua kichwa huwezi kumkuta akielezea sera za chama chake ili wananchi waelewe na kuchambua sera zao, ila wao hukalia kuikosoa CCM kana kwamba bila CCM kufanya makosa hawawezi kuwa na maneno.

umegonga nyundo mkuu
 
Mfomo wa majimbO haufai Afrika sana sana utatuletea mgawanyiko.
 
Kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusiana na utendaji wa serikali katika kufanya maamuzi yake kuelekea kwa wanainchi wanaowaongoza , hali iliyopelekea maamuzi mengi kufanywa mkoani Dar es salaam kana kwamba nchi hii inao mkoa mmoja tu na mingine si mikoa bali ni wilaya, kata , mitaa na tarafa za mkoa wa Dar es salaam .

kufanya hivi kumeinyima mikoa mingine kupiga hatua za maendeleo kwa kutegemea Dar es salaam wanamua nini kuelekea mikoa mingine na mbaya zaidi mikoa hii imekuwa ikusanya mapato kutoka kwenye vyanzo duni walivyo navyo na kupeleka Dar es salaam na Dar ndo wanaamua nani tumpe? nani tumnyime? hali hii imedumaza fikra na utashi wa viongozi kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa weledi katika kuijenga mikoa yao.

serikali za majimbo ni nini?
hizi ni serikali za mikoa zenye mamlaka kamili ya kubuni na kukusanya mapato ya mkoa husika na kutumia kupitia bajeti ya mikoa yao na kutoa huduma kwa jamii ikiwemo huduma za msingi kama elimu , afya , miundombinu , na usalama maeneo yao husika.

viongozi wa serikali za majimbo watakuwa ni akina nani na watapatikanaje ?
viongozi wa serikali za majimbo watakuwa ni kama mkuu wa mkoa wa kuchaguliwa na wanainchi wa mkoa husika na huyu lazima awe na elimu ya kutosha kusimamia maslahi ya mkoa , mkurugenzi wa mkoa huyu ni wa kuajiriwa na tume ya ajira ya mkoa kwa kuleta mkakati wake wa kusaidia mkoa kupiga hatua kwa kutumia rasirimali kidogo kwa matumizi ya wengi ambaye huyu atakuwa na timu yake ya kufanya kazi za kusukuma maendeleo kama ilivyoa sasa kwenye halmashauri zetu.

Viongozi wengine ni wabunge wa wilaya na madiwani wa kata husika zinazounda mkoa wa husika ama jimbo ambao hawa watakuwa na majukumu ya kuwawakilisha wanainchi kwenye serikali ya mkoa au jimbo.

Nini manufaa ya serikali za majimbo?
Haya ni baadhi ya manufaa ya serikali za majimbo.......

kupata uhuru wa kufanya maamuzi.
Kitu kingine muhimu kinachoweza sasa kutushawishi kuelekea kwenye serikali za majimbo ni kupata uhuru wa wanainchi kuamua nini wanataka na nini hawataki kifanyike mkoani mwao na hii bila kuingiliwa na mamlaka za juu hapa kwa mfano maamuzi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza na mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuamua kuondoa machinga kwa kuweka jiji safi na lenye staha wakati huo huo baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji hawakutaka jambo hili litendeke na mwisho wa siku likatendeka halafu anakuja mkuu wa nchi anasema hilo jambo halikupaswa kutendeka .....hii inaua maamuzi makini , ubunifu , weledi , na ufujaji wa fedha vibaya hapa ikumbukwe kuwa katika kuwaondoa machinga jiji Mwanza kunadhaniwa kulitumika fedha. sasa kuondoa hili ni kuwa na serikali za majimbo.

