Unadhani Mama hawajui? anawajuwa sana hawezi kuwa Rais wa nchi halafu aijue kitu gani kilitokea na kina nani waliokuwa wanataka kuichana katiba, anawajuwa vizuri sana na uhakika kisha shughulika nao, sio kwa kuwapiga ila anawatoa katika mfumo. Mimi nadhani Speaker wa bunge alihusika. Hata ile clip yake iliyomfanya aachie kiti ilikuwa kama sababu tu walimlia timing tu, kwani ile hotuba ungeiskiliza yote hakusema vibaya lakini watu wakakata kile kipande jamaa ikabidi amwage tu. CCM wakimpenda mtu hawamuachi wangempigania lakini Ndungai aliachwa mzima mzima mpaka na siasa kachukia. Ndungai aliona fursa ile, mtu wa tatu alikuwa yeye baada ya makamu wa Rais, aliona aunde na machawa wake wapinge mwanamke ili apewe yeye lakini Jeshi wakasimama na katiba ndio maana akasema kuna watu walisahau katiba inasema nini. Ni Ndungai na wenzake kina Kabudi na yule mbunge wa Ismani.