"Ni yeye 2020" Ni slogan mbovu kwa CHADEMA kuelekea Uchaguzi

"Ni yeye 2020" Ni slogan mbovu kwa CHADEMA kuelekea Uchaguzi

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,792
Reaction score
2,421
Kile ambacho CHADEMA imekuwa ikikosoa wengine ndicho inachokuja nacho. Walilalamika juu ya neno Tanzania ya Mag..... .

Kwanini CHADEMA mnakuja na slogan inayohusu mgombea na sio wananchi. Je, uchaguzi huu umelenga kuwa na faida kwa nani!? Mpiga kura au mpigiwa kura.

Kama ilivyokuwa kwa CCM walivyokuwa na Moto tofauti Kama Hali mpya, nguvu na Kasi. Au hapa Kazi tu. WanaCHADEMA mnatakiwa mje na Moto utakaowalenga watu na sio mgombea.

Labda tuangalie mbele mamtoni Trump alikuja na slogan Make America great again. Africa Malawi mpinzani alikuwa na slogan yake.

Slogani ndio muongozo wa sera. Lazma CHADEMA mje na Moto uneoelezea kwa kifupi mnachotaka kukifanya. Uwe wazi, wa kiswahili, mfupi na unaoeleweka kirahisi.

Kuanza kutukuza wagombea sio swala sahihi. Kipi mnachokusudia kuwafanyia watanzania. Njooni na slogan mzuri. Kwa nilivyowasikiliza inaweza ikawa.

*Tanzania mpya ya haki na usawa kwa kila mtu.
hapa mtagusa kile mnachopigania kila siku, uchumi wa mtu moja moja, Uhuru wa kujieleza na katiba mpya

*Tanzania kwanza, uchumi wa mtu kwanza.

*Mwanzo mpya wa maendeo.
*Serikali ya watu
*Tanzania mikononi mwako.
*Mabadiliko halisi ya kiuchumi

*kwa pamoja tutafikia malengo

( Hapa mtahusisha kila haki ya kila mtu inagusa maendeleo ya mtu mwingine na lazma kuunganisha nguvu ili kuendelea) mfano

1. Maslah Bora kwa watumishi wa umma na sekta binafsi huleta Bei Bora ya mazao ya kilimo hasa chakula kwa wakulima, huwapa faida nzuri wafanya biashara hakuna anayeumia pekeyake. Mafundi na hata taasisi za fedha.
2. Au Kodi Rafiki na mazingira Bora ya biashara kwa wafanyabiashara huleta Bei nzuri ya bidhaa kwa watumishi, wakulima na raia wa kawaida.
3. Upatikanaji rahisi wa pembejeo, usafiri na uhuru wa kibiashara husaidia Bei nzuri ya vyakula.



Mi sio mpenzi wa chama chochote Cha siasa Ila naamini mtifuano mzuri wa sera nzuri utatupa mwanzo mzuri kwa atakaeshinda kuwa na vision haijalishi NI Nani. Upinzani imara NI lazma kwa maendeleo ya taifa.
 
Nimekuelewa sana.
Sema ile ya #NguvuYaUmma waliipatia sana
 
Nyinyiem bhana, Mara ooh nyalandu ndiye anayefaa sijui mara vile mara hivi yaani ili mradi tu
...... Vumilieni #mwisho wa ubaya aibu #
 
Kama huna mapenzi na vyama vya siasa unasubiri nini kufa ?
Instagram media - CDeBdaNJf1T ( 643 X 640 ).jpg
 
Slogan kitu gani bwana, tunaangalia sera, hataivo umejijibu mwenyewe haya ya mwisho.
 