Serikali za majimbo zitaondoa dhana ya uporaji wa Rasirimali za mikoa husika,
kwakua serikali hizi zitakuwa zinafanya maamuzi ya rasirimali kwa manufaa ya wanainchi wa jimbo husika hakutakuwa tena na uporaji wa rasirimali kama madini , watu, fedha ,wanyama ,ardhi n.k kwa kisingizio kuwa serilikali inataka kutumia hiki ama serikali itachimba dhahabu kwa manufaa ya watanzania ambao hata hawaonekani na hapa kuna mifano anuai mingi tu ambayo imewafanya watanzania wengi kutoka kwenye majimbo yenye utajiri kuwa wakiwa na wengine kuwa na furaha sasa kwa maana hiyo serikali za majimbo ni suluhu ya jambo hili.

Serikali za majimbo zitasukuma maendeleo ya nchi kwa haraka zaidi.
Kutokana wanainchi kuamua kwa kila liwezekalo kujenga mikoa yao kupitia maendeleo ya mikoa nchi nayo itakuwa imepata maendeleo kwa haraka kwakua wanainchi watakuwa na hamasa ya kushindana na mikoa mingine na si kubweteka na kusubili ruzuku ya serikali kuwapa ili waendeshe mikoa yao , bali itawafanya kubuni njia za mapato nyingi ili kukidhi mahitaji yao na kwa maana hiyo mwanaichi hata shurtishwa tena kutoa kodi bali atatoa kwa hiari yake.

Ongeza maoni yako, kosoa na kuboresha kwa manufaa ya nchi.
 
Watakuja humu kupiga kelele lakini huu ni ukweli. Mamlaka mikoani yanazimwa polepole, sasa karibu kila kitu ni Dar es Salaam, kuna ukweli katika hili. Kuna propaganda ati majimbo yataleta ukabila, hii ni hoja mufilisi.
 
Ulichosahau ni kuwa serikali za majimbo hufanya kazi kwenye nchi ambazo zina ubaguzi wa
1.Kikabila
2.Rangi

Nchi zenye tabia hizo ndizo hutumia utawala wa majimbo.

Mfano ni Marekani ,Afrika ya kusini,Kenya,Nigeria ,INDIA,SUDAN NK.Kumaliza ubaguzi wa rangi na wa kikabila ndio Nchi hugawanywa kwenye majimbo.

Majimbo ni kama nchi kamili kabisa yenye raisi wake ambaye ni GAVANA wa JIMBO.Mtu kutoka jimbo moja kwenda jingine sehem zingine huhitaji kuwa na kitu kama passport na visa ya kuingilia jimbo lingine.

Tanzania haina tatizo la ubaguzi wa rangi wala kabila.

Mfumo wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo kuwa maskini wa kutupwa kama hayana raslimali.Mfano chini ya mfumo wa majimbo mkoa wa Morogoro ungeongoza kwa utajiri sababu umeme wote unatoka kidatu morogoro pesa zote za umeme nchi nzima wangetakiwa wapewe watu wa morogoro.
Bandari ya dar es salaa na uwanja wa ndege wa dar mapato yote yangekuwa ya dar tu hayaendi popote.Mikoa kama singida,dodoma,kigoma nk ingekufa maskini wasingekuwa hata na barabara ya lami.Marekani wanakotumia huo utawala wa majimbo kuna majimbo maskini hadi yanatia huruma.

Utawala wa majimbo ni wa wabaguzi wa kikabila na kirangi.
 
Ni kweli hii kitu inauma mtu anaposimama na kusema Dar ndo Tanzania wakati kuna mikoa ina rasilimalia nyingi kama madini Maziwa na Bunga lakini wananchi wake hata maji hakuna!
Me mwenyewa naitamani sana hii kitu!.
 
naona kwa mfumo huu ndo maana nchi hizo zina maendeleo ya uhakika ukilinganisha na mifumo yetu mibovu ambayo tunaitumia na kwa hoja ya mikoa mingine itakuwa maskini eti kwa kukosa rasirimali si kweli kwani kila mkoa una rasirimali za kipekee kwenye kila mkoa na kupitia rasirimali hizo wanaweza kupiga hatua za kimaendeleo ..ni kheri kufahamu mikoa Fulani haina rasirimali tukajikita kutafuta mbinu za kuiimboa kuliko kufanya kwa pupa bila takwimu halisi
leo hii mikoa yenye rasirimali ni masikini kama mikoa isiyo na rasirimali
 
Ulichosahau ni kuwa serikali za majimbo hufanya kazi kwenye nchi ambazo zina ubaguzi wa
1.Kikabila
2.Rangi

Nchi zenye tabia hizo ndizo hutumia utawala wa majimbo.

