Ni wapi naweza kupata mkopo usio na RIBA ndani ya Tanzania hii?

ToniXrated

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2022
Posts
1,134
Reaction score
2,993
Amani iwe nanyi.

Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.

Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.

Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!

Asanteni
 
Mkuu usiendekeze Sana dini!
Au muombe Mungu huo mkpo wa bila riba.

Mambo mengine ni outdated! Kwaiyo wanafunzi wasipokee pesa(helbs) kwa Sababu ya riba??!

Fanya Kama dharula.
#nakopesha laki Moja kwa laki na nusu
10m kwa 15m
Karibu
 
Asante kwa mchango wako!
 
Amana bank wameanza kuweka riba? Au wale PBZ..jaribu kucheck bank hizi
 
Amani iwe nanyi.

Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.

Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.

Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!

Asanteni
Kama mtumishi kakope hazina....
 
Nenda msikitini
 
Kwanza nikupongeze Kwa kushikilia dini. Jitahidi pia usichepuke, Wala usipige mitungi.
Kuhusu mikopo, Check na NBC, Wana hicho kitengo Cha Islamic banking. Au People's Bank of Zanzibar. Wana hiyo mikopo isiyo na riba.
 
Amana bank wameanza kuweka riba? Au wale PBZ..jaribu kucheck bank hizi
Hawakopeshi fedha , wanakopesha vitu ambapo ni mfumo ule ule wa riba tu sema umezungushwa.

Mfano unataka milioni 10 ununue gari, wao wanasema tunalinunua hilo gari kwa 10m halafu tunakuuzia wewe kwa milioni 13. Then unalipa kidogo kidogo.

Ila ukiwafata wakupe fedha hawatoi.
 
Quran 2:275

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu
 
Kuna kuazima na kukopa....kuazima utarudisha km ilivyo na hiyo ni kwa mtu unayemfahamu...kukopa ni kwa mtu ambaye hamjuani au taasisi na yeye hiyo ni kazi yake sasa atafanyaje kazi isiyokua na faida!
 
Quran 2:278-279

"Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini.

Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe."

Sasa ndugu kuamua kujitangazia vita na Mungu kwa ajili ya Riba si balaa hili. Maana hujui Mungu atakupiga pigo gani, wapi na lini. Na kwenye vita ,Mungu siku zote ndio mshindi.

Nimeshuhudia watu wakifilisiwa kutokaana na hii mikopo ya Riba na hata wale ambao mwanzo biashara zao zilionesha ustawi mkubwa baadae zilikuja kuyumba na wakaanguka.
 
Back
Top Bottom