Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!

Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!

..Wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere baadhi ya Wachagga walihamishwa na kupelekwa Morogoro.

..Ndio maana leo hii Ifakara imetoa mbunge ambaye ni mzao wa Wachagga waliohamishiwa huko na Mwalimu Nyerere.

..Majuzi Mh.Kimei aliiomba serikali uangalie uwezekano wa kuwatafutia wananchi wake ardhi maeneo mengine nje ya Kilimanjaro.

..Nakumbuka kuna mwana JF alianzisha mada kuhusu ombi la Mh.Kimei lakini kulikuwa na michango mingi ya kibaguzi kupinga ombi hilo.

..Kwa taarifa yenu, hili zoezi litafika maeneo mengi ya Tanzania. Kuna dokezo la serikali kuhusu kutwaa ardhi za wananchi lilivuja na Mh.Ole Sendeka alihoji bungeni lakini Waziri Kairuki na Waziri Mhagama walikana kuwa dokezo hilo halijajadiliwa na serikali.

..Sikiliza hapa chini alichoongea Mh.Ole Sendeka.


View: https://m.youtube.com/watch?v=tz1QLDnaqIE&pp=ygUVT2xlIFNlbmRla2EgKyBrYWlydWtp

Cc Nguruvi3
 
Mada hii inaonekana ya kijinga jinga , lakini ni wake up call.

..kuna migogoro mingi sana inayohusu wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za taifa.

..nadhani unakumbuka jinsi Mh.Waitara alivyoangua kilio bungeni kuhusu matatizo, na migogoro, kati ya wahifadhi wa Serengeti, na wananchi wa jimbo la Tarime Vijijini.
 
Mimi binafsi siamini kwenye kuhamisha watu na kuwatoa kwenye makazi yao, ningetamani zaidi hiyo nguvu ingeelekezwa zaidi kwenye ELIMU ya utunzaji wa hizo maliasili..!!

tukisema tuwahamishe tutahamisha wepi na kuacha wepi..? Sote tunafahamu kuwa asilimia kubwa sana ya nchi yetu imezungukwa na ardhi yenye kila aina ya utajiri, tutafika pahala itabidi tuhamishe wakazi wa nchi nzima sasa..!

Ila ukhalisia unabaki pale pale hakuna nguvu yoyote inawekwa kwenye kulinda vivutio vyetu, tunataka tu faida bila kutengeneza mazingira madhubuti ya kulinda mazingira yetu..!!

Usinifanye niandike gazeti kwa uchungu mkuu kwa yanayotendeka..!!
Na population control ni muhumu sana pia
 
View attachment 3075375
Kama kuna kivutio cha utalii kinachojulikana duniani ni mlima Kilimanjaro.

Kivutio hiki kinaingiza watalii wengi sana mwaka hadi mwaka.

Jamaa wanaokaa karibu, ndugu zangu wachaga, wanachoma moto mazingira na kuharibu uoto kila mwaka.

Wahamishwe kwenda Msomera , Kilindi Tanga.

Kama imewezekana Ngorongoro, huku tutashindwa nini?

Wasalaam Aleikhum.

NB
Sitaki matusi.
Ho watalii a vibutio vya asili wakianza kuja Mbeya sijui tukimbilie Malawi?
 
View attachment 3075375
Kama kuna kivutio cha utalii kinachojulikana duniani ni mlima Kilimanjaro.

Kivutio hiki kinaingiza watalii wengi sana mwaka hadi mwaka.

Jamaa wanaokaa karibu, ndugu zangu wachaga, wanachoma moto mazingira na kuharibu uoto kila mwaka.

Wahamishwe kwenda Msomera , Kilindi Tanga.

Kama imewezekana Ngorongoro, huku tutashindwa nini?

Wasalaam Aleikhum.

NB
Sitaki matusi.

Good idea.

Kama kweli swala ni kulinda Mazingira waanzie huko tuone kweli wako serious ....!!

Anyway, wote tunajua kwa sasa kuwa Ngorongoro ni biashara ya Maza na Wajomba zake ..... Period. Hakuna cha mazingira wala mama yake mazingira.
 
Back
Top Bottom