Mfano ni Marekani ,Afrika ya kusini,Kenya,Nigeria ,INDIA,SUDAN NK.Kumaliza ubaguzi wa rangi na wa kikabila ndio Nchi hugawanywa kwenye majimbo.

Majimbo ni kama nchi kamili kabisa yenye raisi wake ambaye ni GAVANA wa JIMBO.Mtu kutoka jimbo moja kwenda jingine sehem zingine huhitaji kuwa na kitu kama passport na visa ya kuingilia jimbo lingine.

Tanzania haina tatizo la ubaguzi wa rangi wala kabila.

Mfumo wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo kuwa maskini wa kutupwa kama hayana raslimali.Mfano chini ya mfumo wa majimbo mkoa wa Morogoro ungeongoza kwa utajiri sababu umeme wote unatoka kidatu morogoro pesa zote za umeme nchi nzima wangetakiwa wapewe watu wa morogoro.
Bandari ya dar es salaa na uwanja wa ndege wa dar mapato yote yangekuwa ya dar tu hayaendi popote.Mikoa kama singida,dodoma,kigoma nk ingekufa maskini wasingekuwa hata na barabara ya lami.Marekani wanakotumia huo utawala wa majimbo kuna majimbo maskini hadi yanatia huruma.

Utawala wa majimbo ni wa wabaguzi wa kikabila na kirangi.

Hivi hujaona dar inavyobagua sehemu nyingine na soon dodoma itakuwa hivyo hivyo. Lakini pia hili li nchi ni likubwa centre haiwezi kujua yote yanayotokea na mahitaji ya sehemu zote hivyo majimbo yanasaidia. Faida nyingine ni kuwa na ushindani kati ya majimbo na bado the centre itakuwa na madaraka yake.
 
Ubataka CCM tuchukue sera ya CHADEMA? Utasubri sana kijana!

Mzee Tupatupa
Haya mambo yapo siku nyingi CDM sio wa kwanza na wala hiyo isiwe nongwa. Kwani CCM hawajafanyia kazi hoja ya CDM au chama kingine. Kama inafaa ichukueni ipigeni msasa mtupe kitu bora. Mbona hata mkulu partly ametokana na sera za CDM hata kama wao walibadilisha gia angani. Ufisadi isingekuwa issue sijui raisi angekuwa nani kama si EL labda BM.
 
Ulichosahau ni kuwa serikali za majimbo hufanya kazi kwenye nchi ambazo zina ubaguzi wa
1.Kikabila
2.Rangi

Nchi zenye tabia hizo ndizo hutumia utawala wa majimbo.

Mfano ni Marekani ,Afrika ya kusini,Kenya,Nigeria ,INDIA,SUDAN NK.Kumaliza ubaguzi wa rangi na wa kikabila ndio Nchi hugawanywa kwenye majimbo.

Majimbo ni kama nchi kamili kabisa yenye raisi wake ambaye ni GAVANA wa JIMBO.Mtu kutoka jimbo moja kwenda jingine sehem zingine huhitaji kuwa na kitu kama passport na visa ya kuingilia jimbo lingine.

Tanzania haina tatizo la ubaguzi wa rangi wala kabila.

Mfumo wa majimbo husababisha baadhi ya majimbo kuwa maskini wa kutupwa kama hayana raslimali.Mfano chini ya mfumo wa majimbo mkoa wa Morogoro ungeongoza kwa utajiri sababu umeme wote unatoka kidatu morogoro pesa zote za umeme nchi nzima wangetakiwa wapewe watu wa morogoro.
Bandari ya dar es salaa na uwanja wa ndege wa dar mapato yote yangekuwa ya dar tu hayaendi popote.Mikoa kama singida,dodoma,kigoma nk ingekufa maskini wasingekuwa hata na barabara ya lami.Marekani wanakotumia huo utawala wa majimbo kuna majimbo maskini hadi yanatia huruma.

