Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Marekani kafuatilie kila jimbo lina katiba yake.Ndio maana majimbo mengine yanaruhusu ushoga mengine hayataki na wameweka kwenye katiba zao.
America kuna katiba moja tu nayo ni Federal constitution ambapo states zote pale America zina_obey,States zimebakiwa na bylaws wanazozitumia ktk masuala madogo madogo kama vile immigration, elections, development projects, nk na bado hizo bylaws zinaendana na sheria zilizomo kwenye katiba mama (federal constitution).
 
Acha uongo.NAKUPA KATIBA YA JIMBO LA TEXAS HII HAPA

http://www.statutes.legis.state.tx.us/Docs/CN/htm/CN.1.htm
 
Ni vizuri wanasiasa na watunga sera wakawa wazi katika hili, kama kweli mfumo unatufaha waje watalamu katika jukwaa hili waseme je twaweza kweli ama la! kushindwa kuwashawishi wananchi katika mambo ya ukweli ila ubakia kusema
 
Acha uongo.NAKUPA KATIBA YA JIMBO LA TEXAS HII HAPA

THE TEXAS CONSTITUTION ARTICLE 1. BILL OF RIGHTS

Sasa hapo kipi kinakuchanganya?Hiyo bado ni bylaws tu.Kila nchi imejichagulia definition yake ya legal framework yake ieleweke vipi.Ebu nenda hapo Texas waulize wananchi ipi wanayoitambua kama constitution kati ya hiyo ya State na ile ya federation.Mbona hata NGOS na vyama vya siasa vinavyo katiba pia?
 
Ni vizuri wanasiasa na watunga sera wakawa wazi katika hili, kama kweli mfumo unatufaha waje watalamu katika jukwaa hili waseme je twaweza kweli ama la! kushindwa kuwashawishi wananchi katika mambo ya ukweli ila ubakia kusema

Ni bahati mbaya wanasiasa na vyama hawataki kuelezea sera zao.Wanachokalia ni kulipua mabomu tu ya nani kala nini au kaiba.Sawa yule kala au kaiba lakini wewe sera zako ni zipi zifafanue hawataki.Yaani inauma sana.Hawawatendei haki wananchi kwamba je wachague mtu kwa kuwa kalipua bomu au wamchague kwa sera zake.Wanaweka wapiga kura njia panda kwenye mikanganyiko.Mtu ansema tu sera ya majimbo halafu anatokomea bungeni au mitini bila kufafanua wala nini.
 
Yaani mkoa wa MARA uuite BUKOBA STATE!!!!! Utapigwa panga wewe(just kidding).
Ila huo mfumo wa majimbo ukikosa uongozi mzuri ni hatari kwa umoja wa kitaifa.
 
Sasa hapo kipi kinakuchanganya?Hiyo bado ni bylaws tu.Kila nchi imejichagulia definition yake ya legal framework yake ieleweke vipi.Ebu nenda hapo Texas waulize wananchi wanatii constitution ipi kama si ya federation.Mbona hata NGOS na vyama vya siasa vinavyo katiba pia?

Kwa hiyo hawajui kingereza.Hawaelewi maana ya Constitution na Bylaws? wewe ndie unajua?
 
Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE - washirikishe Wameru usikie mawazo yao? hawatakubali kamwe kitu kama hicho
 
Ccm hawataki kuona kitu kama hicho

Sio kila kitu kinachosemwa kinyume na ccm ni kizuri au sio kila kinachofanywa na ccm ni kibaya. Serikali za majimbo zinaweza kuwagawa watu kwani jimbo linakuwa kama nchi jirani ya kenya, uganda au rwanda, hivyo kunakuwa na utaratibu wa kuingia na kutoka jimbo moja kwenda lingine.
Kila jimbo linakuwa na utawala wake, hadi hapo hamuoni kuwa majimbo yenye utajiri wa raslimali yanaweza kuwa na sheria kali za uhamiaji hasa kwa vijana wanaosaka maisha? Hao wanaotaka tuwe na mfumo huo wangeuelezea faida na hasara zake kwa kulinganisha na mfumo wa sasa kwa mazuri na mabaya yake, au kama ni mfumo wa kuiga unaweza kuboreshwa kuendana na hali halisi ya Tanzania.
 
