Ni wakati wa Daraja la Kigamboni kupitika bure, bila kulipia

Mkuu nakuelewa uzuri sana ila nimelenga katika “maintenance” ya daraja.

Wenye ajira, wenye biashara zao wanapaswa kulipa kiasi fulani ili utunzaji wa daraja uwe na ufanisi. Hili daraja ni tofauti na daraja la wami kimatumizi kwani hili latumika na wakazi wote wa Kigamboni na hata wa kutembea.

Daraja la mto Wami ni jukumu la wizara ya ujenzi na miundombinu na lenyewe pia lilipaswa kudhibitiwa matumizi yake na kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara badala ya kupiga.

Nakuelewa sana ila Kigamboni ni daraja lilojengwa kimradi zaidi, hivyo tozo haiwezi kukosa.

Ndo maana nikasema waangalie hizo tozo na wawatoze wananchi kulingana na kipato chao.

Madaraja yote nchini kama yamejengwa kwa fesha za mkopo itabidi fedha kiasi pia zitoke kwenye tozo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…