Mkuu unasoma hizo "aya" bila uelewa wake..........ikiwa wataka hivyo ulazimishavyo iwe basi Waislamu wote haitowafaa biashara yoyote
Uislamu juu ya suala la Riba..umetoa njia ambazo waislamu wataweza kuepuka "Riba" hiyo isiyotakiwa
Yasiofaa
1.haifai kuomba riba
2.haifai kuomba mkopo wenye riba
Ifaavyo
3. Musharakah - mwenye pesa na mwenye biashara wanakuwa washirika, wanafanya pamoja na kugawana faida
4.Murabaha-Benki inanuua bidhaa unayotaka,halafu inakuuzia kwa faida (Cost-plus financing)
5..Ijarah-benki inakukodisha kifaa na unanua baada ya muda wa kukodi (Lease)
6.Bay Salam - Mfano, mkulima analipwa kabisa kwa ajili ya mazao yake, na aleta mazao baada ya kuvuna bdae
7.Mudharaba-Benki inawekeza kwako na kuchukua asilimia ya faida ya shughuli husika (e.g 60:40) (Profit n risk sharing)
ziada
Muislam hapaswi kuwekeza (invest) kwenye kitu chochote, kuna utararibu wake na tathmini lazima ifanyike kujua kama maeneo hayo yanakubalika kisheria (sharia compliant).
Tunajua kuwa huwezi ku invest kwenye pombe, kamali, riba, n.k, lakini sio hivyo tu. Kampuni inaweza kuwa kwenye biashara halali, mfano kilimo, lakini ikakosa vigezo vingine vya uwiano wa ki-fedha (financial ratios).
Vigezo hivi vya ki-fedha vinaangalia;
1. Kiasi cha mkopo wa riba kinachangia kiasi gani katika mali zote za kampuni (interest-bearing debt/total assets shuld not exceed 30%)
2. Kiasi cha amana (interest-earning) kampuni ilichoweka benki na mali zote (interest-bearing deposits/total assets) kisizidi 30%
3. Kiasi cha mapato yanayotakana na maeneo yaliyokatazwa yasizidi 5% (non-permissible income)
4. Na “accounts receivables” zisizidi 49% ya mali za kampuni
Kama unataka kununua hisa (shares), kampuni lazima ikidhi vigezo hivyo juu.
Na hii sio kwa waislam tu, ni kwa mtu yoyote, kwa kuwa vigezo hivyo vinaiweka kampuni katika nafasi nzuri ya kuwa na maendeleo makubwa (high growth potential)
Mwisho
Watu wengi wanalalamika kuwa ni ngumu kuepuka riba, baadhi ya sababu wanazotoa ni hizi;
1. Wanatia shaka huduma za kibenki za kiislam na kusema kuwa ni ujanja tu kubadili riba na kuiita faida. Matokeo yake wanaendelea kutumia huduma za kibenki za kawaida (conventional banking)
2. Hawana hufahamu wa utararibu wa huduma za kibenki za kiislam
3. Wanasema benki za kiislam zinatoa masharti magumu ya mikopo, haswa like suala ka kutotoa mikopo ya fedha taslim (cash loans). Hali hii inapelekea thamani ya benki za kiislam (total assets) kuendelea kuwa chini ya assets za conventional banks.
Ukiangalia total assets za 50 top conventional banks only ni USD 69.6 trillion, wakati za islamic banks total globally ni USD 2.2 trillion, ila ukuaji unaendelea vizuri.
JE, NI VIP TWAWEZA KUEPEKANA NA RIBA?
KI-Iman (Religiously)
1. Kuamini kuwa rizki inapangwa na Mwenyezi Mungu, waweza acha riba na Yeye akakupa rizki yako kama kawaida (tawakkul)
2. Kumbuka kuwa kuna adhabu kubwa ya kujihusisha na riba (punishment). Financially
1. Fungua akaunti katika benki zenye utararibu usio na riba
2. Wekeza pesa zako katika mifumo isiyo na riba. Usiweke pesa zako kwenye government bonds, government bills, stocks (hisa) za makampuni yenye kufanya biashara haramu, speculation, n.k
3. Fungua akaunti za akiba (savings) ili uepukana na haja za kuomba mikopo
4. Usiingie mikataba yenye masharti ya kulipa penalties za riba
Socially (ki-jamii)
1. Ishi kwa mujibu wa kipato chako (live below your means) ili kuepuka vishawishi vya kutaka kukopa
2. Jiunge na utaratibu wa vikundi vya kupeana mikopo isiyo na riba, kama vile islamic saccos
Kumbuka kuwa madhara ya riba ni mabaya hapa duniani, na mibaya zaidi kesho akhera.
Surah Al-Baqara, Verse 276:
يَمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ
Allah does not bless usury, and He causes charitable deeds to prosper, and Allah does not love any ungrateful sinner.
Some Credit ziende kwa: Salum Awadh
cc.Partner in business
Mshana Jr