Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Wananchi wazalendo wa msomera mkoani Tanga, ambao hapo kabla walikua wakiishi ndani ya hifadhi ya Taifa ngorongoro, ambapo baadae kwa kushauriana na mamlaka za serikali, na kwa hiyari na utashi wao, Lakini pia kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa, na urithi wa vizazi vijavyo, wananchi wale waTanzania wazalendo walikubali kuondoka kutoka hifadhini na kwenda kuishi katika eneo mbadala walilotengewa huko msomera mkoani Tanga..
Wananchi hawa wazalendo nchini, kaya zaidi ya elfu moja, zenye watu zaidi ya elfu nane, walikubali wito wa Serikali wa kuondoka maeneo yale, ili kuepusha uharibifu wa mazingira ya hifadhi na kutunza mali asili katika eneo hilo ambazo zilikua zimaanza kuharibika na zilikua hatarini zaidi kupotea na kutoweka kabisa...
Na kwa hatua za kisheria na kikatiba ilizichukua serikali, eneo la hifadhi ya Taifa ya ngorongoro hakuna tena watu wanaishi ndani yeke..
Wavamizi wa hifadhi zote za Taifa nchini watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, ili kuilinda na kutunza maliasili za Taifa kwa maslahi mapana ya waTanzania wote...🐒
Mungu Ibariki Tanzania