Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Joined
Sep 17, 2014
Posts
67
Reaction score
24
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi:

1. Mwanza, Kagera, Geita yawe BUKOBA STATE

2. Shinyanga, Tabora na Katavi yaitwe TABORA STATE.

3Dodoma, Singida na Morogoro yaitwe DODOMA DC STATE.

4. Dar, Pwani na Tanga yaitwe DAR ES SALAAM STATE.

5. Lindi, Mtwara na Ruvuma yaitwe COASTAL STATE.

6. Arusha, Manyara na Kilimanjaro yaitwe KIRIMANJARO STATE.

7. Kigoma na Rukwa yaitwe WEST STATE.

8. Mbeya, Iringa na Songwe yaitwe GREEN STATE,

9. UNGUJA STATE

10. PEMBA STATE.

Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.


Kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusiana na utendaji wa serikali katika kufanya maamuzi yake kuelekea kwa wanainchi wanaowaongoza , hali iliyopelekea maamuzi mengi kufanywa mkoani Dar es salaam kana kwamba nchi hii inao mkoa mmoja tu na mingine si mikoa bali ni wilaya, kata , mitaa na tarafa za mkoa wa Dar es salaam .

kufanya hivi kumeinyima mikoa mingine kupiga hatua za maendeleo kwa kutegemea Dar es salaam wanamua nini kuelekea mikoa mingine na mbaya zaidi mikoa hii imekuwa ikusanya mapato kutoka kwenye vyanzo duni walivyo navyo na kupeleka Dar es salaam na Dar ndo wanaamua nani tumpe? nani tumnyime? hali hii imedumaza fikra na utashi wa viongozi kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa weledi katika kuijenga mikoa yao.

serikali za majimbo ni nini?
hizi ni serikali za mikoa zenye mamlaka kamili ya kubuni na kukusanya mapato ya mkoa husika na kutumia kupitia bajeti ya mikoa yao na kutoa huduma kwa jamii ikiwemo huduma za msingi kama elimu , afya , miundombinu , na usalama maeneo yao husika.

viongozi wa serikali za majimbo watakuwa ni akina nani na watapatikanaje ?
viongozi wa serikali za majimbo watakuwa ni kama mkuu wa mkoa wa kuchaguliwa na wanainchi wa mkoa husika na huyu lazima awe na elimu ya kutosha kusimamia maslahi ya mkoa , mkurugenzi wa mkoa huyu ni wa kuajiriwa na tume ya ajira ya mkoa kwa kuleta mkakati wake wa kusaidia mkoa kupiga hatua kwa kutumia rasirimali kidogo kwa matumizi ya wengi ambaye huyu atakuwa na timu yake ya kufanya kazi za kusukuma maendeleo kama ilivyoa sasa kwenye halmashauri zetu.

Viongozi wengine ni wabunge wa wilaya na madiwani wa kata husika zinazounda mkoa wa husika ama jimbo ambao hawa watakuwa na majukumu ya kuwawakilisha wanainchi kwenye serikali ya mkoa au jimbo.

Nini manufaa ya serikali za majimbo?
Haya ni baadhi ya manufaa ya serikali za majimbo.......

kupata uhuru wa kufanya maamuzi.
Kitu kingine muhimu kinachoweza sasa kutushawishi kuelekea kwenye serikali za majimbo ni kupata uhuru wa wanainchi kuamua nini wanataka na nini hawataki kifanyike mkoani mwao na hii bila kuingiliwa na mamlaka za juu hapa kwa mfano maamuzi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza na mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuamua kuondoa machinga kwa kuweka jiji safi na lenye staha wakati huo huo baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji hawakutaka jambo hili litendeke na mwisho wa siku likatendeka halafu anakuja mkuu wa nchi anasema hilo jambo halikupaswa kutendeka .....hii inaua maamuzi makini , ubunifu , weledi , na ufujaji wa fedha vibaya hapa ikumbukwe kuwa katika kuwaondoa machinga jiji Mwanza kunadhaniwa kulitumika fedha. sasa kuondoa hili ni kuwa na serikali za majimbo.

Serikali za majimbo zitaondoa dhana ya uporaji wa Rasirimali za mikoa husika,
kwakua serikali hizi zitakuwa zinafanya maamuzi ya rasirimali kwa manufaa ya wanainchi wa jimbo husika hakutakuwa tena na uporaji wa rasirimali kama madini , watu, fedha ,wanyama ,ardhi n.k kwa kisingizio kuwa serilikali inataka kutumia hiki ama serikali itachimba dhahabu kwa manufaa ya watanzania ambao hata hawaonekani na hapa kuna mifano anuai mingi tu ambayo imewafanya watanzania wengi kutoka kwenye majimbo yenye utajiri kuwa wakiwa na wengine kuwa na furaha sasa kwa maana hiyo serikali za majimbo ni suluhu ya jambo hili.

Serikali za majimbo zitasukuma maendeleo ya nchi kwa haraka zaidi.
Kutokana wanainchi kuamua kwa kila liwezekalo kujenga mikoa yao kupitia maendeleo ya mikoa nchi nayo itakuwa imepata maendeleo kwa haraka kwakua wanainchi watakuwa na hamasa ya kushindana na mikoa mingine na si kubweteka na kusubili ruzuku ya serikali kuwapa ili waendeshe mikoa yao , bali itawafanya kubuni njia za mapato nyingi ili kukidhi mahitaji yao na kwa maana hiyo mwanaichi hata shurtishwa tena kutoa kodi bali atatoa kwa hiari yake.

