Ni wakati wa kumpa credit zake Baraka Mpenja

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Tusisubiri mpaka mtu afe ndio tumpe sifa.

Kwa heshima na taadhima, leo nimeona tumpe sifa zake mtangazaji bora wa mpira hapa Tanzania kwa upande wa televisheni, ndugu Baraka Hudson Mpenja wa Azam Tv.

Huyu jamaa ni mbunifu sana, ana matumizi ya maneno yake flani flani hivi ambayo huleta ladha pale unapofatilia hizi mechi zetu za kibongo. Hakika kwa wafatiliaji wa mpira wa kibongo watakuwa wanaelewa nazungumzia nini!

Kwasasa Baraka Mpenja ndio anaifanya Azam Tv iendelee kuwa juu katika mechi za kibongo, na amechochea watu wengi kufatilia ligi ya bongo, ni wakati sasa wa Azam Tv kumleta Mwl Kashasha ili awe mchambuzi kando ya utangazaji wa Mpenja.

Hongera sana, Baraka Mpenja endelea kutupa burudani kwa karama yako kubwa uliyopewa na Mungu.
 
Kuna muda hayo maneno yanazidi na kukera sana. Awe professional aache uswahili mwingi. Ndio kutia chumvi mda mwingine sio mbaya ila ikizidi inakuwa kero sana sasa.

Nawashauri ma commentator wa kibongo wawasikilize akina Peter Drury watajifunza namna ya kuwa ma pro.

Still a learner though.
 
Picha tafadhali
 
Drury na Beglin ni habari nyingine aisee.
 
Huyo ukitaka umuelewe vizuri awe anatangaza mechi ya Simba au Mbao dhidi ya Yanga halafu Yanga wafungwe goli! Utamsikia what a goal! fantastic! bla bla nyingiii! Nahisi ni mshabiki wa mbumbumbu fc kama sikosei! Mimi simpi credit kwakweli.
Yanga mnachojua sasa hivi ni kulalamika tu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Maaajabu!! Haya ni maajabu!!
Linafungwa goal Gani Hili!!.
Nauliza!, Linafungwa Goal Gani Hili?.
Hivi Macho Yake Yanaona Kama Mimi!!.
Au Macho Yako Yanaona Kama Mimi.
Nani Alisema Simba Hawaendi hatua ya Makundi!!?.
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚Raha Sana Aiseh!!
 
Soka letu kivyetu vyetu. Hao wengine peleka hukoooo. Mtu mpenda sifa za kijinga utamjua tuu tunajadili soka la Bongo wewe unaleta ujuaji....shithole
Huelewi chochote wewe ji.nga sana. Mie nimem quote mtu mwingine unajipendekeza. Fuatilia niliye mquote then utagundua wewe ni fa.la.
 
Kwa hakika yuko vizuri sana huyu kijana! Amenikumbusha enzi za akina Ezekiel Malongo. Tupia picha na na. Ya cm nmpigie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