Serikali za majimbo ni mfumo ufaao kwa wale walioshindwa kuunda taifa moja hasa baada ya kutoka vitani.Marekani walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi basi.Wakaona waweke mfumo wa majimbo ambao kila bwana la vita litakuwa na jimbo lake halafu wawe na serikali ya shirikisho tu.Ndio kisa cha marekani kuwa na serikali za majimbo.Marekani ni nchi nyingi ndani ya nchi.Hizi nchi ndogo ndogo zinaitwa majimbo.

Urusi nao walipoanza kutwangana wakaona hawawezani wakaanzisha serikali za majimbo na kuwa na serikali ya umoja ile ya putin.

Afrika kusini nao walitwangana weee baadaye wakakubali yaishe nao wana serikali za majimbo.

Kenya pia baada ya vita za kikabila ilibidi waunde serikali za majimbo zenye magavana n.k ili kugawana madaraka kwa kila bwana la vita la kikabila.Wameshindwa kuunda Kenya moja.

Tanzania tuliweza kufanya nchi moja toka mwanzo hivyo majimbo yakamezwa sababu kila waanzisha serikali walitaka wote nchi moja tu.

Tatizo wengi ni watu wa ku-copy vitu bila kusoma historia ya kwa nini kulikuwepo majimbo? Mtu akienda USA akatembelea kule akapewa pizza na kuongeleshwa kingereza kidogo akirudi nchini anakuwa bila kutafakari utasikia sera ya chama chetu ni majimbo nimeona USA!!!!!

Nchi kama somalia na sudan kusini mojawapo ya namna ya kutatua matatizo yao ya kisiasa ni kuunda serikali ya majimbo ambayo kila jogoo la vita linapewa eneo linakokubalika halafu kunakuwa na serikali ya shirikisho.
Kuunda serikali ya majimbo kwa nchi kama tanzania ni kuisambaratisha nchi na kurudi kule kwenye ukabila na umaeneo.
Umenena. Na huo ndiyo ukweli. Na ukiangalia sana nchi zote zilizo na mfumo wa majimbo hapa afrika, bado kuna kitu kama ukabila kinawatafuna. Mifano mizuri umeisema kama Somali, sudani kusini, Nigeria, Ethiopia nk,. Kwa sababu baadhi ya tawala za majimbo zinakuwa dhaifu matokeo yake ni vuguvguvu la kuondoa utawala wa jimbo na vurugu zinaanza na hiyo inakuwa shida ya nchi nzima. Ethiopia ni mfano mzuri. jimbo la Oromyia, mapigana yapo ambayo yamewafanya watu wawe wakimbizi kwa sababu ya udhaifu uliokuwepo kwenye jimbo hilo. sasa wanataka kujitenga. Ethiopia ilipoanzisha majimbo, watu wasitoka kwenye majimbo wafukuzwa. hasa wafanyakazi, walirudishwa makwao ili watu wa jimbo hilo wapate kazi. Tukianzishwa majimbo sitashangaa Msambaa anayefanyakazi Mwanza kufunkuzwa au makonde aliyeopo Kigoma kurudishwa Mtwara. hatujashindwa TZ kuendesha nchi kama ilivyo, kitu cha mhimu ni kuwa na mgawanyo sawa wa mapato, watu wadilifu na wenye weledi wanatakiwa waongoze hii nchi. siyo wanaoingia kwenye madaraka kwa njia ya fedha.
 
