Ni wakati wa Daraja la Kigamboni kupitika bure, bila kulipia

𝐓𝐮𝐧𝐚𝐤𝐨𝐞𝐥𝐞𝐤𝐞𝐚 𝐡𝐢𝐯𝐢 𝐯𝐢𝐯𝐮𝐤𝐨 𝐯𝐢𝐭𝐚𝐤𝐮𝐣𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐤𝐚𝐦𝐚 𝐌𝐰𝐞𝐧𝐝𝐨𝐤𝐚𝐬𝐢 𝐤𝐞𝐫𝐨 𝐲𝐚𝐤𝐞
 
Huo ndio ukweli.
Ukikopa ni LAZIMA ulipe, hakuna namna!
 
Acheni utahila, Hilo daraja serikali imekopa trilioni kadhaa kutoka NSSF Ndio maana wanakusanya
 
Kama daraja limerudisha pesa iliyotumika kujengea hakuna haja ya kulipia
 
Inawezekana,wakipunguza kununua ndege ,magari ya kifahari + kudhibiti ufisadi..
Hayo mengine uliyotaja ni porojo. Cha muhimu ni kuwa daraja limejengwa kwa michango ya wanachama wa NSSF na zinatakiwa zirudi.
 
"daraja limejengwa kwa pesa za wananchi maskini, na hao wananchi maskini wanalipia ili kupita kwenye daraja hilo" kweli hiki ni kichwa cha mwendawazimu.

Lile Daraja limejengwa kwa mkopo wa hela za NSSF na inaweza kuwa ni moja ya sababu ya wazee wetu kunapata hela kiduchu wanapostaafu.....
ILA ni kweli pia kuwa, ikimpendeza Mama Serikali ichukue/Ilipe hilo deni la NSSF watu wapite bure!
 
Hayo mengine uliyotaja ni porojo. Cha muhimu ni kuwa daraja limejengwa kwa michango ya wanachama wa NSSF na zinatakiwa zirudi.
Kwa hiyo wa daraja la Tanzanite(maana nalo ni mkopo Wakorea) nalo lilipiwe?...

Najua hutaki tu kukubali ,hilo jina linakutia UPOFU ila Serikali ikiamua kubeba huo MKOPO Inawezekana, nimekupa nini cha kufanya
ILA ni SUALA la Muda, tu,WanaKigamboni sio WAJINGA na wahaki ya kupata KEKI hata kidogo ya huyu Mama Tanzania
 
Kwani pesa zimerudi????
Nyie mnataka kupita dezo

Ova
 
Richard unaelewa nini watu wanachosemea? Mbona daraja la Wami hakuna hayo mambo.Mbali ya kuachia foleni lakini pia garama za kulipia kwani Kuishi kigamboni ndiyo iwe mateso kutoka na kurudi? Tanzanite mbona hakuna malipo? Nafikiri ni wakati muafaka wananchi wa Kigamboni nao wapate unafuu sasa katika kulipa maana ni Kigamboni pekee ndiyo watu wanalipa, Unasema sijui walipe kwa simu ishu siyo kulipa kwa njia ipi ishu garama za masiha na bado kulipia ndiyo kazi.Mbona kuna miradi mingi inalipwa na kodi na wananchi hawajalalamika sababu wanajua kulipa indirect.
 
Jamani ili tuoate huduma Bora heri tuwape sector binfasi wajenge na kutoza kama ilivyofanya NSSF kigamboni,,hivyohivyo hara daraja la kigongo busis linatakiwa magari yalipie ushuru ilinkurudisha pesa zilizojengwa ili zijenge hata Barbara za Rami za pembezon,,daraja la Tanzanite inatakaiwa magari na pikipiki yalipie ushuru ilia turudishe mkobo wa kolea huku tukibaki na Barbara..Tufa ye hibyo ili kupubgyza mikodkodi ya ovyoovyo sehemu nyingine
 
"daraja limejengwa kwa pesa za wananchi maskini, na hao wananchi maskini wanalipia ili kupita kwenye daraja hilo" kweli hiki ni kichwa cha mwendawazimu.
Daraja lilijengwa kwa pesa za mifuko ya wafanyakazi. Wakishakusanya Chao ni halali lirudishwe serikalini. Au serikali ifidie kilichobaki ipitishe wananchi wake bure
 
Acha kulazimisha watu waamini ujinga wako. Unatoa mfano usioendana na mada. Nchi haiendeshwi kwa huruma bali sheria.
 
Wapite bure kwani ni la serikali...pale wamewekeza watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…