Ongeza maoni yako, kosoa na kuboresha kwa manufaa ya nchi.
 
Hapo Utaleta Usawa Wa Mgawanyo Wa Rasmali Ingawaje Kuna Watu Hawataelewa Maana Yake
 
Umetumia vigezo vipi? usitupotezee muda. Eleza kitu kinachoeleweka. What? Why? How?



 
Naona sasa Chadema mnataka kuigawa nchi, Kwa hiyo kila COUNTY itakuwa na rais wake?
 
..... Siungi Mkono Majina Kama Bukoba State, Knjaro Na Mengne Yanayowakilisha Jina La Mkoa.
 
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.

Ccm hawataki kuona kitu kama hicho
 
Mfumo uliopo sasa ni mzuri sana kwani unawezesha maeneo madogo madogo kama mikoa kufanya kazi kama state badala ya kuwa na maeneo makubwa ambayo yataleta utendajiji hafifu.

Ndio maana tunaanzisha mikoa na wilaya mpya ili kusogeza huduma na kuondoa urasimu
 
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.

Serikali za majimbo ni mfumo ufaao kwa wale walioshindwa kuunda taifa moja hasa baada ya kutoka vitani.Marekani walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi basi.Wakaona waweke mfumo wa majimbo ambao kila bwana la vita litakuwa na jimbo lake halafu wawe na serikali ya shirikisho tu.Ndio kisa cha marekani kuwa na serikali za majimbo.Marekani ni nchi nyingi ndani ya nchi.Hizi nchi ndogo ndogo zinaitwa majimbo.

Urusi nao walipoanza kutwangana wakaona hawawezani wakaanzisha serikali za majimbo na kuwa na serikali ya umoja ile ya putin.

Afrika kusini nao walitwangana weee baadaye wakakubali yaishe nao wana serikali za majimbo.


Kenya pia baada ya vita za kikabila ilibidi waunde serikali za majimbo zenye magavana n.k ili kugawana madaraka kwa kila bwana la vita la kikabila.Wameshindwa kuunda Kenya moja.

Tanzania tuliweza kufanya nchi moja toka mwanzo hivyo majimbo yakamezwa sababu kila waanzisha serikali walitaka wote nchi moja tu.

Tatizo wengi ni watu wa ku-copy vitu bila kusoma historia ya kwa nini kulikuwepo majimbo? Mtu akienda USA akatembelea kule akapewa pizza na kuongeleshwa kingereza kidogo akirudi nchini anakuwa bila kutafakari utasikia sera ya chama chetu ni majimbo nimeona USA!!!!!

Nchi kama somalia na sudan kusini mojawapo ya namna ya kutatua matatizo yao ya kisiasa ni kuunda serikali ya majimbo ambayo kila jogoo la vita linapewa eneo linakokubalika halafu kunakuwa na serikali ya shirikisho.
Kuunda serikali ya majimbo kwa nchi kama tanzania ni kuisambaratisha nchi na kurudi kule kwenye ukabila na umaeneo.
 
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.

Na kwanini isiwe Jimbo la Bukoba badala Bukoba State? yaani kwanini tutumie neno State na SIYO Jimbo?
 
Ulichoandika kina akisi msimamo wa January Makamba kuhusu sera ya majimbo
 
We mjinga sana, kenya wana marais wangapi? Haupo mfumo huu huko kenya? USA kuna marais wangapi...hivi vipropaganda vyenu vya kip umbafu huwa vinawasaidia nini, mshe nzi kabisa wewe

Naona sasa Chadema mnataka kuigawa nchi, Kwa hiyo kila COUNTY itakuwa na rais wake?
 
Kuwepo kwa mfumo wowote wa kiutawala ukiwemo wa majimbo lazima kuendane na mambo ya msingi kwa maslahi ya taifa: ULINZI NA USALAMA, UTAWALA WA SHERIA, UMOJA, USIMAMIZI NA MGAWANYO WA RASLILMALI, HUDUMA ZA MSINGI, NA UENDELEZAJI UCHUMI WA TAIFA kwa faida ya wananchi wote. Sijui kama Tz tumeimarika kiasi cha kuchukua mfumo wa utawala kama huu.
 
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.

Nakubaliana nawewe kuhusu majimbo lakini sikubaliani na wewe kuhusu majina ya majimbo. Mtazamo wangu ni

Jimbo la Kaskazini, Arusha, Manyara, Kilimanjaro.
Jimbo la Pwani: Dar, Pwani, Tanga.
Jimbo la kati: Dodoma, Singida Morogoro
Jimbo la kanda ya ziwa: Mwanza, Kagera, Geita, Mara,shinyanga
Jimbo la kusini: Lindi, Mtwara, Ruvuma
Jimbo la magharibi: Kigoma, Rukwa,tabora
Jimbo la nyanda za juu: Mbeya, Iringa
 
Back
Top Bottom