Sio kila kitu kinachosemwa kinyume na ccm ni kizuri au sio kila kinachofanywa na ccm ni kibaya. Serikali za majimbo zinaweza kuwagawa watu kwani jimbo linakuwa kama nchi jirani ya kenya, uganda au rwanda, hivyo kunakuwa na utaratibu wa kuingia na kutoka jimbo moja kwenda lingine.
Kila jimbo linakuwa na utawala wake, hadi hapo hamuoni kuwa majimbo yenye utajiri wa raslimali yanaweza kuwa na sheria kali za uhamiaji hasa kwa vijana wanaosaka maisha? Hao wanaotaka tuwe na mfumo huo wangeuelezea faida na hasara zake kwa kulinganisha na mfumo wa sasa kwa mazuri na mabaya yake, au kama ni mfumo wa kuiga unaweza kuboreshwa kuendana na hali halisi ya Tanzania.

Faida zake ni nyingi sana,chache nizijuazo ni hizi:
1)utasaidia kuondoa urasimu ktk uekezaji,makampuni yanayotaka kuwekeza yatasajili moja kwa moja ktk serikali za majimbo
2)utachochea ushindani wa kimaendeleo kati ya majimbo
3)maendeleo yatapatikana kwa haraka ktk majimbo husika kwavile vipaumbele vya miradi ya kimaendeleo vinafahamika vyema na rasilimali fedha na watu vitakuwepo vya ku_implement these development programs
4)utasaidia kupanua wigo wa kidemokrasia kwa kuwa kila chama kinaweza kupata fursa ya kutawala majimbo flani na hivyo kupata pia fursa ya Ku_implement sera zao za kiuchumi na endapo zitaleta mafanikio ktk majimbo hayo itakuwa mwanzo wa vyama hivyo kuaminiwa na hivyo kupewa ridhaa ya kuongoza nchi.
5)unasaidia kuondoa uhodhi (monopolization of power) wa madaraka wa chama kimoja kama ilivyo sasa
6)unasaidia kupunguza matumizi makubwa ya serikali kuu kwakuwa shughuli nyingi muhimu za kimaendeleo zitatekelezwa ktk ngazi za majimbo
Ni hayo tu yangu machache,wengine wataongezea.
 
Umenena. Na huo ndiyo ukweli. Na ukiangalia sana nchi zote zilizo na mfumo wa majimbo hapa afrika, bado kuna kitu kama ukabila kinawatafuna. Mifano mizuri umeisema kama Somali, sudani kusini, Nigeria, Ethiopia nk,. Kwa sababu baadhi ya tawala za majimbo zinakuwa dhaifu matokeo yake ni vuguvguvu la kuondoa utawala wa jimbo na vurugu zinaanza na hiyo inakuwa shida ya nchi nzima. Ethiopia ni mfano mzuri. jimbo la Oromyia, mapigana yapo ambayo yamewafanya watu wawe wakimbizi kwa sababu ya udhaifu uliokuwepo kwenye jimbo hilo. sasa wanataka kujitenga. Ethiopia ilipoanzisha majimbo, watu wasitoka kwenye majimbo wafukuzwa. hasa wafanyakazi, walirudishwa makwao ili watu wa jimbo hilo wapate kazi. Tukianzishwa majimbo sitashangaa Msambaa anayefanyakazi Mwanza kufunkuzwa au makonde aliyeopo Kigoma kurudishwa Mtwara. hatujashindwa TZ kuendesha nchi kama ilivyo, kitu cha mhimu ni kuwa na mgawanyo sawa wa mapato, watu wadilifu na wenye weledi wanatakiwa waongoze hii nchi. siyo wanaoingia kwenye madaraka kwa njia ya fedha.

