Ni wapi naweza kupata mkopo usio na RIBA ndani ya Tanzania hii?

Torati 23:19-20
 
Kwahiyo ni haram kwa muislam kuwekeza pesa zake katika Mifuko kama UTT amis au kununua shares?

Hebu tufafanulie ndugu kwa faida ya wote
Quote kwenye post hiyo

"Muislam hapaswi kuwekeza (invest) kwenye kitu chochote, kuna utararibu wake na tathmini lazima ifanyike kujua kama maeneo hayo yanakubalika kisheria (sharia compliant)"
 
Ndugu mfano nataka nikope pesa kwa ajili ya kufanya biashara yangu ya ununuzi wa mazao vijijini huko, lets say 10M ...halafu naenda ktk benki ya kiislam mfano amana bank wanawezaje kunisaidia kupata kiasi hicho cha fedha ilihali wanasema hawatoi pesa taslim?!
 
Hapa Tanzania huwezi kupata nenda Burundi uko unaweza kupata
 

Njia pekee nikuingia partnership na wewe...mtaifanya hiyo biashara pamoja mkigawana faida ama hasara
aidha kwa makubaliano ya kimlinganyo wa shares au mnakuwa washirika mkifanya biashara pamoja nakugawana faida
 
Mkuu usiendekeze Sana dini!
Au muombe Mungu huo mkpo wa bila riba.

Mambo mengine ni outdated! Kwaiyo wanafunzi wasipokee pesa(helbs) kwa Sababu ya riba??!

Fanya Kama dharula.
#nakopesha laki Moja kwa laki na nusu
10m kwa 15m
Karibu
Unaweza nikopesha mil 200 narudisha mil300
 
Ameen..shukran ndugu
 

Kumbukumbu la Torati 23:19-20 SRUV​

Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu chochote kikopeshwacho kwa riba; mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
 
njia pekee nikuingia partnership na wewe...mtaifanya hiyo biashara pamoja mkigawana faida ama hasara
aidha kwa makubaliano ya kimlinganyo wa shares au mnakuwa washirika mkifanya biashara pamoja nakugawana faida
Kwahiyo kinachotakiwa ni kuwaeleza mategemeo ya faida unayoweza kuipata katika biashara n.k then wao ndio wanapanga uwagawie faida kiasi gani ? Vp kuhusu ile principle wanayokupa (10M)?? Unawarudishiaje?
 
Mungu anaruhusu riba

Na ndo maana wale waliopewa Taranta, aliyezifukia alimtoa na kusema bora ni yule aliyepeleka kwa watoza riba na taranta kuongezeka
 
Nenda BRANCH huko unaweza ukaamua usirudishe. Pesa ziko nje nje. Shusha application Yao kwenye simu yako ndani ya dakika kumi utapata mkopo wa bure. Utarudisha siku ukijisikia. Nadhani wale ndugu zao TALA hawapo Tena nchini. Nao walikua wanakopesha mpaka wapiga debe vituo vya daladala.
 
Mungu anaruhusu riba

Na ndo maana wale waliopewa Taranta, aliyezifukia alimtoa na kusema bora ni yule aliyepeleka kwa watoza riba na taranta kuongezeka
Kwa imani yako ila kwenye uislam hilo jambo ni HARAM
 
Ehh kumbe
Japo faida yake ni kwamba watu watatimiza malengo husika
 
Kuna ile bank ya Kiislamu inatwa AMAN kama sikosei hawana riba
 
Tupiamo link yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani iwe nanyi.

kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Asanteni

Amini nakuambia, tofauti na muislamu mwenzako, hakuna mkopeshaji asiyependa riba. Kwa andiko lako maana yake ni kwamba, hata akikupa sehemu ya pesa yake bila kukutoza riba (asiye muislamu) lazima kuwemo na riba aliyowatoza wengine.

Nachelea kusema, MKOPO NI HARAMU KWAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