Ni wakati wa Daraja la Kigamboni kupitika bure, bila kulipia

Ni wakati wa Daraja la Kigamboni kupitika bure, bila kulipia

keshobora

Member
Joined
Jun 5, 2024
Posts
32
Reaction score
76
Kutokana na wingi wa watu wanaokaa na kutembelea Kigamboni pamoja na shida ya usafiri kuelekea na kutokea Kigamboni ni wakati sasa wa serikali kufanya maamuzi magumu ya kuruhusu vyombo vya usafiri vipite bila tozo zozote ili kurahisisha huduma za usafiri.

Kwa tabu ambayo wanachi wanapata sasa ya kuvuka kwa foleni kubwa na kusubiri kwa sababu ya kulipia tozo, hakika umefika wakati serikali ilifikirie suala la kuacha kukusanye pesa ya kivuko. Ninaamini wananchi wengi sana wataongeza imani na serikali kwa kusamehe gharama za kivuko.

Note:
Kigamboni vivuko vinasumbua sana kwani vinachelewa kuja na vingi vinahitaji matengenezo watu wengi wanapanda ila roho juu sanaaaa, daraja ni mkombozi kwa mwananchi
 
Picha tafadhali kuonesha foleni kubwa nyakati gani katika Road toll Julius Nyerere bridge eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Daraja la Kigamboni lakusanya bilioni 83 tangu kufunguliwa 2016. Makusanyo yafikia 1.3B kwa mwezi -

Ughaibuni foleni njia ya kulipia
1717700034137.png

1717700221501.png
 
Daraja limejengwa kwa pesa za Wanachama wa NSSF siyo kodi za wananchi. So kile ni kitega uchumi cha NSSF

Na gharama yake bilioni za shilingi za kitanzania 337 hadi sasa wamekusanya jumla kubwa ya bilioni 83 tu tangu 2016, bado mwendo mrefu labda miaka karibuni 8 ijayo kwa mahesabu mtaji wa NSSF utakuwa umelipa.

Kigamboni waoneshe uzalendo hadi 2040 NSSF watakuwa wamerejesha gharama za uwekezaji
 
Hizo gharama serikali itazipata kwenye kodi nyinginee
 
Back
Top Bottom