Ni wapi naweza kupata nyama safi ya Kitimoto for the weekend hapa Dar

Ni wapi naweza kupata nyama safi ya Kitimoto for the weekend hapa Dar

Ilala boma pale flat kuna mbunifu anatengeneza hadi sambusa zake!ni tamu sana ukipata muda pita pale ule mishikaki,roast,kavu na sambusa zake!

Pia nasikia kuna sehemu mburahati huko inavuma sana ingawa wadau wanasema mazingira yake mmm,na sehemu nzuri kulizo zote dar kwa sasa nenda Coco Beach!pale utapata ya kuchoma na style ambayo hutaenda kula sehemu ingine!pita pale!wameiga wale wa slip way village pale ambao wanauza kwa uzito!400mg kwa 20,000 uzungu sana pita pale Coco!utanipa habari yake!

Na mwisho pia nakupa ubunifu wako!nenda sehemu yako unayopenda!waambie waichemshe kwanza nyama ulioagiza!ikiiva!nunua safari lager moja,mimina mule na funika iendelee kuchemka na ile nyama!ile bia(mafuta) ikikauka itakuwa iko tayari!ukila ile nyama na taste yake sidhani kama utapenda kula hizo roast au kavu tena!!!

Nadhani huyu ni yule kaka (stan-kempisk) aliyefariki kama mwezi june. Kweli tunakosa vitu vya uhakika hasa hii mboga alikuwa akiweka ile salad yake ya beetroot!
 
Leviticus 11:7-8 :- And the pig, because it parts the hoof and is cloven-footed but does
not chew the cud, is unclean to you. You shall not eat any of their
flesh, and you shall not touch their carcasses; they are unclean to
you.
 
hivi Dar Kuna sehemu maalum inapotengenezwa kitimoto ya PORI?
 
Tembelea Sinza B-Bar/Sinza Mbele ya Sansiro na Sehem Nyingine nyeti nzurii ya Kujificha ni Rudz Farm Bahari Beach ambapo atuweza kula Soseji zilizookwa za Kitimoto. Ni Balaaaaaaa.
 
Leviticus 11:7-8 :- And the pig, because it parts the hoof and is cloven-footed but does
not chew the cud, is unclean to you. You shall not eat any of their
flesh, and you shall not touch their carcasses; they are unclean to
you.
Mkuu! Sasa hivi hatupo tena chini ya sheria! The BLOOD OF JESUS flee us from Those laws! We are now free! Hivyo Usikariri! Elewa!!
 
Mleta post hujasema upo wapi ila kama upo Tanga, nenda mwembeni pale mapana. Utakutana na mtaalam Godi. Hutajuta aisee.
 
Leviticus 11:7-8 :- And the pig, because it parts the hoof and is cloven-footed but does
not chew the cud, is unclean to you. You shall not eat any of their
flesh, and you shall not touch their carcasses; they are unclean to
you.
Mkuu! Sasa hivi hatupo tena chini ya sheria! The blood of jesus flee us from laws! We are now free! Usikariri!
 
Maneno yote ni Mwenge pale nyuma ya TRA karibu na magorofa ya jeshi kuna bingwa anaitwa CHUWA,kuna jamaa alinipa ushuhuda kuwa hakuwahi kula nyumbani kwake kwa siku kama 20 hivi mfululizo maana kila jioni lazima aripoti hapo, ukila rosti unaweza kumtaliki mkeo,mimi huwa nabeba na mkate kabisa wa kumalizia ile rosti.
Mkuu umetisha aisee. Nimecheka hapa mpaka wife na son wananishangaa!
 
Back
Top Bottom