Ni wakati wa Rais Samia kuziangalia bidhaa zilizopanda bei kutokana na matamko ya kisiasa na kuumiza wananchi wa hali ya nchi

Nimemwambia jamaa hajasoma bandiko langu bali amekurupuka tu kucoment maana kwenye bandiko nimeelezea hatua kwa hatua hata layman anaweza kunielewa.
 
Wiki iliyopita kwenye nakala ya gazeti la Daily News bodi ya Sukari walitangaza tenda ili apatikane mtu wa kuagiza Industrial Sugar.
Sasa industrial sugar, ilikuwa inaingizwa na wenye viwanda wenyewe, ikaonekana kuna uhuni unafanyika, ok!kama wameona watangaze tenda sawa!!ila kwenye brown sugar huku ndio kuna shida, kwanza hizo tenda kuzipata ni shida, na kuna wazee wachache tu(wahindi)ndio wanazo hizo hata kama wanazidiwa lakini wamesha hodhi soko!!
Wanatengeneza upungufu ili bei ipande, na viwanda vya ndani wanapiga tu kelele kuwa hawana soko wakati uwezo wa kulisha soko hawana!!
 
Lakini unakubaliana nini kilikuwa chanzo cha bei kupanda? Kama bei itakataa kushuka kwa sababu soko la dunia limebadirika pia haijustfy kilichofanyika huko nyuma.
 
Sasa mkuu sukari ni tofauti kwani kwa tanzania kwa mwaka mahitaji ni kama tani 450, 000 lakini viwanda vya ndani uwezo wake ni kama tani 150, 000! tu!!hawawezi kuwa na nguvu ya kupanga bei ya soko, ndio maana miaka kama 7 nyuma viwanda vya ndani vilikuwa vinalia kukosa soko la sukari yao kutokana na bei kuwa kubwa kulinganisha na sukari ya nje, ni kweli kuna nyingine ilikuwa inaingizwa kwa magendo.ila kodi kubwa ni chanzo hasa cha bidhaa kutofautiana bei toka nchi moja na nyingine.
 
Sasa pengo la tani 300,000 linazibwaje? Sio ndio kusababisha kupanda kwa bei?
 
Yaani mambo mengine kweli, huwa yanaudhi sana...eti kulinda viwanda vya ndani... yaani kulinda uzembe na uroho wa wachache, kujitajirisha na kuumiza wananchi wasio na uwezo wa kuwa na viongozi, wenye uchungu wa kusemea.... yaani jamani tunaomba Mama yetu ikikupendeza, kwenye hali sema neno ili roho za watu wako zipone... kazi iendelee.
Jambo la msingi sana hilo mkuu. Maana huku kwetu Lita 20 ya mafuta ya kupikia inaenda mpaka 84,000/= (mafuta ambayo si alizeti)
 
Magufuli ndio chanzo cha yote ayo, anaingia yeye sukari bei kg tsh 1800/=, akaleta siasa zake sukari ikapanda na haikushuka Tena, ilibakia kutuma task force kuvamia magodown ya watu
 
rubbish
 
Na sisi tuemdeleze kwa kasi kilimo cha michikichi, sun flag, karanga na mazao mengine yanayoweza kuzalisha mafuta ya kula na kushawishi wawekezaji ujenzi wa viwanda vya kutosha kwenye uzalishaji wa mafuta haya.
 
Kulinda viwanda vya ndani ni jambo jema ila kuwe na mipaka. Sio kulinda kwa gharama za mlaji wa mwisho.
 
Na sisi tuemdeleze kwa kasi kilimo cha michikichi, sun flag, karanga na mazao mengine yanayoweza kuzalisha mafuta ya kula na kushawishi wawekezaji ujenzi wa viwanda vya kutosha kwenye uzalishaji wa mafuta haya.
Kabisa mkuu. Hii ni fursa pia kwa watanzania.
 
Sasa pengo la tani 300,000 linazibwaje? Sio ndio kusababisha kupanda kwa bei?
Ndio maana huo upungufu wa tani laki 3, kila mwaka lazima sukari hiyo iagizwe toka nje, na ni miaka yote hilo linafanyika, sasa tatizo la awamu ya tano, kulijaa ukiritimba kwenye utoaji vibali hivyo, wanavitoa sio kwa muda muafaka, ndio maana tatizo limekuwa likijirudia kila leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…