Mkuu hata nigeria majimbo yamekuwa tatizo kubwa toka wapate uhuru.Jimbo la biafra lilileta shida.Hivi karibuni majimbo yenye utajiri wa mafuta yamekuwa yakileta shida nigeria kutimua wageni wasio wenyeji wa jimbo.Hivi wachaga kwa mfano wakikimbizwa toka majimbo mengine kwa sera hiyo wakaanza kukimbiza wageni warudi kwao kilimanjaro ardhi ya kilimanjaro inaweza ikawatosha kweli? Maana idadi yao hailingani na ardhi ya kilimanjaro!

Pia kuna majimbo ya kaskazini kule kwenye boko haram.Ni taabu tupu.Matatizo ya majimbo hayo hasa la maiduguri limekuwa tatizo la nchi nzima!Mfumo wa majimbo kwa afrika ni tabu tupu.Sielewi kwa nini una washabiki Tanzania.Afrika kusini watu huwa wanakimbizana kama kuku wakifukuza wasio wenyeji wazawa wa jimbo husika.Mfumo wa majimbo ukianza mbunge kama Lema hawezi kuwa mbunge Arusha!!!! Au KIWIA akawa mbunge wa Mwanza AU Mnyika akawa mbunge wa Ubungo au halima mdee akawa mbunge KAWE atatakiwa akagombee kwao ambako ndiko mzawa mwenyeji wa huko.

JImbo laweza pata uhuru na maendeleo.YAKIKOLEA LITATAKA KUJITENGA KUWA NCHI KAMILI.
 
Faida zake ni nyingi sana,chache nizijuazo ni hizi:
1)utasaidia kuondoa urasimu ktk uekezaji,makampuni yanayotaka kuwekeza yatasajili moja kwa moja ktk serikali za majimbo
2)utachochea ushindani wa kimaendeleo kati ya majimbo
3)maendeleo yatapatikana kwa haraka ktk majimbo husika kwavile vipaumbele vya miradi ya kimaendeleo vinafahamika vyema na rasilimali fedha na watu vitakuwepo vya ku_implement these development programs
4)utasaidia kupanua wigo wa kidemokrasia kwa kuwa kila chama kinaweza kupata fursa ya kutawala majimbo flani na hivyo kupata pia fursa ya Ku_implement sera zao za kiuchumi na endapo zitaleta mafanikio ktk majimbo hayo itakuwa mwanzo wa vyama hivyo kuaminiwa na hivyo kupewa ridhaa ya kuongoza nchi.
5)unasaidia kuondoa uhodhi (monopolization of power) wa madaraka wa chama kimoja kama ilivyo sasa
6)unasaidia kupunguza matumizi makubwa ya serikali kuu kwakuwa shughuli nyingi muhimu za kimaendeleo zitatekelezwa ktk ngazi za majimbo
Ni hayo tu yangu machache,wengine wataongezea.

Hapo namba 4 kuna tatizo bado hujaliona. Sera ya ccm haikubaliani na serikali ya majimbo, sasa huoni kwamba endapo ccm ikashikilia majimbo kadhaa kuna uwezekano wa kubadili mfumo huo ambao wao hawautaki, unadhani kipi kitashindikana ukizingatia kwamba governer au mtawala wa jimbo ni kama rais wa nchi? Mfumo huu unatia shaka hasa kama mdau mmoja alivyosema hapo juu kwa kutolea mfano somalia na nigeria.
 
Acha uongo.NAKUPA KATIBA YA JIMBO LA TEXAS HII HAPA

THE TEXAS CONSTITUTION ARTICLE 1. BILL OF RIGHTS
Again nitakwambia kuna tofauti kubwa kati ya FEDERAL na DEVOLVED states. Katika federation power comes from the 'majimbo' up to the 'serikali kuu', lakini kwenye devolved state power ipo mikononi mwa serikali kuu na hizo za majimbo zinagawiwa tu! USA na Germany ni federal states, Kenya, UK, South Africa na India ni devolved states. Kuhusu kuwa na katiba inategemea tu na makubaliano kati ya serikali kuu na hizo serikali za majimbo.
Tanzania hatuundi federation tunaunda a devolved state!
 
