Ni wazo tu: Wachaga wahamishwe maeneo ya Mlima Kilimanjaro!

..Wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere baadhi ya Wachagga walihamishwa na kupelekwa Morogoro.

..Ndio maana leo hii Ifakara imetoa mbunge ambaye ni mzao wa Wachagga waliohamishiwa huko na Mwalimu Nyerere.

..Majuzi Mh.Kimei aliiomba serikali uangalie uwezekano wa kuwatafutia wananchi wake ardhi maeneo mengine nje ya Kilimanjaro.

..Nakumbuka kuna mwana JF alianzisha mada kuhusu ombi la Mh.Kimei lakini kulikuwa na michango mingi ya kibaguzi kupinga ombi hilo.

..Kwa taarifa yenu, hili zoezi litafika maeneo mengi ya Tanzania. Kuna dokezo la serikali kuhusu kutwaa ardhi za wananchi lilivuja na Mh.Ole Sendeka alihoji bungeni lakini Waziri Kairuki na Waziri Mhagama walikana kuwa dokezo hilo halijajadiliwa na serikali.

..Sikiliza hapa chini alichoongea Mh.Ole Sendeka.


View: https://m.youtube.com/watch?v=tz1QLDnaqIE&pp=ygUVT2xlIFNlbmRla2EgKyBrYWlydWtp
Cc Nguruvi3
 
Ni kweli pia hapa Kizimkazi kuna fukwe nzuri sana zinazovutia watalii.

Tunaomba nasi watu wa kizimkazi tuhamishwe tuhamie Msomera ili zijengwe hotel nzuri na fukwe ziboreshwe na kuwa nzuri na bora kwa watalii.
Kuna madini?
 
Mada hii inaonekana ya kijinga jinga , lakini ni wake up call.

..kuna migogoro mingi sana inayohusu wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za taifa.

..nadhani unakumbuka jinsi Mh.Waitara alivyoangua kilio bungeni kuhusu matatizo, na migogoro, kati ya wahifadhi wa Serengeti, na wananchi wa jimbo la Tarime Vijijini.
 
Na population control ni muhumu sana pia
 
Ho watalii a vibutio vya asili wakianza kuja Mbeya sijui tukimbilie Malawi?
 

Good idea.

Kama kweli swala ni kulinda Mazingira waanzie huko tuone kweli wako serious ....!!

Anyway, wote tunajua kwa sasa kuwa Ngorongoro ni biashara ya Maza na Wajomba zake ..... Period. Hakuna cha mazingira wala mama yake mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…