Watu huru na Uhuru wa kupata habari pia uhuru wa taasisi , manispaa na Halmashauri ktk kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao ya kijiografia

Serikali Mpya kuweka mfumo thabiti na utaratibu kuzisaidia Idara zake za kiraia kufanya mabadiliko ya ndani kiutendaji ili kuziwezesha kuwatumikia watanzania bila ubaguzi na kwa haraka

 
Steven Lumola mjumbe toka Bukene, Tabora aongea mazito kuhusu maoni ya waTanzania wa mikoa ya Tabora, Singida, Morogoro, Pwani na Tanga katika mahojiano exclusive ndani ya Mlimani city wakati wa mkutano Mkuu wa CHADEMA



Source : EastAfricaRadio
 
Wakala aliyemwakilisha Tundu Lissu, David Jumbe, aongea na Swahilivilla TV
Mr. Jumbe ameongelea mwamko, wito, na utashi wa wananchi mikoani walivyo tiririka kutaka kumdhamini “Mtia Nia” Tundu Lissu



Swahili Villa Online TV kutoka Washington DC na Studio zetu za jiji Dar es Salaam Tanzania, tumefanya mahojiano na David Jumbe, ambae ni wakala aliyemwakilisha Makamu wa Chama cha Chadema Mr. Tundu Lissu kuchukuwa fomu ya kutia nia ya nafasi ya Urais kupitia Chama cha Demokrasia Na Maendeleo (Chadema).

Mr. Jumbe ameongelea mwamko, wito, na utashi wa wananchi mikoani walivyo tiririka kutaka kumdhamini “Mtia Nia” Tundu Lissu. Kwa mengi aliozungumzia, sikiliza Full Interview kati ya Dr. Patrick Nhigula na David Jumbe.
Source : swahili villa
 
Watu huru na Uhuru wa kupata habari pia uhuru wa taasisi , manispaa na Halmashauri ktk kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao ya kijiografia

Serikali Mpya kuweka mfumo thabiti na utaratibu kuzisaidia Idara zake za kiraia kufanya mabadiliko ya ndani kiutendaji ili kuziwezesha kuwatumikia watanzania bila ubaguzi na kwa haraka


Ndio wana siasa wetu hao halafu mnamsifia ni mtaalamu wa constitution wakati ameshindwa kubaini huko alipotoka muundo wa katiba yake ni federal (nchi zote zenye constitution ya aina hiyo ndio zinavyofanya mambo).

Sisi katiba yetu ni ‘unitary’ na nchi zote zenye katiba ya design hiyo ndio wanavyofanya mambo kama Tanzania; ni siasa ya A level aina ya constitution.

Mambo ya media censorship EU ndio usiseme kuna watershed hours, quota za vipindi vyao hasa national media nchi kama UK unakuta vipindi utakavyorusha 70% lazima viwe vimetengenezwa UK na control zingine kibao vunja kanuni ndio utamjua regulator wao ‘Ofcom’, ukienda France unakuta radio kwa siku airuhusiwi kupiga more than 15% ya mziki ambao lugha iliyotumika sio kifaransa.

Anacheza kwenye maswala ya censorship EU asikie tu, point ya msingi TRA ni tatizo na katiba raisi awezi kubaki na madaraka yote ifike siku yapunguzwe huko mbeleni.
 
6480B244-DA87-4A2E-B203-1F31DC0C6968.jpeg


Hizo ndio latest regulations ni cha mtoto kwenye censorship nchi za wenzetu siku uitwe kwenye press zetu hizi na mtu kama sheikh Ponda rusha tu malalamiko ya yake kabla ya kutafuta upande wa pili, au kama ilikuwa live usijaribu kufanya ivyo baadae halafu uone moto wake kutoka kwa regulator.

Ukija kwenye uandishi wa magezeti yetu ambayo yanafungwa unakuta nakala aina ushahidi wowote, kwa wenzetu mwandishi na kibali chenyewe unafutiwa.

Tanzania media zinachekewa bado sana kufikia uandishi wa habari wa nchi za wenzetu na hawako kwenye mstari kwa bahati kuna mbwa anan’gata ukijifanya unataka kuruka ukute.
 
Back
Top Bottom