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.
Kwa nini kila mkoa usiwe ni jimbo kivyake (Na Zanzibar iwe ni jimbo moja tu)? Jumla tutakuwa na majimbo 26, ambayo ni sawa kwa nchi kama Tanzania. Kenya ni kama nusu yetu lakini wana majimbo 48!
 
Faida zake ni nyingi sana,chache nizijuazo ni hizi:
1)utasaidia kuondoa urasimu ktk uekezaji,makampuni yanayotaka kuwekeza yatasajili moja kwa moja ktk serikali za majimbo
2)utachochea ushindani wa kimaendeleo kati ya majimbo
3)maendeleo yatapatikana kwa haraka ktk majimbo husika kwavile vipaumbele vya miradi ya kimaendeleo vinafahamika vyema na rasilimali fedha na watu vitakuwepo vya ku_implement these development programs
4)utasaidia kupanua wigo wa kidemokrasia kwa kuwa kila chama kinaweza kupata fursa ya kutawala majimbo flani na hivyo kupata pia fursa ya Ku_implement sera zao za kiuchumi na endapo zitaleta mafanikio ktk majimbo hayo itakuwa mwanzo wa vyama hivyo kuaminiwa na hivyo kupewa ridhaa ya kuongoza nchi.
5)unasaidia kuondoa uhodhi (monopolization of power) wa madaraka wa chama kimoja kama ilivyo sasa
6)unasaidia kupunguza matumizi makubwa ya serikali kuu kwakuwa shughuli nyingi muhimu za kimaendeleo zitatekelezwa ktk ngazi za majimbo
Ni hayo tu yangu machache,wengine wataongezea.

Tatizo ni kuwa vyenye sera tofauti vikishika majimbo tofauti ni kichocheo cha vurugu.Mfano Nigeria kuna vyama vyenye mlengo wa kidini vimeshika baadhi ya maeneo ambako shariah law inatumika.Kwingine kunakuwa na maliberali.Nchi inakuwa ngumu kutawalika.Na ndio tatizo la Nigeria.

Pia nchi inatakiwa maendeleo yasambae kila kona.Wengine wasiachwe nyuma sana.Kukiwa na majimbo yenye uwezo sana yaweza amua kujitenga sababu hayaoni sababu ya kuwabeba wengine ambao uwezo wao mdogo.Nchi pia itakuwa haitawaliki kwa vituko vya majimbo yenye uwezo na yale yasiyokuwa na uwezo.

Wale majimbo ambao uwezo na maendeleo hawana kwa kuwa raslimali kwenye majimbo yao chache waweza anzisha vurugu kuwa wamekuwa maginalized.Na kuanza hata vita dhidi ya majimbo tajiri au wakadai kutaka kujitenga na kuwa nchi kamili.

Dawa ni kuwa na nchi moja inayojali maslahi ya watu wote na watu wote wakiwa huru kuishi popote,kufanya biashara,siasa,shughuli za kiuchumi popote wakiwa watanzania na si watu wanaobaguliwa kikabila,kijimbo au kivyovyote. kinyume cha hapo kutakuwa vurugu
 
As Tanzanians explore structures of government to adopt, I suggest they consider devolution.

Devolution refers to the statutory transfer of powers from the central government of a sovereign state – in this case the Union Government of Tanzania – to governments at a sub-national level – in this case the regions. It differs from federalism in that devolved powers ultimately reside in the central government, thus the state remains, de jure unitary.

Isn’t this the solution to our little problem? It offers us some kind of a midpoint between those who think that we need one government (Unionists) and those who are of the view that we need three (federalists). I subscribe to the view that none of the above will work to quash dissatisfactions fully, and that the latter will lead to the eventual collapse of the Union. As patriots, we should shiver to even entertain such a thought!

Now, imagine a scenario of three tiers of government: The Union government, the regional government and the local government. Each of the 26 regions of the country, counting Zanzibar as one, has its own regional government, consisting of a regional executive committee and a regional assembly.