Utawala wa majimbo ni wa wabaguzi wa kikabila na kirangi.
Mbona hata hapa Tanzania kuna ubaguzi wa rangi na ukabila?
 
Hivi hujaona dar inavyobagua sehemu nyingine na soon dodoma itakuwa hivyo hivyo. Lakini pia hili li nchi ni likubwa centre haiwezi kujua yote yanayotokea na mahitaji ya sehemu zote hivyo majimbo yanasaidia. Faida nyingine ni kuwa na ushindani kati ya majimbo na bado the centre itakuwa na madaraka yake.

Tatizo la serikali za majimbo ni kubwa kuliko unavyoweza kuwaza.Tuchukulie mkoa wa ARUSHA LIWE JIMBO.Linaweza kutaka kuwa JIMBO MFANO KWA kujidai tu kuwa lina mbuga kubwa kuliko zote duniani ya ngorongoro ambayo huingiza mabilioni ya dola.Lakini ukiunda serikali ya majimbo kuna taabu nyingine huibuka.Wakazi wa ngorongoro hawawezi kubali mapato yao ya ngorongoro yaende kuhudumia watu wa Arusha mjini.Watataka yote yabaki ngorongoro.Ukianzisha pia serikali ya majimbo UKAANZISHA jimbo la Kilimanjaro kwa kuwa tu una kiburi kuwa una mlima kilimanjaro ambao watalii huingiza mabilioni watu wa Marangu wanaoishi kuzunguka huo mlima watagoma kuwa mapato ya mlima yasiende kokote zaidi ya kwao.Hawawezi kubali mapato ya mlima wao yaende kuhudumia watu wa Machame kwa MBOWE au SIHA au upareni.Kila mtu kwenye eneo lake na raslimali zake.

Tatizo kama hili ndio ile vita ya kabila la Ogon kule nigeria ambako ken saro wiwa mpigania haki za kabila la ogon alitaka mafuta yanayozalishwa pale yawe ya kabila lake na yafaidishe kabila lake hapo yanapochimbwa.

Nyerere aliliona hilo ndio akataka serikali moja isiyo na ukabila au ubagguzi wa aina yoyote

Ukianzisha serikali za majimbo usidhani eneo lisilo na hizo raslimali litakuwa na dezo ya kufaidi kienyeji.Ukigawa majimbo kiraslimali unaenda hivyo hivyo hadi kivijiji nk kijiji kisicho na chochote kisitegemee dezo kutoka vijiji vingine vyenye raslimali.
 
Naelewa wasiwasi wako lakini matemeo yangu majimbo yatakuwa kitu kipana zaidi na pia kuna kodi za kitaifa na central government itakuwa na uwezo wa income distribution. na niwazi sasa hivi wazo kama hili lawezekana kwani Mola ametujalia natural resources nyingi na pia makabila mengi yametawanyika Tanzania hivyo kupunguza hatari ya ukabila. Nafikiri ukiwa na dhamira na uongozi bora haya yanawezekana.
 
Tanzania tuna majimbo mawili na yanasumbua kama nini.Kuna jimbo la Tanganyika na Jimbo la ZAnzibar.Kilichopo unakijua.Ukianzisha majimbo mengi zaidi ya ZAnzibar unaelewa mziki wake utakavyokuwa mmzito.Hili la Zanzibar tu pasua kichwa.
 
Ni kweli hii kitu inauma mtu anaposimama na kusema Dar ndo Tanzania wakati kuna mikoa ina rasilimalia nyingi kama madini Maziwa na Bunga lakini wananchi wake hata maji hakuna!
Me mwenyewa naitamani sana hii kitu!.
Dar wana miundombinu gani yanmaana kuliko kwingine. Maji hakuna umeme shida barabara....

Usisahahu zaidi ya jusu ya mapato ya nji hii hukusanywa Kariakoo.
 
Back
Top Bottom