The governors and the lieutenant governors are the chief executives and deputy chief executives of the regions respectively.

Of course, the Union government still controls the major revenue bases (income tax, Customs, corporate tax, VAT etc), but the regional governments collect some taxes such as property tax and all taxes on beer and gambling.

A given fraction of the union government’s revenues are shared out among the regions according to a given formula that takes various parameters such as population and land area into account.

Powers devolved to the regional governments include regional agriculture, regional education and health services, regional transport, intra-regional trade, regional planning and development, disaster management and emergency services, regional public works, coordination of local governments et cetera.

All powers not assigned to the regions remain as powers of the Union government. Each region has two senators who represent it in the senate, and is divided into a number of constituencies, depending on its population, for representation in the national assembly.

Each region also serves as a single member constituency for the election of women representatives to the national assembly. In accordance with the Union Treaty, should the president hail from one side of the Union (Tanganyika or Zanzibar), then the vice president must come from the other side.

In the above model, for one, the Zanzibaris will enjoy a reasonable amount of autonomy from the Union. They will have an assembly and executive, serving under a “Governor of Zanzibar.”

They will have authority to make and implement decisions that fall within their exclusive jurisdiction. However, they will have to recognise that they are part of a larger state, Tanzania.

Secondly, it guarantees the safety and continuity of our Union by establishing a strong Union government, unlike in the proposed federal structure. It also honours the Union treaty’s provision of having the president and vice president come from different sides of the Union.

Lastly, it brings with it all the advantages of having a devolved government, including more localised representation of political views, more localised spending of resources, promotes democratic and accountable exercise of power, balances economic development in the country, gives powers of self-governance to the people and enhances the participation of the people in national socioeconomic development, protects and promotes the interests and rights of minorities and marginalised communities.

If properly administered, each of our regions could be turned into a self-sufficient economic territory!
 
Again nitakwambia kuna tofauti kubwa kati ya FEDERAL na DEVOLVED states. Katika federation power comes from the 'majimbo' up to the 'serikali kuu', lakini kwenye devolved state power ipo mikononi mwa serikali kuu na hizo za majimbo zinagawiwa tu! USA na Germany ni federal states, Kenya, UK, South Africa na India ni devolved states. Kuhusu kuwa na katiba inategemea tu na makubaliano kati ya serikali kuu na hizo serikali za majimbo.
Tanzania hatuundi federation tunaunda a devolved state!

Majimbo Yote ni shida tu.Nenda india angalia jimbo la Kashmir linavyosumbua india.Jimbo lina utajiri mkubwa kutwa linaota kujitenga.Ni headache kwa india.Afrika kusini ni balaa tupu wanafukuzana na kukimbizana kwenye majimbo kama kuku.Huwezi KUISHI KWA RAHA au kugombea jimbo lisilo lako kama wewe si mzawa!!!

Nchi ulizotaja ubaguzi kwao ulianza siku nyingi na hivyo kufanya utawala wa majimbo kukubalika kama njia ya kutatua tatizo lao la ubaguzi.Mfano Uingereza (Ubaguzi wa kidini kati ya wakatoliki na waprotestant), Marekani (ubaguzi wa weupe na weusi na wenye kipato na wasio nacho), India (ubaguzi wa kikabila na kidini),Afrika ya kusini (ubaguzi wa rangi),Kenya (ubaguzi wa kikabila),Nigeria (Ubaguzi wa kikabila na kidini kati ya waislamu na wakristo) n.k hao ubaguzi wa kubaguana hawajaanza leo ni wazoefu.Ndio maana wakaamua kuwa na huo mfumo wa kibaguzi wa majimbo.

Tanzania haya tulishayafuta tukaunda nchi moja isiyo na ubaguzi.Ndio maana sera ya majimbo Tanzania haifai.
 
Back
Top Bottom